Kiswahili kimeua lugha za asili za Watanzania kimya kimya

Kiswahili kimeua lugha za asili za Watanzania kimya kimya

Zama za matambiko zilishapita

Bravo Baba wa Taifa Hili Nyerere.

Pia jana nimeshtuka kusikia kuwa KISWAHILI NDIYO LUGHA YA PILI (2) AFRIKA KWA KUWA NA WAZUNGUMZAJI WENGI.

DUNIANI NI YA KUMI (10).
 
Nyerere alifanya vizuri sana nchi inahitaji lugha moja tu...ukitaka lugha ya kwenu rudi ukaishi kijijini..mjini ni kiswahili tu.nchi zote zilizoendelea wana lugha moja tu.

Mbona Rwanda na Burundi zina lugha moja na bado wanachukiana na masikini wa kutupa?
 
Katika mipango ya UNESCO nasikia hata engendered languages and cultures vinapewa kipaumbele. Hapa Tz tunawacheka wenzetu eti wana ukabila kwa kutumia kigezo cha kuongea vernaculars zao hadharani tena kwa kuzipenda wakati sisi tukiamini kuwa ni wamoja sababu sote tunaongea Kiswahili. Tulichosahau ni kwamba Mungu muumba nchi na mbingu ni mwenye mapenzi na anapenda viumbe vyote alivyoviumba ikiwa ni pamoja na lugha zao, right kama Mungu angelijua lugha ni mbaya basi asingeziumba! Patamu hapo.
 
Kaka sidhani kama upo sawa, naona kama unataka kuturudisha nyuma.
Dunia na inakati zinabadilika.
We call it Evolution, ambapo mazingira kiumbe anakuwa exposed ndio huamua kiumbe aweje,
Kama ukitaka hiyo dhana yako iwe practical ni pale maybe tuamue kila mtu arudi akaishi katika ardhi ya Kabila lake which is too awkward,
Mimi nawezasema haya mambo hutokea automatic kadiri nyakati zinavyoenda,

Familia huungana na kuwa ukoo- Kabila- Jamii -Taifa. Utaifa ni Mafanikio makubwa zaidi..

Kumbuka kuwa hakuna Mafanikio Makubwa zaidi katika Jamii zaidi ya Muungano,
Refer USA, RUSIA, UK, CHINA, INDIA,
Sasa kama Mungu alitujalia kiongozi wa kutuunganisha tena Kwa lugha Moja BOLD (Kiswahili) ambayo kwa sehemu kubwa ni Kibantu why not be proud of it?.

Hebu fikiria siku Moja Africa nzima iwe nchi moja inayozungumza Lugha Moja na Rais Mmoja na tuwe na Population Nusu ya Dunia,
Hatuwezi kuwa threat kwa Wazungu?
Narudia, we need to Unite, Unite and Unite to be powerful, Natumaini Kiswahili ndio Lugha pekee itakayoiungansha Africa hata kwa Miaka 100 ijayo.

Tokea lini mtu kuongea lugha yake ikawa ni kurudi nyuma? Kuniambia kuwa Kiswahili (hata jina lenyewe la lugha ni kiarabu) ni lugha yangu na kunikatisha tamaa kuongea lugha yangu ya asili haiwezi kuwa sahihi katika muktadha wowote.
 
Katika mipango ya UNESCO nasikia hata engendered languages and cultures vinapewa kipaumbele. Hapa Tz tunawacheka wenzetu eti wana ukabila kwa kutumia kigezo cha kuongea vernaculars zao hadharani tena kwa kuzipenda wakati sisi tukiamini kuwa ni wamoja sababu sote tunaongea Kiswahili. Tulichosahau ni kwamba Mungu muumba nchi na mbingu ni mwenye mapenzi na anapenda viumbe vyote alivyoviumba ikiwa ni pamoja na lugha zao, right kama Mungu angelijua lugha ni mbaya basi asingeziumba! Patamu hapo.

Watu hawaoni mbali wala hawajitambui, wanadhani kuongea lugha moja na kuua lugha nyingine ndio maendeleo.
 
Watu hawaoni mbali wala hawajitambui, wanadhani kuongea lugha moja na kuua lugha nyingine ndio maendeleo.
Kwa sababu ukiongelea maadili au values (virtues), hivi vitu vipo kwenye asili zetu na lugha ni spice muhimu sana katika kulinda asili! Hakuna kabila hata moja ambalo kwa asili linachochea chuki na kutopendana. Kuwa na attitude ya kushare mazuri kutoka kwa kabila lingine na kukataa mabaya ndio njia ya kuelekea upatano wa kweli!
 
Zama za matambiko zilishapita

Bravo Baba wa Taifa Hili Nyerere.

Pia jana nimeshtuka kusikia kuwa KISWAHILI NDIYO LUGHA YA PILI (2) AFRIKA KWA KUWA NA WAZUNGUMZAJI WENGI.

DUNIANI NI YA KUMI (10).
Safi sana watu wengi hasa wa bara wao wanaendekeza ukabila.ndio maana ushamba hauwahishi
 
Katika mipango ya UNESCO nasikia hata engendered languages and cultures vinapewa kipaumbele. Hapa Tz tunawacheka wenzetu eti wana ukabila kwa kutumia kigezo cha kuongea vernaculars zao hadharani tena kwa kuzipenda wakati sisi tukiamini kuwa ni wamoja sababu sote tunaongea Kiswahili. Tulichosahau ni kwamba Mungu muumba nchi na mbingu ni mwenye mapenzi na anapenda viumbe vyote alivyoviumba ikiwa ni pamoja na lugha zao, right kama Mungu angelijua lugha ni mbaya basi asingeziumba! Patamu hapo.
Nenda katambike huko na vijilugha vyenu huko.
 
