Kiswahili kumbe hakieleweki hata hapo kwa jirani Malawi, tunakikuza kuliko uhalisia, ni ajabu

Kiswahili kumbe hakieleweki hata hapo kwa jirani Malawi, tunakikuza kuliko uhalisia, ni ajabu

Ahaa.. shukrani mkuu
Mkuu nimesema lugha ya taifa ni kichechewa ila si wamalawi wote wanaojua vizuri kichechewa hasa hasa Northen Region kwa maana ya wilaya za mzimba,Rumphi,Nkata bay,Karonga,Chitipa na Khothakoto.Huko wanazumza Sana kitumbuka kuliko kichechewa
 
Ahaa.. shukrani mkuu
Kama unafanya biashara and you want to make money,fikiria kufanya biashara Malawi,kwa mfano shuka ya Masai ambayo tunainunua shillingi elfu kumi za bongo sawa na kwacha elfu tatu au nne za Malawi,ikishafika lilongwe bei yake ni Kati ya shillingi ellfu 24 na 45 za Tanzania,same to building materials
 
Tunapenda kujikuza kama tunavyosema Tanzania inajulikana duniani kote. Hapa ninapoishi ukiongea Tz wanafikiria Tasmania. Ukitaka wakuelewe ongea Kenya hapo wanajua unakotoka. Mimi huwa nauliza unaifahamu kenya, wakisema ndiyo basi unasema sisi ni jirani ila bado hawajui hata hilo jina. Wasomi wa zamani ukiwatajia Nyerere ndo wanakuwa na mwanga kuwa unatoka Africa au Tz. Jamani mnapokuwa nyumbani mkajiaminisha mnafahamika, mnajidanganya. Tanzania haijulikani labda nchi zilizopigania uhuru tu lakini nchi nyingine za Africa yawezekana hawajui hata Tanzania ilipo. We have nothing to be proud of. Kiswahili bado saaana.
Kuwa mzalendo na itangaze Tanzania hapo ulipo bila kujari kwamba ccm inatuharibia nchi.Njia moja wapo na rahisi ni kuhakikisha muda mwingi unavaa mavazi yenye asili ya Tanzania mfano Masai dress,t-shirt zenye jina la Tanzania au mbuga ya Serengeti au ngorogoro na nyumbani kwako na kwenye gari yako bendera ya Tanzania isikosekane.February mwaka huu nilipata marafiki wengi pale The empire State ( New York) just kwa kuvaa suka ya kimasai na kofia yenye jina la Seringeti
 
Nikikuonesha wamalawi wanaojua kiswahili itahalalisha mimi kudai kiswahili kimepanuka Afrika?

Makanisani utakuta mhubiri anaongea kiingereza na mkalimani anatafsiri kwa kiswahili. Ndio kusema umati wote haujui kiingereza?
Asilimia kubwa ya wamalawi waishio lilongwe na wilaya za jirani Kama vile Dowa,Nchitsi,Kasungu,Salima,Dedza,Ntcheu wasomi kwa wasiosoma wanajua kiingereza vizuri.So Kama Magufuli angekuwa anajua kiingereza angeongea kiingereza,ila kwa kuwa hajui basi hamna namna acha mkalimani afanye kazi yake,tusije ambulia kuchekwa siku tukienda huko bwana- sisi wengine tuna michepuko lilongwe eti
 
Mzee Kiswahili hakipimwi kwa kuongelewa sijui Marekani au Ulaya, hao wanajifunza lugha nyingi sana just for curiosity sababu ni wadadisi, Marekani wanajifunza hadi lugha za karne ya 10 ambazo zimepotea siku hizi na wanazitumia hadi kwenye movie, sembeuse Kiswahili..Wanajifunza vilugha vingi sana vidogo sio kuwa wanavihitaji bali ni katika tafiti zao na udadisi

Kiswahili kama kingekuwa kimekuwa kweli watu wangejifunza kwa kuwa wanakihitaji sio kujifunza for the sake of curiosity,

Waafrika wanaotuzunguka ndio watu wa kwanza wanaotakiwa kujua Kiswahili kama kweli Kiswahili kinapanuka, sio watu wa mbali huko ambao hatuna interaction nao
Hapa mkuu umedanganya!!

