KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

OOh Steve D
Mambo vipi asante kwa shukrani zako nimezipokea. Wajua jana baada ya kukupa ile tafsiri niliendelea kufanya utafiti juu ya zile istilahi kupata maana hasa halisi itakayoleta mashiko katika lugha na mfumo mzuri wa matamshi kwa kutumia mbinu mbalimbali,maana nzuri ya maneno uloniuliza ni haya
Analog = analoji,
Boolean Algebra (boolean logic), = aljebra ya Buli,(mantiki ya buli)
Logic gate,= geti mantiki
Microchip, = chipu katiti
Integer data, = data ya namba kamili
Vector, = vekta
Electronics, = elektroniki
Digital electronics, = elektorniki za kidijiti
Function (mathematical function), kadhia ya kihisabati
Boolean function, kadhia ya Buli
BIT, = BITI
Byte,= baiti
Variables (as in programming)= kigeu
Binary numbers,= namba cheuzi
Octal numbers, = namba za okto
hexadecimal numbers, = namba za heksadesimali
Asante sana nadhani maana hii itafaa zaidi
Augustus
Mwanafunzi
Chuo Kikuu cha Essex
Uzamili katika Biashara za Kimataifa(LLM in International Trade Law)
Colchester
Uk
 
Well,sijui hapa linatumikeje lakini neno thread ni utepe au uzi mwembamba.ngoja tuzame zaidi twaweza pata maana nzuri zaidi
 
Mmmh hapana si mwalimu wa kiswahili, fani yangu ni sheria ila nakipenda sana kiswahili,na mara nyingine nimefanya tafsiri kadhaa,kwa kushirikiana na TUKI.Nakijua kiswahili japo kiaina kwa kuwa kidato cha tano nimesoma HGK pale Mkwawa na mwalimu wangu si haba alikuwa mzuri. Naam yupo Makongo sasa,walimwiba.
Kwa ufupi ni hivyo.
 
Maskini ana nafuu zaidi kwani masikini ni poor wakati fukara ni pauper,anayeishi kwenye abject poverty(umasikini uliokithiri)
 
Neno thread, km kitenzi (verb), linamaanisha pia tunga (to thread - kutunga). Kwa mfano, tunga uzi ktk sindano, au tunga shanga. K/hiyo, thread, km nomino (noun), linamaanisha mtungo. Kwa mfano, mtungo wa shanga.
Kwa kuwa mtungo (mmoja), km wa shanga, ni mfululizo wa vitu vingi kwa pamoja vilivyotungwa (km shanga nyingi kwa pamoja, ktk mfano wetu), basi new thread humaanisha mtungo mwingine/mpya, au mfululizo mwingine/mpya. Na km kunaongezwa kitu ktk mtungo (km kuongeza shanga kadhaa), basi kuongezwa huko tutakuita mwendelezo/muendelezo wa mtungo/mfululizo.
Hivyo ndivyo kadri nijuavyo.

Ndugu, SteveD, angalia maneno niliyoyawekea wino mwekundu hapo juu. Nadhani yangepaswa kuwa: karibu, shamrashamra, maneno.
Tanzania 1,
Nashukuru sana kwa huo mwangaza na masahihisho.
Analog = analoji,
Boolean Algebra (boolean logic), = aljebra ya Buli,(mantiki ya buli)
Logic gate,= geti mantiki
Microchip, = chipu katiti
Integer data, = data ya namba kamili
Vector, = vekta
Electronics, = elektroniki
Digital electronics, = elektroniki za kidijiti
Function (mathematical function), kadhia ya kihisabati
Boolean function, kadhia ya Buli
BIT, = BITI
Byte,= baiti
Variables (as in programming)= kigeu
Binary numbers,= namba cheuzi
Octal numbers, = namba za okto
hexadecimal numbers, = namba za heksadesimali
Asante sana nadhani maana hii itafaa zaidi
Augustoons, Hapo juu kwenye 'digital electronics' naona kama kuna utata vile, maana hapo awali ulisema digital ni tarakimu/tarakinishi au basi kufanana na hivyo. Lakini hapo juu umeweka 'dijiti', kuna nakala moja ya gazeti linalopatikana kwenye IppMedia.com lilitumia neno 'dijito' kuwakilisha digital; sasa miye ndiyo maana nikaja na neno langu jipya la 'puru', kwa sababu tu makusudi, maana tukizidi kuyanyambulisha haya maneno kutoka kiingereza saa nyingine tutaanza kujichanganya wenyewe.

