Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa hamna cha aibu wala nini, tunajuzana, kabla ya Kiswahili Wapwani wote walikua na lugha zao.
Tatizo kubwa wewe linalokushumbua kwenye ubongo wako
ni kuchanganya kati ya watu waliosaidia kuenea kwa kiswahili, na asili lugha ya kiswahili,
kuna mifano mingi sana inayothibitisha kwamba kiswahili ni zao la kibantu.
lugha zote za kibantu zinafanana kimatumishi, kimantiki, kimaana, kimuundo, n.k.
lakn lugha ya kiaarabu ni tofouti kabisa na kiswahili
kimuundo,kimaana,kimuundo,na kimantiki. hata kimaandishi
| Swahili | Arabic | Meaning |
|---|---|---|
| hatari | خطر | Danger. Also the title of a 1962 movie starring John Wayne, set in Africa. |
| Safari | سفر | Travel. Also: trip |
| mahali | محل | Place |
| vitabu | كتاب | Book |
| msumari | مسمار | Nail |
| kata | قطع | Cut, chop |
| habari | خبر | news |
| huru | حر | free |
| dhamiri | ضمير | conscience |
| kamusi | قاموس | dictionary |
| baridi | بارد | cold |
| samahani | سامحني | forgive me, excuse me |
| rafiki | رفيق | companion, friend |
| tafadhali | تفضل | please |
| furahi | فرح | happy |
| Swahili | Arabic | Meaning |
|---|---|---|
| asubuhi | صبح | morning |
| dakika | دقيقة | minute |
| saa | ساعة | hour |
| wakati | وقت | time |
| alasri | العصر | late afternoon |
| magharibi | المغرب | sunset |
| alfajiri | الفجر | dawn |
| karne | قرن | century |
| Swahili | Arabic | Meaning |
|---|---|---|
| alkhamisi | الخميس | Thursday |
| ijumaa | الجمعة | Friday |
| Swahili | Arabic | Meaning |
|---|---|---|
| Tausi | طاوس | Peacock, being non-native to Africa, it took the Arabic name, which in turn took it from Persian. |
| Swahili | Arabic | Meaning |
|---|---|---|
| nusu | نص | Half. The proper classical Arabic word is نصف nisf. In many present day dialects it is "nus", like in Swahili. |
| robo | ربع | Quarter |
| sita | ستة | 6 |
| saba | سبعة | 7 |
| tisa | تسعة | 9 |
| ishrini | عشرين | 20 |
| thalathini | ثلاثين | 30 |
| arubaini | أربعين | 40 |
| hamsini | خمسين | 50 |
| sitini | ستين | 60 |
| sabini | سبعين | 70 |
| thamanini | ثمانين | 80 |
| tisini | تسعين | 90 |
| mia | مئة | 100. The middle letter in classical Arabic is Hamza, however, in present day dialects, like Swahili, it is a Y sound. |
| elfu | ألف | 1000 |
Kiswahili ni Kibantu.Hakuna lugha ambayo haijakopa maneno ya lugha nyingine. Hata hicho Kiingereza kina maneno mengi ya kilatini. Kiswahili nacho kina maneno toka Lugha mbalimbali. Kiswahili pia kina maneno ya Kiyahudi mf. Damu, mamlaka, maji nk. Lugha kuwa na maneno ya lugha nyingine ni kitu cha kawaida.
Maana ya neno hakufanyi kuwa jambo loote kuwa la Kiarabu, ndio Swahili ni neno lenye asili ya Arabuni, lakini vipi kuhusu lugha za pwani za kibantu ambazo ndizo zinazounda lahaja za Kiswahili? Mvita, Pate, Makunduchi, Unguja, Kilwa nayo ni maneno ya Kiarabu?Kaka naomba uanze na kutafuta maana ya neno Swahili, hapo ndio itakua rahisi kuelewana. Waafrika walikua na lugha zao.
Ndio Kikuyu ni mojawapo wa lugha za Wabantu. Historia inaeleza Wakikuyu tulitokea Magharibi mwa Afrika halafu tukashuka hadi Tanzania ambapo tuliishi kwa kipindi fulani na kuhamia hatimaye hadi Kenya.
I challenge you to name ONE language which has not borrowed words from other languages. Lugha haziishi kipekee. Watu wanaosema lugha hizo wanawasiliana na watu wa lugha mbalimbali na hapo ndipo wanapokopa maneno. Kwa hivyo kuleta orodha ndefu ya maneno ya Kiarabu au Kireno si ushahidi kwamba Kiswahili ni mchanganyiko.
