1. KOKO HAIDARI MAI
Hiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji".
Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.
2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)
Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.
Kapa ni aina ya kanzu isio na mikono
Usubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma.
3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)
Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.
Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.
4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Kamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.
Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.
5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Hata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangio
Ikimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.