Ndugu, naomba mnipatie tafsiri au ufafanuzi wa neno 'thread' kwa kiswahili kama itumikavyo kwenye forum hii.
Je,neno jarida/daftari/ukurasa yanaweza kufaa kama tafsiri yake ya kiswahili?
Nyongeza; kwa sababu nauliza swali hii karibia na mwisho wa juma kuanza na kwenye shamlashamla za Eid, nawasihi basi kwa wale wepesiwepesi wa kuchombeza na maneno kuwa tayari nimeshafikiria neno 'kamba' na 'uzi' na nafikiri hayafai kuwakilisha neno thread kama litumikavyo kwenye forum hii. Ahsanteni.
SteveD.
Neno
thread, km kitenzi (verb), linamaanisha pia
tunga (to thread - kutunga). Kwa mfano,
tunga uzi ktk sindano, au
tunga shanga. K/hiyo, thread, km nomino (noun), linamaanisha
mtungo. Kwa mfano, mtungo wa shanga.
Kwa kuwa mtungo (mmoja), km wa shanga, ni
mfululizo wa vitu vingi kwa pamoja vilivyotungwa (km shanga nyingi kwa pamoja, ktk mfano wetu), basi
new thread humaanisha
mtungo mwingine/mpya, au
mfululizo mwingine/mpya. Na km kunaongezwa kitu ktk mtungo (km kuongeza shanga kadhaa), basi kuongezwa huko tutakuita
mwendelezo/muendelezo wa mtungo/mfululizo.
Hivyo ndivyo kadri nijuavyo.
Ndugu, SteveD, angalia maneno niliyoyawekea wino mwekundu hapo juu. Nadhani yangepaswa kuwa:
karibu,
shamrashamra,
maneno.