SoC02 Kiswahili ni Afrika Mashariki, Kiswahili ni Tanzania, Kiswahili ni Amani na Upendo

SoC02 Kiswahili ni Afrika Mashariki, Kiswahili ni Tanzania, Kiswahili ni Amani na Upendo

Stories of Change - 2022 Competition

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
HISTORIA YA KISWAHILI.
Kuna nadharia mbalimbali kuhusiana na historia ya lugha ya Kiswahili. Wapo wanaodai chimbuko la Kiswahili kuwa ni pwani ya Afrika mashariki, wataalamu kama Nae Freeman Granville (1959) kupitia kitabu chake kiitwacho (the medieval of Kiswahili language) anakuja na hoja kuwa Kilwa hata kabla ya karne ya 10 ilikuwa na umuhimu mkubwa kibiashara hivyo basi kulinganana na umuhimu huo wa biashara miongoni mwa wa wabantu wa kilwa na wageni(waarabu) ilipelekea kuibuka kwa lugha moja ambayo ndiyo inasadikika ni Kiswahili leo hii.

download (1).png

Nadharia nyingine ni kama asili ya Kiswahili ni huko Afrika ya magharibi(Kamerun) sababu kuu ni kuwa huko ndiko chimbuko la wabantu kabla ya kutawanyika kutokana na sababu mbalimbali na wapo wataalamu wanaosema kuwa chimbuko la Kiswahili ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Nadharia zote zaweza kuwa na mashiko kwa kuwa lugha ya Kiswahili ina maneno ya kibantu, kiarabu na baadhi ya maneno kutoka lugha tofauti kama kireno, kiingereza na kihindi kitu kilichochewa na muingiliano wa watu wa jamii tofauti kutokana na biashara pamoja na ujio wa wakoloni.

UMRI WA LUGHA YA KISWAHILI.
Lugha hii inakadirirwa kuwa na takribani na miaka 800 hadi 1000 toka kuanza kwake katika vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka uarubuni, uajemi, na uhindi walipokutana na wenyeji wakazi wa Afrika.

Lugha ya Kiswahili iliweza kuzaliwa kutokana na wenyeji wabantu kupokea maneno mengi kutoka lugha tofauti hasa maneno ya kiarabu katika kuwasiliana.

DGd3TobXYAAqQX7.jpg

Kuenea kwa lugha ya kiswahili.
Kupitia biashara na muingiliano wa watu lugha ilianza kuenea sehemu mbalimbali za ulimwengu. wakati wa ukoloni lugha ya Kiswahili iliweza kusanifiwa na kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye misingi wa lahaja ya unguja.

Kiswahili ni nini?
Kiswahili
ni lugha miongoni mwa lugha takribani elfu saba(7000) zinazozungumzwa ulimwenguni ikiwa inazungumzwa haswa katika eneo la Africa mashariki(Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kaskazini mwa Msumbiji).

Nchi zinazozungumza kiswahili.
Kiswahili ni lugha rasmi ya taifa katika nchi ya Tanzania na kenya. Uganda pia iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Iddi amin matumizi ya Kiswahili yalipingwa na waganda kutokana na historia ya utawala wa kijeshi.

Mashariki mwa Kongo Kiswahili kimeenea sana na ni moja kati ya lugha nne za kitaifa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Nchini Rwanda mnamo tarehe 8 februari 2017 bunge lilifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, kifaransa na kiingereza.

Map-of-East-African-countries-Source-United-Nations-43.png

Mafanikio ya kiswahili.
Tarehe 23 mwezi novemba mwaka 2021 shirika la umoja wa mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO lilitangaza rasmi tarehe 7 ya julai kila mwaka kuwa siku ya kiswahili duniani.

download.png

Ni moja katika hatua muhimu za mafanikio ya Kiswahili katika anga za kimataifa. Katika azimio hilo lenye kurasa tatu, inaelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na uamuzi wa kikao cha 212 cha bodi utendaji ya UNESCO kwa kutumia misingi mikuu kumi ambayo ni:

