Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,897
Kiswahili kinabanangwa na kuvizwa hasa na wasomi ambao huchanganyanya lugha ya kiswahili na kingereza makusudi wakijinaki kuwa wao ni wasomi,jamani eleweni kuwa kujua kingereza haimaanishi kuwa mtu amesoma,kingereza ni lugha yenye dhima sawa na nafasi sawa kama kiswahili,kidigo au kibondei.utasikia mtu anasema" i wish ningekuwepo nimcheki alivyo shine".eti huyu ni mswahili mzawa asiejua kiswahili kiasi cha kushindwa kutafuta kiswahili cha i wish,check,shine.wasomi wengi wana mawazo mgando na fikra potofu.kidumu kiswahili milele daima!
Kiswahili c kigumu ila waswahili ndio wagumu.hudhan kuwa kwa vile wamezaliwa wanaongea kiswahili basi wanajua kiswahili.ni lazma tujifunze kiswahili ili tuwe weledi.suala la tafsiri ni kwamaa hiyo ni taaluma inayojitegemea na c kila mtu anaweza kufanya,hvyo kuweka misamiati ya kisayans ya kingereza haimaanishi kua kiswahili hakina msamiati wa maneno hayo.ntakupa mfano maneno ya kingereza"download" na "upload" yanamaana ya KUPAKIA na KUPAKUA.maneno haya yamekuja baada ya ujio wa ngamizi{computer}.neno kama ANTIBODY lina neno la kiswahili FINGOMWILI.ukiangalia kiswahili ni tajiri ila waswahili wenyewe ni masikini wa lugha
sio suala la kujidai,manake hata wakati wa kusoma sekondari (o-level, manake sijui hata kiswahili chake), unajikuta english language una A, kiswahili una C. Kiswahili ni kigumu sana na tukiongea kiswahili kitupu sidhani kama tutaelewana,hasa kama tunaongelea sayansi ngumungumu. ni kujitahidi,lakini tusiwacheke wanaotohoa mkuu.
Kiswahili kinabanangwa na kuvizwa hasa na wasomi ambao huchanganyanya lugha ya kiswahili na kingereza makusudi wakijinaki kuwa wao ni wasomi,jamani eleweni kuwa kujua kingereza haimaanishi kuwa mtu amesoma,kingereza ni lugha yenye dhima sawa na nafasi sawa kama kiswahili,kidigo au kibondei.utasikia mtu anasema" i wish ningekuwepo nimcheki alivyo shine".eti huyu ni mswahili mzawa asiejua kiswahili kiasi cha kushindwa kutafuta kiswahili cha i wish,check,shine.wasomi wengi wana mawazo mgando na fikra potofu.kidumu kiswahili milele daima![/QUOTE]
Hapo juu, ndivyo ulivyoanzisha mada. Ulisema kuchanganya kiingereza na kiswahili na kujionesha usomi wetu.
Hoja na majibu yangu na ya wengine ni kwamba katika zama hizi, ni vigumu sana ukafanikiwa kuongea kiswahili kitupu na ukafikisha ujumbe uliokusudiwa kwa msikilizaji. Hii ni kwa sababu kiswahili kinaachwa nyuma na mambo mengi ya kimaendeleo, kisayansi, teknolojia, n.k.
Nikakupa mfano wa zile sentensi pale juu na maneno kadhaa. Wewe mwenyewe nafikiri ulichanganyikiwa kwa kukosa kiswahili chake.
Hebu sasa tembelea jukwaa la Science and technology hapa JF, utakuta vijana wanawasiliana na wanaelewa kitu inaitwa Symbian na android.
