Baada ya kusahau nywila(password) ya kadi
yangu ya kiotomotela(ATM) nikaamua kukaa
mgahawani (restaurant) jirani na kilipo
kiotomotela (ATM) na kuagiza vibanzi (chips)
vikavu na sharubati (juice) baridi sana!
Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua
tarakilishi mpakato (laptop) na kujaribu
kufungua diski mweku (local disk) iliyogoma
kufunguka kwa wakati huo. Nikafungua diski
tepetevu (floppy disk) na kukuta imevamiwa
na mtaliga(virus). Nguvu ikaniishia,
nikashindwa hata kushika wala kupalaza
kisharazio(cursor) cha tarakilishi yangu. Siku
yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau
hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.