Kiswahili kilibuniwa pia, sio lugha asili ya Mwafrika

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mara nyingi nimejikuta nikishambuliwa na wadau kwa ajili sisi Wakenya hupenda kutumia lugha zetu za asili pamoja hata na Kingereza. Watu wengi hupenda kuniambia kwa kutokutumia Kiswahili sana, ina maana mimi mtumwa. Ni muhimu ifahamike hata Kiswahili kilibuniwa tu kama Kingereza na sio lugha yetu ya asili. Jina Swahili linatokana na neno Sahil la kiarabu. Kiswahili kimechanganya humo ndani lugha nyingi, ikiwemo hata Kireno. Umuhimu wa lugha siku zote ni kuelewana, hamna cha utumwa wala nini.

Haya maneno hapa ya Kiswahili yaliotoka kwenye lugha ya Kireno

Dancador - DANGURO
Vinyo - MVINYO
Carta - KARATA
Copas - KOPA
Pao - PAU
Sete - SETI
Trunfo - TURUFU
Tabaquerra - TUMBAKU
Bibo - BIBO
Pera - PERA
Bandeira - BENDARA
Bomba - BOMBA
Boia - BOYA
Buli - BULI
Foronha - FORONYA
Caixa - KASHA
Copo - KOPO
Caraco - KOROSHO
Lenco - LESO
Mesa - MEZA
Padre - PADRI
Peca - PESA
Roda - RODA
Sapata - SAPATU
Sombreiro - SHUMBURERE
Trombeta - TARUMBETA
 
Kumbe maneno yakitoka kwa lugha ingine ndio inapoteza asiliye? Hayo uliyoyasema ni asilimia ngapi ya maneno yote ya Kiswahili?
 
hakuna jipya hapo..hiyo ni mojawapo ya nadharia ya chimbuko la Kiswahili...
 
Kumbe maneno yakitoka kwa lugha ingine ndio inapoteza asiliye? Hayo uliyoyasema ni asilimia ngapi ya maneno yote ya Kiswahili?

Hiyo ni mfano wa lugha moja ambazo zilihusika katika kukitengeneza Kiswahili. Humo ndani kuna hadi maneno yaliotoka kwenye lugha zetu za asili.
 
Kama kilibuniwa tu,
naomba utufafanulie,
lugha yetu ya asili ni nini?

tatizo unalochaganya wewe, ni kuchukua maneno yaliyosaidia kupata misamiati mingi ya kiswahili kupitia kwa wenzetu. jambo ambalo lilisababishwa na mwingiliano kati ya waarabu, waareno, n.k

Unafikiri ni kwa nini kati ya meneno uliyotaja hakuna hata moja neno la kichina.

kajipange upya hapa umechemsha
 
Punguza jazba halafu usome historia, kwanza fanya utafiti jina swahili kama nilivyosema limetokana na neno sahil la Kiarabu. Kiswahili kilibuniwa kama lugha ya kuwezesha Waarabu na Wabantu kuelewana katika maongezi. Mimi nakipenda ila ni vyema turekebishane, muache hizo kauli eti yeyote anayeongea Kingereza ni mtumwa ilhali hata Kiswahili sio lugha ya asilia kama Kinyakyusa, Kisukuma n.k.
 
Achana naye huyu mkenya. Ni limbukeni kweli kweli, halafu ni mkabila wa kutupwa. Atakupotezea muda tu. Bado anaishi gizani (maisha ya kale)!
 
Punguza jazba halafu usome historia, kwanza fanya utafiti jina swahili kama nilivyosema limetokana na neno sahil la Kiarabu. Kiswahili kilibuniwa kama lugha ya kuwezesha Waarabu na Wabantu kuelewana katika maongezi. Mimi nakipenda ila ni vyema turekebishane, muache hizo kauli eti yeyote anayeongea Kingereza ni mtumwa ilhali hata Kiswahili sio lugha ya asilia kama Kinyakyusa, Kisukuma n.k.

Tatizo, linalokusumbua wewe kumbe umekekereka na neno kuambiwa mtumwa,,,! sasa unatafuta jia ya kujifariji kwa kukishambulia kiswahili,

hauna lolote wewe!
 