Kinachofanya lugha fulani kuwa international au kuwa lugha kubwa ni mambo mengi mojawapo n kiasi au idadi ya watumiaji kwa maana kwamba je kwa kiasi gan lugha hiyo inatumiwa hvyo kuwepo na watumiaji wa kiswahili kwenye hayo mataifa tajwa n sababu mojawapo au indicator mojawapo kuwa lugha hiyo imeenea na inazid kukua

Kingine n influence ya lugha hiyo kwenye sayamsi na teknolojia mfano simu nying sashv za androd nk zimewekewa mfumo wa lugha ya kiswahili

Sababu n nyng lakn cha kuelewa hapa n kwamba s kweli et wazungu wanafanya hvyo kwenye lugha yetu kwa ajili ya tafti hapana!!! Hiyo n sababu mojawapo lakn zipo sabab nyngne nyingi tuuu za mtu kujifunza lugha ya pili mfano n kama hyo yaan for research nk

Sababu nyingine n za kifamilia mfn wazaz wa Mtoto A wakahamia kwenye taifa X linalozungumza lugha 1 hvyo mtoto atalazimika kujifunza hiyo lugha kwa sabab hizo

Kingine n sababu tu za mtu kuamua kujifunza ,,kingne n sababu za kimasomo lazma ujifunze lugha ya pili sabab n nyng lakn cha kuelewa hapa n kuwa sababu za mtu kujifunza kiingereza n zile zile kama za kiswahili !!
 
Umeanza matusi tena mbona ulikua na mada nzuri tu?

Sawa twende hadi utaelewa.

Umesema wengine wanaojua kiswahili watakuepo ikiwa 50% of popn itakua inazungumza lugha husika.

Sasa umejuaje kama wote waliohudhuria hawajui kiswahili?

Ikiwa wapo/ watakuepo wanaojua kiswahili hiki ulichoandika ni sahihi?
We jamaa sijui kwa nini huelewi wakati nakuelezea hadi basi.
Sijasema hakuna wanaojua Kiswahili, ninesema kinafahamika na wachache sana ndio maana mkalimani akahitajika
 
Hapa mkuu umedanganya!!

Kinachofanya lugha fulani kuwa international au kuwa lugha kubwa ni mambo mengi mojawapo n kiasi au idadi ya watumiaji kwa maana kwamba je kwa kiasi gan lugha hiyo inatumiwa hvyo kuwepo na watumiaji wa kiswahili kwenye hayo mataifa tajwa n sababu mojawapo au indicator mojawapo kuwa lugha hiyo imeenea na inazid kukua

Kingine n influence ya lugha hiyo kwenye sayamsi na teknolojia mfano simu nying sashv za androd nk zimewekewa mfumo wa lugha ya kiswahili

Sababu n nyng lakn cha kuelewa hapa n kwamba s kweli et wazungu wanafanya hvyo kwenye lugha yetu kwa ajili ya tafti hapana!!! Hiyo n sababu mojawapo lakn zipo sabab nyngne nyingi tuuu za mtu kujifunza lugha ya pili mfano n kama hyo yaan for research nk

Sababu nyingine n za kifamilia mfn wazaz wa Mtoto A wakahamia kwenye taifa X linalozungumza lugha 1 hvyo mtoto atalazimika kujifunza hiyo lugha kwa sabab hizo

Kingine n sababu tu za mtu kuamua kujifunza ,,kingne n sababu za kimasomo lazma ujifunze lugha ya pili sabab n nyng lakn cha kuelewa hapa n kuwa sababu za mtu kujifunza kiingereza n zile zile kama za kiswahili !!
Simu zimewekewa lugha nyingi tu mkuu, ila haimaanishi hizo lugha ni kubwa sana kiasi hicho. Kwenye computer kuna hadi windows za Kizulu, sasa utasema Kizulu ni lugha kubwa? Si inaongelewa hapo South tu?