Ukitaka kuangalia nasaba ya lugha hasa angalia muundo wake wa maneno, sentensi na virai. Kwa muundo tu wa maneno utagundua kwa Kiswahili na Kiarabu havina nasaba moja kabisa. Vitenzi vya Kiarabu vina mizizi ya konsonant tatu kwa mafano drs, ktb, nk na uambishaji hufanywa kwa kutumia ruwaza fulani zenye vokali zinazochomekwa kwenye mizizi hiyo ukapata kitu kama <daras>,<katab>, <duris>, <kutib>, nk. Mfumo huo upo katika lugha zenye nasaba na Kiarabu kama Kiyahudi, Kihabeshi, nk. Kiswahili, kwa upande wake, vitenzi vyake vinaundwa kwa mizizi yenye irabu na konsonant km -andik-. Na ukitaku kuambisha au kunyambulisha unaongeza vipande kabla na baada ya mzizi, unavitunga kama ushanga vile. Kumbuka Kiarabu kinachomeka viambisho. Huu ndiyo muundo wa Kibantu.
Tena angalia kitu kinachoitwa ngeli. Hizo hazipo kabisa katika Kiarabu. Na katika lugha za mchanganyiko wa lugha za Kibantu, km Kilingala, utaona kwamba ngeli ni chache zaidi. Lugha zenye historia isiyo ya mchanganyiko unaousema zina mfumo complicated wa ngeli. Lugha wanazodai zinatokana na mchanganyiko mara zote zinarahisisha vitu kama. Lakini kwa Kiswahili sivyo.
Ushahidi wa wana isimu na wanaakiolojia unatuonesha kwamba chimbuko la Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyozungumzwa pwani ya Kenya. Ni kweli imechukua maneno mengi ya watu wa kuja. Lkn hiyo si nasaba yake. Chunguza usitegemee maneno ya mtaani tu kutoa hoja ya vitu ambavyo unajua kwamba wengine lazima watakuwa wamevichunguza kwa makini.
Vipi unaikana lugha yenu. Inatakiwa ujivunie. Au una kinyongo kwa sababu ina asili ya pwani nawe ni wa bara? Disclosure: Mimi pia ni mtu wa bara huko Tanzania. Lugha yangu ya kwanza si Kiswahili. Lakini nazipenda lugha zote na sijaona sababu nzuri ya kuipuuzia lugha yoyote.
Tatizo kaka naona umedandia bila kufuata majadala wote ama hujanielewa
- Kwanza mimi Kiswahili nakipenda na kujivunia ila ni muhimu kuelezeana ukweli sio kupondana
- Tayari nilisema lugha zote zimeomba maneno kutoka kwenye lugha zingine, ila utakuta maneno haya ni ya kuongezea tu na sio ya msingi. Kila lugha ina maneno ya msingi kwa mfano saa na majira ya siku, hesabu yaani ukiangalia maneno ambayo Kiswahili kimeomba utajiuliza kwani kabla ujio wa hizi lugha zingine, kilitumika vipi hadi hata neno "damu" ni la kuomba, hata jina "swahili" ni la kiarabu.
- Nimesema kabla ujio wa Kiswahili, watu wa Pwani walikua na lugha zao. Sijabisha kwamba Wabantu walihusika pakubwa kukibuni lakini ifahamike kunazo lugha zetu za jadi ambazo ndio za msingi. Watanzania wengi hutuponda sisi Wakenya kila tukiongea lugha zetu za jadi, wanataka kila mtu aongee Kiswahili. Sisi Wakenya huwa tunahimiza sana uwezo wa ku
ongea lugha nyingi, zikiwemo hata Kingereza na Kiswahili pamoja na zetu za jadi.
Ni kweli asilimia kubwa ya maneno ambayo ni nomino (noun) yametokana na kiarabu na lugha zingine zikiwemo lugha za wabantu lakini maneno mengi ambayo ni vitenzi (verb) yametokana na lugha za wabantu na kwa uelewa wangu uti wa mgongo wa lugha ni vitenzi ndo maana kibantu kinapewa asilimia kubwa kuwa ndo asili ya lugha ya kiswahili.Ukizidisha utoto na matusi nitakuacha na kuwasubiri watu wazima waje tujadili, jifunze kujadili mada bila matusi. Lugha yoyote ya jadi humu duniani huwa haikopi maneno hata ya msingi. Kiswahili chenyewe kimekopa hadi maneno mengi sana ya msingi kama majira na nyakati.
Soma hii taarifa hapa
Introduction
Swahili is a language that fuses African Bantu with Arabic. Arab sailors and traders have established links and ties with East Africa for centuries, their language strongly merged with the local language to produce a creole derivative.
The word Swahili itself is derived from Arabic Sawahili سواحلي which is plural for ساحل meaning [Language] of the Coast.
