kiswahili kinabakwa nani akitetee

kiswahili kinabakwa nani akitetee

Joined
Jan 17, 2013
Posts
28
Reaction score
3
Natarajia vyombo vya habari ndio viwe dira ya kuonesha njia katika matumizi sahihi ya lugha, lakini ukisikiliza unakuta ni madudu matupu. mfano mdogo tu ni RADIO ONE! jioni huwa wanajiunga na BBC kipindi huwa kinaitwa dira ya dunia. lakini baada ya matangazo utasikia radio one wameweka jingo inayosema "ulikuwa unasikiliza kipindi cha bbc" ndio unajiuliza sasa kilpindi ni bbc au radio ndio bbc? je radio one hawajui kuwa ile ni radio ya bbc na kipindi cha jioni ni dira ya dunia na asubuhi ni amka na bbc? ni ujinga wa nani hapo mhalili au wote tu? si wote wanasikia madudu haya! wapi weredi hapa?
 
Ni kweli kabisa nachukizwa mno na matumizi yasiyo sah:hi ya lugha yetu, tena utasikia tokomeza zero badala ya tokomeza sifuri tunainyonga lugha yetu wenyewe
 
Natarajia vyombo vya habari ndio viwe dira ya kuonesha njia katika matumizi sahihi ya lugha, lakini ukisikiliza unakuta ni madudu matupu. mfano mdogo tu ni RADIO ONE! jioni huwa wanajiunga na BBC kipindi huwa kinaitwa dira ya dunia. lakini baada ya matangazo utasikia radio one wameweka jingo inayosema "ulikuwa unasikiliza kipindi cha bbc" ndio unajiuliza sasa kilpindi ni bbc au radio ndio bbc? je radio one hawajui kuwa ile ni radio ya bbc na kipindi cha jioni ni dira ya dunia na asubuhi ni amka na bbc? ni ujinga wa nani hapo mhalili au wote tu? si wote wanasikia madudu haya! wapi weredi hapa?

Hicho katika rangi nyekundu ni kitu gani?
 
Hicho katika rangi nyekundu ni kitu gani?

jingo ni sauti iliyorekodiwa na huwekwa mahususi kila baada au kabla ya kipindi au hata kati kati ya kipindi. mfano mmoja ni huo nimekupa baada ya kipindi cha DIRA YA DUNIA ambacho hurushwa na Idhaa ya kiswahili ya BBC kupitia radio one na RFA ukisikiliza mwisho wa matangazo hayo kwa radio one utasikia "ULIKUWA UNASIKILIZA KIPINDI CHA BBC" hiyo sauti ndio huwa inaitwa jingo! nadhani wameitohoa kutoka kwenye neno la kingeleza " JINGLE" ama mfano mwingine wa jingo ni kabla ya kipindi cha michezo cha radio one utasikia mziki malum na maneno "SPOTI LEO" na kale kamziki kataendelea kidogo na ndipo mtangazaji ataanza kutiririka na habari za michezo. bila shaka umenielewa. ila kwa kujiridhisha naomba usikilize radio One saa 12:30 jioni mwanzo wa matangazo utamsikia mtangazaji wa BBC akikitambulisha kipindi kuwa ni DIRA YA DUNIA na mwisho ataaga kwa kukumbusha kwamba kipindi kilikuwa dira ya dunia. kasheshe ni sekunde moja tu baada ya BBC kumaliza wanangia sasa WASWAHILI wamiliki wa kiswahili radio one WATANZANIA wanautia mchuzi maji "ULIKUWA UNASIKILIZA KIPINDI CHA BBC" huwa natamani KUMEZA NDALA! kwa machungu
 
Back
Top Bottom