Hizo Android System za Kiswahili hajuna hata Waswahili wanazozitumia, wanatumia English version, sasa lugha ina ukubwa gani sijui hapo wakati hata natives speaker wake wanaiona ngumu
 
Hivi kuna ajabu gani wamalawi kutokuelewa kiswahili? Ndio ni jirani zetu lakini wana historia tofauti na sisi.
Naona mleta mada amekazania kuwa nchi ili isemekane kuwa inawazungumzaji wa lugha kama kiswahili wa kutosha eti wanaozungumza lugha hiyo wawe 50% sijui hii ameitoa wapi?
Nchi ambazo zinafahamika kuwa na wazungumzaji wa kiswahili ni Tanzania, Kenya, Uganda kiswahili ni lugha ya jeshini, Kongo-kiswahili ni lugha moja wapo kubwa katika top 5-kwa ukubwa wa nchi ile huwezi ukasema ni awchahche wanao zungumza kiswahili karibu ukanda wote wa mashariki hadi Lubumbashi. Burundi iko vizuri sana na Rwanda pia imo. Visiwani yaani Zanzibar ni nchi nyingine wasemavyo wao. Ukilinganisha na lugha nyingine za kiafrika ni wazi kiswahili kinazungumzwa na watu wengi zaidi ukiacha kiarabu kwa hiyo ni lugha kubwa. Na serikali ina kila sababu ya kupigia debe kiswahili na kuongoza kukikuza. Hivyo Raisi kuhutubia kiswahili kama ana mkalimani mzuri ni sawa tu. Siamini kama wengine wanavyotaka kutuaminisha kuwa JPM hajui kingereza.

Baada ya kuandika hayo yote ghafla mada ikaunganishwa na uwezo wa kiswahili kuwa lugha ya kufundishia. Mimi kwangu hili ni swala lingine kabisa. Lina uhusiano mdogo kwa sasa na kama kiswahili kiko kiasi gani nje ya mipaka yetu. Kinadharia sioni ubaya wa watu kuwa na shauku ya kutumia kiswahili toka primary hadi vyuo vikuu, lakini kiuhalisia kiswahili kina safari ndefu ya kufikia hapo. Sasa kuna wale ambao kula yao iko kwenye kupigia debe kiswahili (wanaona nafasi ya kula au ni wanasiasa wanaotuhadaa)-hawa wanakuza mambo kupita kiasi kama kama nchi hiyo ndiyo nia yetu basi tuwekeze kwenye kiswahili kwa muda mrefu (20 years say) tujenge lugha itakayo mudu kubeba masomo ya sekondari na vyuo vikuu na pia kupata walimu watakao tayarishwa kw kazi hiyo.

Kuhusu uhusiano wa kingereza na kiswahili-tukubali tu maamuzi (option) yetu sio kingereza au kiswahili bali ni kingereza na kiswahili. Serikali iwe na mkakati wa kupata walimu bora wa lugha hizi mbili. Huko kote yunako ambiwa wameendelea kwa kutumia lugha zao, tunafichwa ukweli kuwa lugha zao zinafundishwa sambamba na kiingereza au lugha kama hiyo. Na Hapa ndio raisi wangu JPM sikubaliani nae kwani ni zaidi ya mara moja amesikika akikiponda kiingereza au watanzania wanaofikiri kingereza ni muhimu.
 
Bahati mbaya hata jiografia ya Burundi huifahamu. Mpaka nafika Bujumbura nimepita mikoa na wilaya kibao na zote wanazungumza kiswahili.
kwa kuwa unatukuza cha kwenyu utasema hivyo, Burundi sijasema hawajui Kiswahili Kabisa, nimesema wanaojua sio zaidi ya 30%..
 
Mkuu ukiona mtu anaponda kiingereza kwa kujifanya Mzalendo jua huyo sio msafiri ndio maana hajui umuhimu wake na mtu anajifunza lugha za Nchi husika kama kuna vitu anafanya hapo ili kuweza kuwasiliana kwa urahisi na Raia wa hiyo Nchi...
 
