WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Asiyejua maana haambiwi maana.
Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi
kusema ukweli vinanichanganya kati ya nahau, methali na misemo.
Fuata nyuki ule asali
tembea uone
NDIO HAPO SASA!
Methali ni proverbs au?
na Nahau ni idiomatic expressions..au mnasemaje wajuzi wa lugha?
asante mkuu, yani mie ndio kiazi wa both.... nimejua rasmi kwamba ujanja wangu ni kuunga-unga sentensi tu... nothing more!!!Nimeamini kuwa ni kweli mimi sijui kiswahili wala kiingereza. Na lugha ya kwetu milimani nayo haipandi.
Aibu tupu!
Ah!, hii imekaa vyema! nashukuru mkufunzi!3. Mchama ago hanyeli huenda akawia papo.
Mchama = kuchama (mtu)=kuhama (mtu)
Ago= (?)
hanyeli= hanyi (halinyei)
akawia= kuwia= kurejea
Papo= hapo hapo
Anaehama pahala hatakiwi apanyee kwa kuwa inawezekana akarudi hapo hapo. Au kwa kiswahili cha siku hizi ni kuwa usipaharie pahala kwa sababu unahama kwa kuwa unaweza ukarejea hapo hapo 🙂
Wakuu nisaidieni kujua maana ya methali
1. KOKO HAIDARI MAI
2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI
3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO
4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Nitajaribu namba nne na tano;
4)Mbachao ni mkeka kuukuu . ambao unautumia kwa shida naraha,lakini huo
msala ulioazima kwa jirani yako utautumia muda mfupi tu kwani mwenyewe atauhitaji baadaye
hivyo itabidi uurudishe.
5)Kwa wale wa vijijini wanaotumia jiko la kuni lenye mafiga matatu wataelewa vizuri mfano huu
wewe unapika mfano chakula kwenye hilo jiko la kuni, umewasha moto umetoka kidogo
kwenda anakuja mtu nyuma anazima moto na anatoa kuni., hivyo unachopika hakitaiva.
hii inaonya kwamba kuna fitina nyingi katika jamii zetu, watu hatutakiani mema.
asante1. KOKO HAIDARI MAIHiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji". Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.Kapa ni aina ya kanzu isio na mikonoUsubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma. 3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAOKamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAEHata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangioIkimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.
1. KOKO HAIDARI MAI
Hiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji".
Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.
2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)
Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.
Kapa ni aina ya kanzu isio na mikono
Usubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma.
3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)
Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.
Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.
4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Kamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.
Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.
5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Hata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangio
Ikimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.
msala nayo maana yake nini!?? au ni mkeka mpya?
5. Please hebu dadavua zaidi kiasi, mimi nimeshatumia jiko la kuni ila bado sijakunyaka vizuri mkuu!
Shukran sana Mkuu1. KOKO HAIDARI MAI