Wewe na BAKITA yako mtakapo ibuka kutuletea maneno ya kiswahili kumaanisha symbian na android, watu wengi watakuwa wameishazoea ya kiingereza. Sasa hapo tatizo liko wapi, mjomba pangu pakavu? Sio kwamba hatukipendi kiswahili, tunakipenda sana, ndio lugha yetu. Lakini kuwasiliana kwa kutumia kiswahili peke yake ni ngumu. Labda kama kuongea mambo ya kawaida tu ya kupika pilau na kushangilia mechi ya mtibwa na maji maji, hapo kiswahili kitupu kinaweza tumika
Nakushangaa na ntaendelea kukushangaa,tatzo ni kwamba wewe ni muhafidhina{consevative},mdhanifu{idealist} na una mawazo mgando kuhusu kisw{samahan cjakutukana}.umeweka sentens hapo juu halaf ukasema kua ukiongea hvyo watu hawatakuelewa,nadhan unakubal fika sasa kuwa kumbe kiswahili kinacho msamiati wa kutosha lakini waswahili hawakijui sawia kiswahili kias ambacho hukiona kigumu{ikiwemo wewe}.kwa hiyo hoja sasa ni kueleweka na sio tena kiswahili hakina msamiati toshelevu.nikushauri tu uwasiliane na wataalam km una uvulivuli wa mambo na si kuhukumu lugha kuwa ni ngumu.kumbuka kiswahili kina mlea binaadam tangu kuzaliwa kwake hadi kufa mf.ni ushairi simulizi hasa kipengele tanzu ya nyimbo.kuna nyimbo za kuzaliwa mtoto,nyimbo za kubembeleza mtoto"oooh mtoto oooh,babio kenda mjini kafungwa,kafungiwa debe mbili za mpunga...",nyimbo za mtoto ajifunzapo kutembea"...kasimama peke yake,amuonesha mchumba wake...",nyimbo za jando na unyago,nyimbo za harusi,na nyimbo za mazishi.ukiangalia mtiririko huu utaona kuwa lugha inabadilika kutegemea hitajio na mabadiliko ya binadam,nacho kiswahili kimefata mkondo huohuo.kutokujua kwetu kiswahili,tusihukumu kiswahili kigumu bali sisi ndo vchwa maji wa kisw.
Kama umenielwa pale juu, basi nafikiri utaacha kunishangaa, na kukubali kuwa wewe ndiye idealist. Mimi sikubaliani nawe kuwa sisi ni vichwa maji, labda wengine. Lakini mimi binafsi ninajijua na ninajua watanzania wengi ambao sote tuna uwezo mkubwa. Na hata sasa ninaongea lugha zingine mbali na kiswahili na kiingereza na lugha zetu za kimatumbi za bongo. Tunaposema kiswahili ni kigumu sio kwamba tukijifunza hatuelewi. Ugumu upo kutokana na kwamba kimeachwa nyuma na maendeleo ya jamii nzima ulimwenguni. Jamaa zako wa BAKITA walitakiwa kuwa na kimbelembele cha kuibuia misamiati mipya inayoendana na maendeleo duniani, na walitakiwa wahakikishe maneno hayo yanatumika na vyombo vya habari. Sasa leo hii, nikikuuliza neno BONANZA ni kiswahili au kiingereza, si ajabu utaniambia ni kiswahili, wakati sio. Sasa kwanini BAKITA wasitoe ufafanuzi kuwa Bonanza sio kiswahili na wala haimaanishi tamasha la michezo? Vijana wanaendelea kulitumia, almradi ujumbe unafika.
Mimi nilianza kusikia internet kimachalechale mwaka 1995 pale Dar, lakini nilikuja kujua neno mtandao miaka 3 baadaye, na nafikiri niliwahi kujuajua kwa sababu ya kuwa na tabia kufuatilia sana mambo ya kielimu watu wengine inawezekana waliendelea kwa miaka kadhaa bila kujua kuwa mtandao kwa wakati ule ulikuwa unamaanisha internet. Sasa kuna neno network, ambapo neno mtandao linaonekana ndio maana halisi ya network. We bwana, kiswahili ninakipenda sana lakini kinaachwa nyuma kama vifaranga vya bata. Na hiyo ndio sababu ya kuwa kigumu kueleweka.