Hivi kuna ajabu gani wamalawi kutokuelewa kiswahili? Ndio ni jirani zetu lakini wana historia tofauti na sisi.
Naona mleta mada amekazania kuwa nchi ili isemekane kuwa inawazungumzaji wa lugha kama kiswahili wa kutosha eti wanaozungumza lugha hiyo wawe 50% sijui hii ameitoa wapi?
Nchi ambazo zinafahamika kuwa na wazungumzaji wa kiswahili ni Tanzania, Kenya, Uganda kiswahili ni lugha ya jeshini, Kongo-kiswahili ni lugha moja wapo kubwa katika top 5-kwa ukubwa wa nchi ile huwezi ukasema ni awchahche wanao zungumza kiswahili karibu ukanda wote wa mashariki hadi Lubumbashi. Burundi iko vizuri sana na Rwanda pia imo. Visiwani yaani Zanzibar ni nchi nyingine wasemavyo wao. Ukilinganisha na lugha nyingine za kiafrika ni wazi kiswahili kinazungumzwa na watu wengi zaidi ukiacha kiarabu kwa hiyo ni lugha kubwa. Na serikali ina kila sababu ya kupigia debe kiswahili na kuongoza kukikuza. Hivyo Raisi kuhutubia kiswahili kama ana mkalimani mzuri ni sawa tu. Siamini kama wengine wanavyotaka kutuaminisha kuwa JPM hajui kingereza.

Baada ya kuandika hayo yote ghafla mada ikaunganishwa na uwezo wa kiswahili kuwa lugha ya kufundishia. Mimi kwangu hili ni swala lingine kabisa. Lina uhusiano mdogo kwa sasa na kama kiswahili kiko kiasi gani nje ya mipaka yetu. Kinadharia sioni ubaya wa watu kuwa na shauku ya kutumia kiswahili toka primary hadi vyuo vikuu, lakini kiuhalisia kiswahili kina safari ndefu ya kufikia hapo. Sasa kuna wale ambao kula yao iko kwenye kupigia debe kiswahili (wanaona nafasi ya kula au ni wanasiasa wanaotuhadaa)-hawa wanakuza mambo kupita kiasi kama kama nchi hiyo ndiyo nia yetu basi tuwekeze kwenye kiswahili kwa muda mrefu (20 years say) tujenge lugha itakayo mudu kubeba masomo ya sekondari na vyuo vikuu na pia kupata walimu watakao tayarishwa kw kazi hiyo.

Kuhusu uhusiano wa kingereza na kiswahili-tukubali tu maamuzi (option) yetu sio kingereza au kiswahili bali ni kingereza na kiswahili. Serikali iwe na mkakati wa kupata walimu bora wa lugha hizi mbili. Huko kote yunako ambiwa wameendelea kwa kutumia lugha zao, tunafichwa ukweli kuwa lugha zao zinafundishwa sambamba na kiingereza au lugha kama hiyo. Na Hapa ndio raisi wangu JPM sikubaliani nae kwani ni zaidi ya mara moja amesikika akikiponda kiingereza au watanzania wanaofikiri kingereza ni muhimu.
Umenisoma mkuu kiasi fulani, ninachosema Kiswahili ni lugha kubwa kweli ikilinganishwa na native languages nyingine za Kiafrika, nilichopinga ni hii promo inayopewa hasa kwenye vyombo vya habari kuwa imeenea kote Afrika na nje ya Afrika eti hadi wazungu wanaizungumza na kuwa hatuhitaji tena English sababu Kiswahili inaweza kuzungumzwa sehemu nyingi ikaeleweka
hili mimi ndio nalipinga...ndio nikatoa huo mfano wa malawi leo
 
Simu zimewekewa lugha nyingi tu mkuu, ila haimaanishi hizo lugha ni kubwa sana kiasi hicho. Kwenye computer kuna hadi windows za Kizulu, sasa utasema Kizulu ni lugha kubwa? Si inaongelewa hapo South tu?

Hizo Android System za Kiswahili hajuna hata Waswahili wanazozitumia, wanatumia English version, sasa lugha ina ukubwa gani sijui hapo wakati hata natives speaker wake wanaiona ngumu
Mkuu ni kweli lakn kutokuwa na muitikio chanya kwa wazawa haifanyi kiswahili kushindwa kukua na kuenea kwake ,,hulka ya wazawa wa taifa lolote lile kutopenda vyakwao ipo hata ukienda Ulaya hasa Uingereza ipo hivyo hii kawaida
 
Tunapenda kujikuza kama tunavyosema Tanzania inajulikana duniani kote. Hapa ninapoishi ukiongea Tz wanafikiria Tasmania. Ukitaka wakuelewe ongea Kenya hapo wanajua unakotoka. Mimi huwa nauliza unaifahamu kenya, wakisema ndiyo basi unasema sisi ni jirani ila bado hawajui hata hilo jina. Wasomi wa zamani ukiwatajia Nyerere ndo wanakuwa na mwanga kuwa unatoka Africa au Tz. Jamani mnapokuwa nyumbani mkajiaminisha mnafahamika, mnajidanganya. Tanzania haijulikani labda nchi zilizopigania uhuru tu lakini nchi nyingine za Africa yawezekana hawajui hata Tanzania ilipo. We have nothing to be proud of. Kiswahili bado saaana.
Uwe unajiita mkenya.

