Baada ya kusahau nywila (password) ya kadi yangu ya kiotomotela (ATM) nikaamua kukaa mgahawani (restaurant) jirani na kilipo kiotomotela (ATM) na kuagiza vibanzi (chips) vikavu na sharubati (juice) baridi sana!
Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua tarakilishi mpakato (laptop) na kujaribu kufungua diski mweku (local disk) iliyogoma kufunguka kwa wakati huo. Nikafungua diski tepetevu (floppy disk) na kukuta imevamiwa na mtaliga(virus). Nguvu ikaniishia, nikashindwa hata kushika wala kupalaza kisharazio(cursor) cha tarakilishi yangu. Siku yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.