...and with reference to
this post of yours if you don't mind Pundit, can you pls further explain why it's doomed, particularly the Internet. Thank you.
Kwa sababu, you just don't create a product that has no demand, or very little demand.Kama watu wanataka kufanya hii project kama academic exercise au cultural enrichment of the internet that's fine, but it is an impractical goal that will cost more than it is worth.
Wengi wa watumiaji wa mtandao tayari wanajua Kiingereza cha kutosha ku get around (ndio hao hao wanaotafsiri) na wachache wasiojua Kiingereza, hicho kiswahili cha IT cha "taradishi" na vikorokoro vingine kama hivyo vitawazingua zaidi ya kiingereza, angalau kiingereza kuna maneno yanajulikana lakini wao hawayajui kwa hiyo wanaweza kuwauliza wenzao, kiswahili unaweza kukutana na maneno ya IT ukakuta hamna hata mtu mmoja anayejua.And these are the kind of people that do not even know that The Kamusi Project exist, or that Google is your friend.
Kwa hiyo hii effort ni nzuri, lakini kwa sasa itaishia kama feature nzuri sana ya Microsoft Word ambayo hutumiwa o.oo1 percent of the time. Mpaka utakapokuwa na hadhira ya kutosha, mpaka utakapokuwa sio tu na umeme pamoja na internet vijijini, bali pia na compyuta pamoja na purchasing power ya kuiwasha hiyo computer na kuiunganisha kwenye internet, audience mnayoifanyia kazi haipo, na sijui kama itapata internet access maishani mwangu.
Besides, audience hiyo ingekuwa inajua kiswahili labda tungeweza kusema mnafanya maandalizi, lakini sasa hivi hata hiyo audience yenyewe Kiswahili haijui. Kiswahili as a coherent language is under the threat of extinction -with the exception of some pockets in Zanzibar, Mrima and Mvita-
Speaking of Mrima and Mvita, which lahaja are you going to write in? Or are you going to butcher Kiswahili with "papo hapos" a la the good book?
These are the apparently insurmountable challenges, they need not hinder your process -and in no way did I mean to project cynicism- but I just saw these as challenges, prove me wrong by having a Yahoo type content rich heavy traffic portal.
Nchi zote zenye kutumia lugha zao kwa sana kwenye IT na internet zina either literacy levels za juu sana, au uchumi wa juu sana, nyingi zina vitu viwili hivi pamoja.Kabla hatuja vi address hivi pamoja tutakuwa tunawatafsiria wazungu na watu wengine wanaotaka kujifunza kiswahili pamoja na sisi wenyewe, ndiyo mambo ya 0.0001 percent hayo.
Back in 03 I was talking to Brian Greene, the celebrated Columbia profesor and author of the bestselling "The Elegant Universe" he was all for it, but I was asked, was there a demand? I had to be frank with myself, ningetafsiri ningemtafsiria nani? Kile kitabu na ma concept yake ya high and mighty particle physics ambayo mengine hata katika kiingereza ndiyo yanapatiwa manenono kingeeleweka katika kiswahili au ushabiki tu? Na je, ningeweza kutafsiri, watu ambao wangekuwa interested kukisoma katika kiswahili si ndio hao hao wenye uwezo wa kukisoma kiingereza? Na watu ambao hawajui kiingereza probably wasingejua mambo mengi ambayo ni background knowledge ambayo muandishi hawezi kufafanua kwa kujua ni kama prerequisite fulani, je unaweza kumuelewesha mtu jinsi gani relativity ilivyokuwa revolutionary kama hawajui Newton na Einstein na the progression that happenned there?
Kwa hiyo unaweza kukuta hili kuwa practical likawa swala la uchumi na literacy zaidi kuliko content.