Hata hiyo kenya yako, wengine hawaijui vile vile. Kwani wewe tuvalu unaijua??? Ni nchi kubwa tu na inajulikana na wenye matumizi nayo.
 
Sasa wewe kuwasiliana na hao ndugu zako ndio kuwa DRC wanajua Kiswahili kwa 50% ? Unafikiri Congo au Burundi nzima ipo kwa hao ndugu zako?
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho zaidi
Hata tz hamna wanaojua kishwahili kwa akili zako.

Umeishafika kijijini kwenu,alikozaliwa baba yako!!!kiswahili kinazungumziwaje!!!
 
Kiswahili is overrated kabisa!

Ningekua Nyerere ningesema English iwe national language halafu lugha za makabila kila kabila libaki nazo zisipotezwe!

English ni bora maana ndio defacto world's language!

Ningefanya kama alivyofanya Lee Kuan Yew hapo Singapore!

Makabila yabaki,kila kabila liwe strong na mila na origins zake..Watu wakae na makabila yao kwa imani zao na mila zao bila kuingiliwa.

Sio Kiswahili kimekuja kimeua makabila mengine yote,watu hawana identity tena,wanabaki kua moderate loosers,hawapendi kwao walipotoka maana mizizi ya origins zao Nyerere aliziua tayari,wamebaki Watanzania wanotangatanga tu hawana origin of belonging!

International hatutoboi maana hatujui English na hapa nchini kwa kiswahili bado tunatangatanga hatuna origins tena!

Kwanini Wakenya ni wazalendo kupita maelezo kuhusu Kenya zaidi ya Watanzania na Tanzania yao?

Sababu ni kua,Wakenya wana ancentral lands zao zilizopo kenya na wapo emotionally attached nazo,Tanzania hakuna kabila hata moja Nyerere aliyaua for the sake of Kiswahili,watu wapo juu juu tu hawana belonging bora liende!

Hakuna ukabila maana mwanadamu mheshimu na kabila/origin yake,sio unaliua,unajenga taifa lenye mizizi feki!
Unaweza tangazia familia yako na mambo yakaenda vizuri tu, embu niambia ni kabila gani wahusika wamelitelekeza na kujiita waswahili.
 
Ukisikia kwenye vipindi vya Radio na Tv na mijadala mbalimbali jinsi Kiswahili kinavyokuzwa na huku Wakikiponda Kiingereza, utadhani Kiswahili ni lugha moja iliyoenea sana

Ila Kumbe ukienda nchi ambayo tunapakana nayo kabisa, Malawi hapo licha ya kuwa tume interact kwa miaka zaidi ya 55 sasa bado Kiswahili hakieleweki huko, Ushahidi ni hapo TBC, wanaongea English na kilugha chao, Magufuli mwenyewe ilibidi aongee Kiingereza na rais wao jana, na hata leo alipoona kuongea Kiingereza muda mrefu pengine itakuwa changamoto akaongea Kiswahili ilibidi kuwepo na mkalimani ili awatafsirie watu wa Malawi kwa Kiingereza..!

Kiingereza kinapondwa sana kuwa ni lugha ya wakoloni haifai lakini ndio lugha inayotuunganisha Waafrika, yaani sisi Majirani wetu wa karne nyingi hapo Malawi hatuwezi kuwasiliana pasipo Kiingereza, ukienda majirani wengine pia hapo Uganda, Zambia, Rwanda bado hutaeleweka na wengi usipozungumza Kiingereza

So tusijidanganye Kiswahili eti ni lugha kubwa wakati inazungumzwa na nchi moja na nusu tu..! Yaani Tanzania na Kenya, Kenya wanaongea English zaidi kuliko Kiswahili, habari zao na mijadala inaongelewa kwa Kiingereza kuliko Kiswahili, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii, Magazeti, Tv n.k wanatumia English kuliko Kiswahili

So Kiswahili kwa sasa ni kama lugha ya Tanzania tu na wala sio Afrika Masahariki achilia mbali Afrika ambako ndio baadhi ya watu wanasema

Tuachane na pride, tujifunze English.. Tukikuza Kiswahili chetu ni muhimu japo sijaona ushaishi wa Tanzania Kiuchumi au kiutamaduni utakaofanya Waafrika wengine wengi wakihitaji na kujifunza...