hiyo yote ni kwa sababu ya kukiendekeza kiingereza
kichina ni kigumu kuliko kiswahili lakini kwa kuithamini lugha yao, kuna maprofesa kule hawajui hata kutamka good morning! na wachina leo hii wanatesa karibu kila eneo, sio teknolojia, biashara, uchumi, siasa, sanaa nk
kwa kweli kiingereza ni moja ya factors zilizotudumaza sana
Mimi nilianza kusikia internet kimachalechale mwaka 1995 pale Dar, lakini nilikuja kujua neno mtandao miaka 3 baadaye, na nafikiri niliwahi kujuajua kwa sababu ya kuwa na tabia kufuatilia sana mambo ya kielimu watu wengine inawezekana waliendelea kwa miaka kadhaa bila kujua kuwa mtandao kwa wakati ule ulikuwa unamaanisha internet. Sasa kuna neno network, ambapo neno mtandao linaonekana ndio maana halisi ya network. We bwana, kiswahili ninakipenda sana lakini kinaachwa nyuma kama vifaranga vya bata. Na hiyo ndio sababu ya kuwa kigumu kueleweka.[/B][/COLOR]
EMT.nawe una ugonjwa wa kuchanganya lugha ndo mana unaunga mkono.hatujakataa lugha kukopa,kila lugha duniani hukopa.hv muingereza akitaka kutamka kwa kingereza"BADA"ambao ni ugali wa muhogo,au BEMBE,SORO unadhan atafanya nn zaidi ya kutohoa maneno hayo kwan hayapo katika utamadun wake!ndo hapo lugha hukopa na kutumia maneno yenye asili ya lugha nyingine.maneno hayo yanapoingizwa kwenye kisw kwa mfano,hayawi tena ya kingereza au kiarabu bali huwekwa na kusanifishwa ili yaendane na sarufi ya kiswa.mfano syntax ni neno la kimombo linaposanifishwa linakua SINTAKSIA,hili neno jipya si kimombo tena bali ni kisw kwan neno sintaksia linafata kanuni za sarufi ya kisw na km ukimwandikia muingereza neno hlo{sintaksia}hawezi kuelewa kwa vile lipo nje na sarufi ya kingereza.
Hebu angalia ujumbe wko utaona ume2mia kingereza mahali ambapo kisw kipo na ungeeleweka vzr tu.angalia maneno AVOID,BORROW,LEXICAL BORROWING,BY THE WAY,MIX. hv kweli hatuna kiswa kinachoeleweka kwa maneno hayo.borrow{kukopa},avoid{kuzuia},mix{kuchanganya},lexical borowing{kukopa kileksika}.tafsiri hii ni kwa mujibu wa ulivyoyatumia maneno katika sentens zako.hivi ungeongea kisw usingeeleweka??c kila wakati kisw hakijitoshelezi,tuchanganye lugha ikiwa tu hakuna budi kufanya hivyo.kinyume chake 2nakiviza kisw cc wenyewe.TUSITAFUTE MCHAWI...
Hahahaha!c kweli ht kdogo mm naongea lugha zaid ya kingereza na kisw lkn sichangany kwa 7bu kila lugha ina miko yake.kwanini huchangany kingereza na kisw"i want to kutembelea that mbuga of animal at ngorongora mbuga ya nation"km ni kwel ulijifunza lg zote sambamba??mm si mdhanifu(idealist) ila u2mwa wa fikra ndo unaokutia uvulivuli.m2 chake bwana!
Hv hujui kisw cha "red" mkuu?hahaha!SISI NDIO 2NAOKIHARIBU,nlimanisha hvyo.neno kuviza linatokana na VIZA,ushawah kusikia"yai viza".sisi wamatumbi wa kibongo 2kipitapita shule 2natabu sn.hv ukiongea na bibi kule kijijin unachanganya na kimombo?hahaha
Mkuu kwa nini unaongelea tuu lugha za Kiswahili na Kingereza wakati suala hili lipo kwenye lugha zaidi ya hizo?
Mkuu kuhusu bibi yangu, naona tayari umeshafanya assumption au ku-generalise kuwa akina bibi huwa wanaishi vijijini tuu na pia huwa hawaelewi kimombo. Ndio maana nimekuambia wewe ni idealistic sana. Otherwise, utakuwa una-think backward. Mkuu sio akina bibi wote wanaishi vijijini. Pia sio akina bibi wote hajui Kingereza.