1. Kiswahili ni mawasiliano.

2. Wazungumzaji wa Kiswahili duniani.

3. Kiswahili Afrika mashariki, kati na kusini.

4. Kiswahili na kufanikisha SDGs(Sustainable Development Goals) na AcFTA(Africa Continental Free Trade Area)

5. Kiswahili katika idhaa za umoja wa mataifa.

6. Umoja wa mataifa na matumizi ya lugha zaidi ya moja.

7. Kiswahili na utajiri katika utofauti wa kiisimu.

8. Kiswahili ni lugha rasmi ya SADC(Southern African Development Community)

9. Kwa nini 7/7 na si tarehe nyingine. Tarehe 7/7/1954 nisiku ambayo chama cha TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION(TANU) chini ya hayati mwalimu julias kambarage nyerere,rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilipitisha Kiswahili kama lugha ya kuunganisha harakati za ukombozi.

10. Maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani

Mafanikio mengine ni kama
  • Kuwepo kwa vyombo vya habari kama televisheni,redio na hata magazeti kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kimataifa vinavyotumia lugha ya Kiswahili kuwasilisha maudhui kwa hadhira.
  • Kuwa lugha ya afrika ambayo ni lugha rasmi katika serikali ya Tanzania na jumuiya ya afrika mashariki.
  • Kuanzishwa kwa kozi mbalimbali za Kiswahili katika ngazi ya shahada katika vyuo vya elimu ya juu kitaifa na kimataifa.
  • Tanzania kuna lugha zaidi ya 100 lakini Kiswahili kinazungumzwa na asilimia 90 ya idadi ya watu na ni moja ya nguzo muhimu inayounganisha makabila 130.
  • Kutumika katika mikutano mikubwa ya kimataifa kama lugha ya majadiliano.
  • Lugha ya Kiswahili kutumika kwenye sanaa kama maigizo,miziki, ushairi na uandishi na kupelekea kazi hizo kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Idadi ya wazungumzaji wa Kiswahili ulimwenguni.
Katika makala ya umoja wa mataifa(UN) mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la elimu,sayansi na utamaduni (UNESCO) Audrey azoulay amesema ikiwa na wazungumzaji kati ya milioni 120 hadi 150 lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zinazoshamiri kuvuka mipaka ya inamozungumzwa.

Inakadiriwa lugha ya Kiswahili ina idadi ya watu kati ya milioni 100 mpaka 200

Kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili.
Ni jukumu la kila mtu kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili. sisi kama watanzania tunapaswa kupenda na kujivunia lugha yetu kwa maana ni sehemu muhimu wa utambulisho wetu kimataifa

Je tunaweza kufanya nini ili kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili?

  • Kuweka msisitizo juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye mitaala ya elimu na shughuli za kiserikali.
  • Uanzishwaji wa majukwaa ya kimtandao yatayowakutanisha wazungumzaji wa Kiswahili popote walipo duniani.
  • Kuzalisha wataalamu wa Kiswahili wenye uadilifu wa hali ya juu watakaoweza kufundisha Kiswahili kimataifa.
  • Kuyapa nguvu ya kifedha na rasilimali watu taasisi na mabaraza ya Kiswahili.
  • Kusisitiza matumizi ya Kiswahili fasaha kwenye vyombo vya habari kama magazeti, televisheni na radio.
  • Kutengeneza kazi za sanaa zenye ubora wa kimataifa lugha ya Kiswahili.
  • Kuongeza ushirikano na mataifa mengine katika nyaja ya biashara na ujirani mwema.

Hitimisho
  • Kiswahili ni Afrika mashariki
  • Kiswahili ni Tanzania
  • Kiswahili ni ustaarabu
  • Kiswahili ni amani
  • Kiswahili ni ushirikiano
  • Kiswahili ni harakati

Marejeo

PICHA. Kwa msaada wa Google.
 
