Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 31
Nadhani hilo neno kwa kiingereza ni provided that-ilhali kwamba.Hata hivyo nitafanya utafiti kwenye vyanzo vyangu na kujua linatunikeje katika muktadha mbalimbali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wee umetuibia turudishie chenji whereas maana yake Kwa kuwa na sio ilhali.Samahani, lakini nadhani kwamba "provided that" ni "ilimradi" (au 'alimradi'), "mradi", "isipokuwa kama". Maana ya "ilhali" ni "whereas".
!!!!!!!!!!wee umetuibia
turudishie chenji whereas maana yake Kwa kuwa na sio ilhali.
Epi Nyu Ia tu Oll
Tafadhali chunga unapobadili neno linavyoandikwa, kwa mfano umeandika "munkali", hilo si neno sahihi au umelikosea spelling kwa hiyo halileti maana yoyote. Nadhani ulitaka kutumia neno munkar.Nino,punguza munkali jf ni sehemu ya vimbwanga pia ukiachilia majibu tunayopeana.Niliposema umetuibia sikumaanisha mwizi,ni moja ya lugha ya vijana ya kudadisi jibu au hali fulani ili kupata maelezo(chenji) zaidi toka kwa muhusika.au tukisema hapa turudishie kiingilio chetu tuna maana hatujakubaliana na wewe tushawishi zaidi.Huko ni kukua kwa lugha na tamathali za semi.Labda basi tufanye neno ilhali nalo ni kwakuwa manaake katika tafisiri nyingi zilifofanyika ikiwamo tafsiri ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania na mikataba mingi neno whereas linatafsiriwa kama KWAKUWA.Na ndio maana katiba kwenye utangulizi imeanza na neno KWAKUWA SISI yuaani WHEREAS WE, the people of ....Ok, hivyo ndivyo navyoelewa japo bado utafiti haujafungwa.
Bila samahani, kwani kiswahili ni lugha inayokuwa kwa haraka sana kwa uchanga wake na kusambaa kwake, inawezekana neno "munkali" lipo nami silijuwi. Nilijuwalo mimi ni munkar(i).Samahani, Zomba, ninavyojua mimi "munkari" ni kisawe cha "kitu kibaya, kitendo haramu, jambo ovu". Lakini watu kadhaa hutumia "munkali" kama kisawe cha "hasira", tazama hapa: Mzee Cheche alisema kwa ghadhabu,kitendo kile kilimpandisha hasira Mode na kujikuta akimvaa Jose,ambaye hakukubali wakaanza kupigana. Ilibidi mzee Cheche awe mpole ili kupunguza munkali wa Mode
"Mode ninyi wote ni wapenzi wangu usiwe na hofu utapata kile ulichokikosa" http://maisha.co.tz/kurasa.php?soma=sukari&habariNamba=641
Unaonaje?
Mwishowe, uliandika "... hiyo inachafuwa...". Je, ulitaka kuandika "inachafua"?
Asante sana.
Bwana mmoja hapa kasema eti thread ni utepe lakini la thread ni Uzi na utepe ni 'Tape', n kwa issue ya thread kama hizi za JF naonelea ziitwe 'nyuzi' kama ingewezekana. na mimi naulizaje Matongo kwa Kiingereza yaitwaje.....wanugu ebu niambieni....KTY (kwa taarifa yenu) nchi jirani kenya Nugu ni aina ya sokwe....lol
Millipede nadhani huitwa jongoo naye centipede huitwa ninii?
tandu Ndo Yule Mwenye Miguu Mingi Na Ku-sting Kama Nge?