Haya wacha nikuache, natumai atatokea mtu mwenye uwezo wa kujadili bila utoto.
 
kila kitu hapa duniani kimeubwa,
kiswahili nacho kiliubwa.
na kila kinachoubwa huwanga kina asali yake.

kiswahili ni lugha iliyoundwa na maneno ya kibantu pekee na kilikolezwa na meneno ya kiarabu kireno kingereza n.k, hali hii ilisababishwa na mwingiliano wa jamii hizi na waswahili,

nimekuuliza, ni kwanini maneno ya kichina, kikorea hayamo kwenye kiswahili.
 
Sijakataa Kiswahili kina maneno mengi ya Kibantu, lakini nasema chimbuko lake ni mchanganyiko wa lugha nyingi za asili pamoja na Kiarabu, Kifaransa, Kireno n.k. Sielewi unachouliza kwanini hamna Kichina ndani yake, hamna mahali nimesema lazima lugha zote za dunia zilihusika.
Kilitokana na wafanyi biashara ambao walitengeneza kitu tunaita kwa Kingerea "creole derivative" yaani lugha inayotokana kwa kuchanganya lugha kadhaa.
 
Huyu mkenya alipojiunga na JF alikuja na papara zake za kujifanya anajua sana kiingereza na eti sijui kiswahili ni lugha duni na kadhalika. Lakini waungwana tulimuweka kitako tukamuelimisha akatulia kidogo. Kwa sasa naona ugonjwa wake umemrudia anaanza kupayuka tena kwamba kiswahili siyo lugha ya Mwafrika. Jamaa boya!
 
asili ya kiswahili, ni wapi hapa duniani.

hayo maneno anayoyaongerea wewe, yana asilimia ngapi katka lugha ya kiswahili
 
Huyu mkenya alipojiunga na JF alikuja na papara zake za kujifanya anajua sana kiingereza na eti sijui kiswahili ni lugha duni na kadhalika. Lakini waungwana tulimuweka kitako tukamuelimisha akatulia kidogo. Kwa sasa naona ugonjwa wake umemrudia anaanza kupayuka tena kwamba kiswahili siyo lugha ya Mwafrika. Jamaa boya!

Najaribu kukupuzilia ila umekuamilia kama kupe. Tatizo lako ni kuwa huna uwezo wa kujadili chochote, hivyo siwezi poteza muda na wewe. Lugha zote ninaongea kulingana na ninayeongea naye, napenda lugha yangu ya asili, halafu hata na lugha za kubuniwa kama Kiswahili na Kingereza.
Kiswahili bado kina mapungufu mengi na siwezi poteza muda sana nacho haswa kikazi.
 
Eti "kiswahili kilubuniwa, na siyo lugha asili ya mwaafrika"

ukisoma hayo maneno uliyoandika kwenye kichwa cha habari, utangudua kwamba una mapugufu makubwa sana!

naomba unitajie asili ya kiswahili ni wapi,
hapa duniani
naomba unieleze ni lugha ngani hapa duniani ambayo haikubuniwa,,
.
 
Kumbe maneno yakitoka kwa lugha ingine ndio inapoteza asiliye? Hayo uliyoyasema ni asilimia ngapi ya maneno yote ya Kiswahili?

Ukiweka na yale ya asili ya kiarabu na kihindi...yanayosalia ni ya makabila mbalimbali pamoja na yanayotokea vijiweni. Si ajabu maana Tanzania yenyewe si imeanza juzi juzi tu. Kabla ya hapo watu walikuwa wakiishi kama isolated tribes or kingdoms wakiwa na lugha zao. Hicho kiswahili nahisi kilitokea baadaye sana, angalau kwa asilimia kubwa ya makabila ya watanzania. Sina hakika wale wa maeneo ya mwambao wa bahari ya hindi na visiwani walianza kutumia kiswahili lini.
 
Kiswahili kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria.kiisimu ni hoja za kisayansi ambazo huonyesha kila neno la kiswahili lina mzizi wa lugha za kibantu na mzizi ni shina la neno kwa kiingereza tunasema (stem)
 
Back
Top Bottom