Tunakubaliana kabisa kuwa haya maneno yanatoka kwenye lugha za kigeni na hayana asili ya lugha zetu za Kibantu. Ni kweli katika nyanja mbali mbali kitaalam maneno haya yanakuwa yametokana na lugha ya Kilatini, hivyo lugha nyinginezo zinavyo yatumia huyarekebisha tu lakini asili yake inabakia. Utata ni kuwa hapo hapo tuna tungia maneno mapya vitu kama 'wavuti' 'luninga' n.k. kama vile ilivyo onekana kwenye project ya Microsoft ya kutengeneza Microsoft Office (sijui niseme Windows) ya Kiswahili. Sasa ndugu yangu, huoni hapo nikija na neno 'PURU' litaleta unafuu zaidi kuwakilisha ulimwengu wa 'digital'?

Mmmh hapana si mwalimu wa kiswahili, fani yangu ni sheria ila nakipenda sana kiswahili,na mara nyingine nimefanya tafsiri kadhaa,kwa kushirikiana na TUKI.Nakijua kiswahili japo kiaina kwa kuwa kidato cha tano nimesoma HGK pale Mkwawa na mwalimu wangu si haba alikuwa mzuri. Naam yupo Makongo sasa,walimwiba.
Kwa ufupi ni hivyo.

Augustoons, HGK Mkwawa... Duuh, ama kweli dunia yetu ni ka-duara kadogo, isije kuwa tulikuwa tunasimama wote pale 'Bomba Tatu' na kuagiza chips 'Makanyagio'!! 🙂

Kuhusu hiyo project ya TUKI, kuna siku nitakutafuta kuongelea zaidi, kwani nina shauku kubwa ya kujua na pia kuendeleza lugha yetu katika ulimwengu wa teknolojia. Na kwa kumaliza tena naomba tu nikudunge na nyongeza ya swali:

'Project' kwa Kiswahili sanifu ni nini? Kuna maneno kama mchakato nakutana nayo lakini sina uhakika... naomba maelekezo.
Natanguliza shukrani zangu.

SteveD.
 
Yap. steve nimekupata
Digital kwa kiswahili sanifu ni tarakimu lakini ukilisanifisha kwa kulitohoa linakuwa dijitina neno hili linaponyumbulika na kuwa digital kwa kiswahili vilevile linanyumbulika kuwa dijito.. hivyo ipp walikuwa sahihi tu kusema digital ni dijito walikosea tu ji wakaweka gi.

Mmmh ndio mkwawa bomba tatu kibanda simama eeh yap nilikuwa mak west pale na mwakanemela as me their chairman.Nilimtaja masebo kifonetiki.Karibu sana kwenye ukuzaji wa hii lugha.
Fungo, Augustus
UK

Kwa heri
 
Je, na unajua kuwa software manaake ni mifumo laini?

Duuh, 🙂,

Ahsante Augustoons, lakini kwanini wasitunge neno jipya tu kuwakilisha software... 'mifumo laini' mimi naona kama description vile badala ya kuwa nomino....


SteveD.
 
Hivi ni "Pasuka na kucheka" Unapasuka ukiwa katika hali ya kucheka.

Au ni "Pasuka kwa kucheka?" Mpasuko wako unasababishwa na kicheko.

Nimesikia pia watu wakisema au/na kuandika, "ame-kwenda kinyume na sheria." Badala ya "kwenda kinyume cha sheria." Vipi ndio vipi?
 
Back to hands of tym.

Enheee... Nakuja na maswali.

Epi Nyu Ia tu Oll
 
"whereas" (wakati, kumbe): Niliambiwa uko Mwanza ilhali uko Mtwara.
 
Nami naomba kujua tofauti ya maneno haya:
Kusojoa, kuvua nguo, na kusaula.
 
Yapata miezi miwili hivi sasa tangu nisanidi Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003 kipatikanacho hapa: http://www.microsoft.com/downloads/...BC-C987-48F5-9707-DC6C7D0E35D0&displaylang=sw

Kwa hiyo violesura vyangu vya word, excel, outlook na power point vyooote viko kwa kiswahili. Ni burudani flani hivi I must say.. maana kuna maneno ya ajabu ajabu hata sijui waliotafsiri wameyatoa wapi, kwa mfano ... kujibu swali lako .. pahala pa "My Computer" pameandikwa 'Ngamizi yangu'. Sasa hata sijui computer kuwa Ngamizi inangamiza nini!
Nadhani ngamizi iliyokusudiwa ni ng'amizi, yaani yenye kung'amuwa. Kwa maana kuwa yenye kujuwa, mfano, mie nimeshang'muwa ujanja wa mtindioubongo. yaani nimeshaujuwa ujanja wa... Nadhani sikupotea kwa hilo. Na sidhani kama ilikusudiwa ngamizi ya kuangamiza.

my computer = ng'amizi yangu, wameshindwa (wamesahau)kuweka hiyo apostrophe inayobadilisha sound ya nga na ng'a
 
Back
Top Bottom