Sana sana wanaojifunza wanajifunza sio kwa kuwa wanakihitaji bali wanajifunza tu kwa udadisi kama amabavyo wazungu wanavyoweza kujifunza Ki Yoruba au Kichewa au Ki Twa

Tofautisha lugha inayokuwa kwa kasi na kuongelewa sehemu nyingi kwa upande wa lugha za Africa kiswahili ndio lugha rasmi inayojulikana kimataifa kusema malawi hawaongei sio kipimo kuwa kiswahili hakiongelewi nimekaa msumbiji provincial ya cabo delgado yote wanazumza kiswahili na cha kushangaza kuna miji ambayo ipo mbali na mpaka wa Tanzania na msumbiji wanazungumza kiswahili...juzi Roma wakati wa kujiandaa na pasaka chuo cha st. Anselm waafrica wanaosoma hapo waliamua kusali misa kwa kiswahili kama lugha pekee rasmi kutoka Africa...sào paulo Brazil nimeshuhudia watoto wakiimba kwa lugha tofauti duniani na wakaimba pia kwa kiswahili unataka lugha hii ikue kwa kiwango kipi? jivunie cha kwako then fanya tafiti kwanza kabla kusema jambo fulani
 
Kuwa mzalendo na itangaze Tanzania hapo ulipo bila kujari kwamba ccm inatuharibia nchi.Njia moja wapo na rahisi ni kuhakikisha muda mwingi unavaa mavazi yenye asili ya Tanzania mfano Masai dress,t-shirt zenye jina la Tanzania au mbuga ya Serengeti au ngorogoro na nyumbani kwako na kwenye gari yako bendera ya Tanzania isikosekane.February mwaka huu nilipata marafiki wengi pale The empire State ( New York) just kwa kuvaa suka ya kimasai na kofia yenye jina la Seringeti
Hawezi mchawi huyo, haya ndio menzetu likiwa nje huko limezubaa kama mhindi uliolala[emoji16][emoji16][emoji16].

Full unyonge kama kamwagiwa maji, anasubiri magu atajwe aanze kusiliba.
 
Asilimia kubwa ya wamalawi waishio lilongwe na wilaya za jirani Kama vile Dowa,Nchitsi,Kasungu,Salima,Dedza,Ntcheu wasomi kwa wasiosoma wanajua kiingereza vizuri.So Kama Magufuli angekuwa anajua kiingereza angeongea kiingereza,ila kwa kuwa hajui basi hamna namna acha mkalimani afanye kazi yake,tusije ambulia kuchekwa siku tukienda huko bwana- sisi wengine tuna michepuko lilongwe eti
Hawawezi wakawacheka, kisa rais kaongea kiingereza kibovu sababu wao sio wajinga kama nyinyi.

Maana hapa pia mnaponda rais kuongea lugha yake.
 
Mkuu ukiona mtu anaponda kiingereza kwa kujifanya Mzalendo jua huyo sio msafiri ndio maana hajui umuhimu wake na mtu anajifunza lugha za Nchi husika kama kuna vitu anafanya hapo ili kuweza kuwasiliana kwa urahisi na Raia wa hiyo Nchi...
Utashindwa kuishi marekani sababu hujui kiingereza!!!! Au wewe mwenzetu ndio husafiri[emoji16][emoji16]
 
Hata tz hamna wanaojua kishwahili kwa akili zako.

Umeishafika kijijini kwenu,alikozaliwa baba yako!!!kiswahili kinazungumziwaje!!!
Basi kumbe ni tatizo zaidi kumbe, hata Tz Kiswahili hakiongelewi na Watz wote
 
Back
Top Bottom