Tokea lini mtu kuongea lugha yake ikawa ni kurudi nyuma? Kuniambia kuwa Kiswahili (hata jina lenyewe la lugha ni kiarabu) ni lugha yangu na kunikatisha tamaa kuongea lugha yangu ya asili haiwezi kuwa sahihi katika muktadha wowote.
Unataka kutambika?
 
Nenda katambike huko na vijilugha vyenu huko.
Umewahi kujiuliza maneno mapya ya Kiswahili yanatoka wapi ...si ni kwenye hivi vilugha!?
Je, unajua kuwa kamusi mpya ya Longman (sijui Oxford?) imetambua neno 'bodaboda' kama jipya kwenye English!?
 
lugha za asili hazifi. watz wengi tunaongea lugha ya asili ila kiswahili pia lazima.
 
Mkuu eka kuhufya wantuh uumu, tatamwia vyedi hata Bible tadaha kuzisoma, amba ne lugha ya kutambikia. MK254
 
Ni ukweli ulio wazi na usioonekana sasa miaka mingi ijayo makabila yetu yatakuwa duni sana, maana sasa hata ukienda Vijijini uwezi kuona tena ngoma zetu za asili, uwezi pata watu waliobobea katika kuelezea historia ya makabila au kabila husika na kama wapo ndio wanaishiria, ukiuliza baada ya wewe nani meingine ana hazina ya kabila hili jibu ni hakuna.

Makabila yetu ni fahari yetu, inapendeza unapoongea lugha ya asili, leo tuna vijana wengi tumesoma, tunasali, tunaishi nao ulimuuliza kabila atakwambia,mie mluo,mie mchaga, mie mnyakyusa,mie mmakuwa au mgogo au muha nk nk lkn ukitaka kuongea atakwambia sijui? Aliejitahdi sana atakwambia najua salam tu, nenda mbali umuulize kwenu ni mkoa flan sehemu gani asiposema sipajui atakwambia tunaendaga tu December sijui.

Hii ni mbaya sana kwa historia yetu. Na Msatakabali wa taifa letu, hatuwezi kuishia kujiita waswahili basi, inapendeza tunapoonesha na asili yetu.

Ndio maana kuna TOFAUTI kati ya mzanzibari na mjita, hawa wote wanaongea kiswahili lakini mmoja anaongea na lugha asili, tukikutana kwenye maharusi, radha inakuja unapoona watu wanacheza nyimbo za kwao. Wanakumbuka Nyumbani.

Tukipoteza kabisa makabila ya asili, tutapoteza mila zetu, tamaduni, miiko na desturi,maana hakuna mila za mswahili, wala miiko aghalabu mambo ya wazalamo ndio uhitwa ya kiswahili, sasa Je wote tunataka kubaki na mila na tamaduni za watu wa pwani? Ambazo ndio sana zinatambulisha uswahili.

Hoja hii ni muhimu, tuwekeze tena katika mila na lugha za asili, wala haitatufanya tuwe wakabila
 
Katika mipango ya UNESCO nasikia hata engendered languages and cultures vinapewa kipaumbele. Hapa Tz tunawacheka wenzetu eti wana ukabila kwa kutumia kigezo cha kuongea vernaculars zao hadharani tena kwa kuzipenda wakati sisi tukiamini kuwa ni wamoja sababu sote tunaongea Kiswahili. Tulichosahau ni kwamba Mungu muumba nchi na mbingu ni mwenye mapenzi na anapenda viumbe vyote alivyoviumba ikiwa ni pamoja na lugha zao, right kama Mungu angelijua lugha ni mbaya basi asingeziumba! Patamu hapo.
Kwanini unaweka UNESCO kama reference?
Who are they to you?
 
Tokea lini mtu kuongea lugha yake ikawa ni kurudi nyuma? Kuniambia kuwa Kiswahili (hata jina lenyewe la lugha ni kiarabu) ni lugha yangu na kunikatisha tamaa kuongea lugha yangu ya asili haiwezi kuwa sahihi katika muktadha wowote.
Can you tell me one, (only one) TANGIBLE thing I'll get after promoting my Beautiful Kihehe in Public ?
We don't need them as a Nation. Trust me.
Mimi naongea sana kilugha nikiwa home kijijini always. Lakini Kiswahili ni Muhimu zaidi.
 
Watu hawaoni mbali wala hawajitambui, wanadhani kuongea lugha moja na kuua lugha nyingine ndio maendeleo.
Lugha za makabila yetu zina mchango upi katika maendeleo? Hebu nidadavulie kidogo twende sawa.
 
huu ni wakati sasa kwa sheria zote zibadiliswe ziwe kwa lugha yetu ya kiswahili hili lina wezekana kwani lugha yetu imedhihirisha kuwa inakidhi, pia tuna wataalamu wa kutosha na weledi,

ni wakati sasa kwa mihimili yote na haswa Mahakama kutumia lugha ya kiswahili ktk taratibu zote za kutoa haki kwa mahakama zote hii itasaidia sana upatikinaji wa haki.
 
Back
Top Bottom