Wakuu, nimeulizwa ghafla na mtu ambaye hakijui vema kiswahili maana ya neno SHUBIRI kwani aliambiwa kuna dawa chungu kama shubiri hakuelewa shubiri ni nini kwa kiswahili wala kiingereza, binafsi nimechemsha!
Naweza kueleweshwa maana yake?
Nimeenda hapa sikupata msaada:
shubiri
Mkuu ushasema kuwa Shubiri ni dawa sasa unataka tafsiri gani tena?
Labda maelezo ya matumizi yake. Shubiri utumiwa kwa wenye kusumbuliwa na maradhi ya ngiri. Dawa chungu sana mfano wa qunaine.
Nakumbuka kuna shairi moja (la Saleh Barkey) limetumika neno hilo shubiri, kwa wale wanagenzi wa kiswahili. Shairi linasema hivi:
Wendavyo huna sumile, huyajali ya njiani
Vikwaruzavyo vitele, waona hujulikani
Huchwi kufungwa kengele, masikini wa rohoni
Siwatajii mchawi , mfumbuweni fumboni
Ulopewa ni
shubiri, pima yakuhusu nini
Ukatamba una ari, umeushika mpini
Waona umevinjari, kumbe uko ukutini
Simfichui mchawi, mtambuweni fumboni
Ngoma hiyo ya kitoto, haikeshi asilani
Kujipulizia joto, raha yake raha gani
Umejitweka mazito, kwa kutaka ubishani
Mchawi hasemwi jina , nawatajia fumboni
Hapa neno Shubiri, lina maana ya umbali au (pima) ni kipimo cha nchi kama tisa hivi.