This article gives some examples of Arabic words still in today's Swahili.
Here are some words.
Time
Swahili Arabic Meaning hatari خطر Danger. Also the title of a 1962 movie starring John Wayne, set in Africa. Safari سفر Travel. Also: trip mahali محل Place vitabu كتاب Book msumari مسمار Nail kata قطع Cut, chop habari خبر news huru حر free dhamiri ضمير conscience kamusi قاموس dictionary baridi بارد cold samahani سامحني forgive me, excuse me rafiki رفيق companion, friend tafadhali تفضل please furahi فرح happy
The terms for time are strongly influenced by Arabic. Many of it taken by the prayer times of Islam.
The Swahili names for the first five days of the week all start with Juma, then the order of the day of the week, Saturday being the first day of the week. Jumaa is derived from the Arabic word جمعة which means Friday, as well as "week. Only two days of the week got the Arabic names:
Swahili Arabic Meaning asubuhi صبح morning dakika دقيقة minute saa ساعة hour wakati وقت time alasri العصر late afternoon magharibi المغرب sunset alfajiri الفجر dawn karne قرن century
Animal Names
Swahili Arabic Meaning alkhamisi الخميس Thursday ijumaa الجمعة Friday
Animal names are all native African Bantu (e.g. simba lion). However, there are a few exceptions.
Swahili Arabic Meaning Tausi طاوس Peacock, being non-native to Africa, it took the Arabic name, which in turn took it from Persian.
Numbers
The number system is also heavily Arabic, although not exclusively so.
Swahili Arabic Meaning nusu نص Half. The proper classical Arabic word is نصف nisf. In many present day dialects it is "nus", like in Swahili. robo ربع Quarter sita ستة 6 saba سبعة 7 tisa تسعة 9 ishrini عشرين 20 thalathini ثلاثين 30 arubaini أربعين 40 hamsini خمسين 50 sitini ستين 60 sabini سبعين 70 thamanini ثمانين 80 tisini تسعين 90 mia مئة 100. The middle letter in classical Arabic is Hamza, however, in present day dialects, like Swahili, it is a Y sound. elfu ألف 1000
List of Swahili Words of Arabic Origin | The Baheyeldin Dynasty
Ni kweli asilimia kubwa ya maneno ambayo ni nomino (noun) yametokana na kiarabu na lugha zingine zikiwemo lugha za wabantu lakini maneno mengi ambayo ni vitenzi (verb) yametokana na lugha za wabantu na kwa uelewa wangu uti wa mgongo wa lugha ni vitenzi ndo maana kibantu kinapewa asilimia kubwa kuwa ndo asili ya lugha ya kiswahili.
"Kiswahihi Kilubuniwa, na siyo lugha asili ya afrika"
jamani naomba mtalamu mmoja tu, wa kiswahili anifafulize vizuri, maana ya hiyo sentesi,
maana kwa maana ya haraka haraka mleta uzi anamanisha
kuna lugha dunianin ambazo hazikubuniwa,
kiswahili kama siyo asili yake ni afrika, asili yake ni wapi?
ndugu yana lawmaina78 usipite bila kujibu hapa.
Nadhani mtoa mada anachomaanisha ni kwamba ukilinganisha hizi lugha kwa umri basi lugha za kibantu na lugha ya kiarabu ni lugha kongwe kuliko kiswahili. Na kama inavyojulikana kiswahili ni matokeo ya muunganiko wa maneno ya kibantu pamoja na kiarabu na lugha zingine ndo maana ametumia neno kubuni.
ukifuatilia majibu yake kuna sehemu nilimuuliza, maneno ya kingeni yana asilimia gapi? kwenye kiswahili ukilinanisha na maneno ya kibantu.,
akajibu maneno ya kibantu yako mengi
kwa maana hiyo kumbe ukichukua maji, ukachanganya kindogo na mafuta ya taa,
kwa hiyo maji yanakuwa mafuta ya taa, ili hali mafuta ya taa ni kindogo tu.
Mfano unaotoa hauhusiani kabisa, maana kabla hujachukua maji na kuyachanganya na mfuta, ina maana maji ylikuwepo kwanza. Lakini hapa mimi nasema Kiswahili hakikuwepo tangu jadi, kimebuniwa kwa kutumia maneno toka kwenye lugha nyingi duniani zikiwemo za Kibantu na za kigeni.
Ila hata hivyo labda hatukuelewana, Kiswahili asili yake Afrika, yaani kilibuniwa Afrika kwa usaidizi wa Waarabu ila sio lugha yetu ya asili (native), tunazo lugha zetu zilizotumika kabla hakijabuniwa.