Upvote 219
HISTORIA YA KISWAHILI.
Kuna nadharia mbalimbali kuhusiana na historia ya lugha ya Kiswahili. Wapo wanaodai chimbuko la Kiswahili kuwa ni pwani ya afrika mashariki, wataalamu kama Nae Freeman Granville (1959) kupitia kitabu chake kiitwacho (the medieval of Kiswahili language) anakuja na hoja kuwa Kilwa hata kabla ya karne ya 10 ilikuwa na umuhimu mkubwa kibiashara hivyo basi kulinganana na umuhimu huo wa biashara miongoni mwa wa wabantu wa kilwa na wageni(waarabu) ilipelekea kuibuka kwa lugha moja ambayo ndiyo inasadikika ni Kiswahili leo hii.

View attachment 2311226

Nadharia nyingine ni kama asili ya Kiswahili ni huko afrika magharibi(kamerun) sababu kuu ni kuwa huko ndiko chimbuko la wabantu kabla ya kutawanyika kutokana na sababu mbalimbali na wapo wataalamu wanasema kuwa chimbuko la Kiswahili ni jamhuri ya kidemokrasia ya congo.

Nadharia zote zaweza kuwa na mashiko kwa kuwa lugha ya Kiswahili ina maneno ya kibantu, kiarabu na baadhi ya maneno kutoka lugha tofauti kama kireno, kiingereza na kihindi kitu kilichochewa na muingiliano wa watu wa jamii tofauti kutokana na biashara pamoja na ujio wa wakoloni.

UMRI WA LUGHA YA KISWAHILI.
Lugha hii inakadirirwa kuwa na takribani na miaka 800 hadi 1000 toka kuanza kwake katika vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka uarubuni, uajemi, na uhindi walipokutana na wenyeji wakazi wa Afrika.

Lugha ya Kiswahili iliweza kuzaliwa kutokana na wenyeji wabantu kupokea maneno mengi kutoka lugha tofauti hasa maneno ya kiarabu katika kuwasiliana.

View attachment 2311228
Kuenea kwa lugha ya kiswahili.
Kupitia biashara na muingiliano wa watu lugha ilianza kuenea sehemu mbalimbali za ulimwengu. wakati wa ukoloni lugha ya Kiswahili iliweza kusanifiwa na kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye misingi wa lahaja ya unguja.

Kiswahili ni nini?
Kiswahili
ni lugha miongoni mwa lugha takribani elfu saba(7000) zinazozungumzwa ulimwenguni ikiwa inazungumzwa haswa katika eneo la Africa mashariki(Tanzania, kenya, Uganda, jamhuri ya kidemokrasia ya kongo na kaskazini mwa msumbiji).

Nchi zinazozungumza kiswahili.
Kiswaahili ni lugha rasmi ya taifa katika nchi ya Tanzania na kenya. Uganda pia iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Iddi amin matumizi ya Kiswahili yalipingwa na waganda kutokana na historia ya utawala wa kijeshi.

Mashariki mwa kongo Kiswahili kimeenea sana na ni moja kati ya lugha nne za kitaifa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Nchini Rwanda mnamo tarehe 8 februari 2017 bunge lilifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, kifaransa na kiingereza.

View attachment 2311232

Mafanikio ya kiswahili.
Tarehe 23 mwezi novemba mwaka 2021 shirika la umoja wa mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO lilitangaza rasmi tarehe 7 ya julai kila mwaka kuwa siku ya kiswahili duniani.

View attachment 2311233

Ni moja katika hatua muhimu za mafanikio ya Kiswahili katika anga za kimataifa. Katika azimio hilo lenye kurasa tatu, inaelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na uamuzi wa kikao cha 212 cha bodi utendaji ya UNESCO kwa kutumia misingi mikuu kumi ambayo ni:

1. Kiswahili ni mawasiliano.

2. Wazungumzaji wa Kiswahili duniani.

3. Kiswahili afrika mashariki, kati na kusini.

4. Kiswahili na kufanikisha SDGs(Sustainable Development Goals) na AcFTA(Africa Continental Free Trade Area)

5. Kiswahili katika idhaa za umoja wa mataifa.

6. Umoja wa mataifa na matumizi ya lugha zaidi ya moja.

7. Kiswahili na utajiri katika utofauti wa kiisimu.

8. Kiswahili ni lugha rasmi ya SADC(Southern African Development Community)

9. Kwa nini 7/7 na si tarehe nyingine. Tarehe 7/7/1954 nisiku ambayo chama cha TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION(TANU) chini ya hayati mwalimu julias kambarage nyerere,rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kilipitisha Kiswahili kama lugha ya kuunganisha harakati za ukombozi.

10. Maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani

Mafanikio mengine ni kama
  • Kuwepo kwa vyombo vya habari kama televisheni,redio na hata magazeti kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kimataifa vinavyotumia lugha ya Kiswahili kuwasilisha maudhui kwa hadhira.
  • Kuwa lugha ya afrika ambayo ni lugha rasmi katika serikali ya Tanzania na jumuiya ya afrika mashariki.
  • Kuanzishwa kwa kozi mbalimbali za Kiswahili katika ngazi ya shahada katika vyuo vya elimu ya juu kitaifa na kimataifa.
  • Tanzania kuna lugha zaidi ya 100 lakini Kiswahili kinazungumzwa na asilimia 90 ya idadi ya watu na ni moja ya nguzo muhimu inayounganisha makabila 130
  • Kutumika katika mikutano mikubwa ya kimataifa kama lugha ya majadiliano.
  • Lugha ya Kiswahili kutumika kwenye sanaa kama maigizo,miziki, ushairi na uandishi na kupelekea kazi hizo kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Idadi ya wazungmzaji wa Kiswahili ulimwenguni.
Katika makala ya umoja wa mataifa(UN) mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la elimu,sayansi na utamaduni (UNESCO) Audrey azoulay amesema ikiwa na wazungumzaji kati ya milioni 120 hadi 150 lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zinazoshamiri kuvuka mipaka ya inamozungumzwa.

Inakadiriwa lugha ya Kiswahili ina idadi ya watu kati ya milioni 100 mpaka 200

Kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili.
Ni jukumu la kila mtu kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili. sisi kama watanzania tunapaswa kupenda na kujivunia lugha yetu kwa maana ni sehemu muhimu wa utambulisho wetu kimataifa

Je tunaweza kufanya nini ili kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili?

  • Kuweka msisitizo juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye mitaala ya elimu na shughuli za kiserikali.
  • Uanzishwaji wa majukwaa ya kimtandao yatayowakutanisha wazungumzaji wa Kiswahili popote walipo duniani
  • Kuzalisha wataalamu wa Kiswahili wenye uadilifu wa hali ya juu watakaoweza kufundisha Kiswahili kimataifa.
  • Kuyapa nguvu ya kifedha na rasilimali watu taasisi na mabaraza ya Kiswahili
  • Kusisitiza matumizi ya Kiswahili fasaha kwenye vyombo vya habari kama magazeti, televisheni na radio
  • Kutengeneza kazi za sanaa zenye ubora wa kimataifa lugha ya Kiswahili
  • Kuongeza ushirikano na mataifa mengine katika nyaja ya biashara na ujirani mwema.

Hitimisho
  • Kiswahili ni Afrika mashariki
  • Kiswahili ni Tanzania
  • Kiswahili ni ustaarabu
  • Kiswahili ni amani
  • Kiswahili ni ushirikiano
  • Kiswahili ni harakati

Marejeo

PICHA. GOOGLE.
Tayari
 
Kura unapigaje?
Kama unatumia Application ya Jamiiforum hakuna sehemu ya kupigia kura.

Jinsi ya kupiga kura unaingia Jamiiforum kupitia browser na kufungua link utaona sehemu ya kupigia kura
 
Attachments

  • Screenshot_20220818-195331.jpg
    Screenshot_20220818-195331.jpg
    78.2 KB · Views: 6
Maelezo bora na yakueleweka sana nimeyapata kutokea kwa hili chapisho, honera sana mwandishi umenifumbua macho. Kiswahili kinazidi kua bora Zaidi maana pita pita zangu mjini playstore nimekutana na hii game inaitwa #swahiliwordcross nimetokea kuipenda kweli nikaona itafaa nishare na wanaforum pia. Nimekutana na misamiati sijai itumia kabisa lakini kumbe inaishi kwenye Kiswahili chetu
1114.png
 
Maelezo bora na yakueleweka sana nimeyapata kutokea kwa hili chapisho, honera sana mwandishi umenifumbua macho. Kiswahili kinazidi kua bora Zaidi maana pita pita zangu mjini playstore nimekutana na hii game inaitwa #swahiliwordcross nimetokea kuipenda kweli nikaona itafaa nishare na wanaforum pia. Nimekutana na misamiati sijai itumia kabisa lakini kumbe inaishi kwenye Kiswahili chetuView attachment 2340538
Shukurani sana Kwa kushare. Unaweza ongezea namna ya kulicheza
 
kulicheza ni kwa kuunganisha herufi zilizo kweny mduara kupata neno jipya la Kiswahili. mfano hilo neno poa lililonekana kati hapo ni baada ya kuanza na herufi ya p nikafuata o nikamalizia na A. ukishikilia herufi moja bila kuachia ukafanya kama unachora mshale unaoelekea herufi nyingingine bila kuinua kidole utaona mshale unajiteneza
 
Attachments

  • Screenshot_20220818-195331.jpg
    Screenshot_20220818-195331.jpg
    78.2 KB · Views: 4
wazungmzaji
Rekebisha hapa mkuu

wazungmzaji = 'wazungumzaji'

Kiswaahili

Kiswaahili = Kiswahili

julias andika kwa herufi kubwa Julius

Sio Julias ni Julius

Jina la Kwanza na la mwisho andika kwa herufi kubwa

azoulay = Auzolay

inakadirirwa kuwa na takribani na miaka 800
kuwa = 'kua'

inakadiridiriwa kua na takribani miaka 800

Tuipende lugha yetu

Kazi nzuri mkuu
 
Kiswahili kwa sasa ni zaidi ya Afrika Mashariki, historia ya kutafuta uhuru ilifanya harakati nyingi kuratibiwa nchini Tanzania na matokeo yake wapigania uhuru karibia wote waliondoka na kiswahili na kukieneza huko. Mbali ya Mozambique kwa sasa mpaka Johanesburg watu wanaongea kiswahili.

Kuna malori kwa sasa zaidi ya 1,000 kwa siku yanatoka na kuingia Dar es salaam, wapambanaji hawa wanazunguka na kiswahili kwa Congo sio tu mashariki Mpaka Lubumbashi watu wanaongea swahili, kuna Sudan, Angola huko kote watu wanavutiwa na kiswahili na utamaduni wa waswahili.

EAC na SADC imetupa nafasi ya kuongeza muingiliano, sasa hivi ni kugonga entry tu na sio VISA tena, kwa wageni wengi wanaokuja uswahili na wanapenga kuongea na kiswahili. Maendeleo ya Soka na idadi ya wageni wanaokuja pia sasa tumemuona Morrison kutoka Ghana akiongea kiswahili achilia Mbali aliyekuwa CEO wa Yanga ameupiga mwingi mno. Wakati timu zetu zitatazamwa na jamii na watu wengi Afrika na Duniani pasi na shaka kiswahili ndio alama yetu.
 
Yote uliyoandika ni kweli wengi wetu tumekuwa na mtazamo hasi juu ya lugha yetu wenyewe na kuona fahari kwenye lugha za wenzetu.

Ukweli ni kuwa tuna Kila sababu ya kujivunia na kupenda lugha ya kiswahili licha ya kuwa ni utambulisho wetu pia ni sehemu ya harakati za ukombozi Kwa Taifa letu

Shukurani sana Mkuu.
 
Rekebisha hapa mkuu

wazungmzaji = 'wazungumzaji'

Kiswaahili = Kiswahili

julias andika kwa herufi kubwa Julius

Sio Julias ni Julius

Jina la Kwanza na la mwisho andika kwa herufi kubwa

azoulay = Auzolay

kuwa = 'kua'

inakadiridiriwa kua na takribani miaka 800

Tuipende lugha yetu

Kazi nzuri mkuu
Mkuu nashukuru sana kwa mapendekezo yako na nitayafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom