Kitabu cha Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) katika PDF

Kitabu cha Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) katika PDF

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITABU CHA ABDUL SYKES KATIKA PDF

Kitabu hiki kilichochapwa na Minerva Press London 1998 sasa kipo katika pdf.

Nimeshindwa kupata link lakini nimewatumia watu wengi katika Whatsapp peaneni humo kwa humo na wenyewe kwa wenyewe mpate kukisoma kitabu hiki bure.

Soma Kwa Furaha.

1663185144467.png
 
kazi kweli kweli
Hand...
''Kazi kweli kweli.''

Hakika kitabu hiki ilikuwa kazi kubwa zaidi si katika kuandika bali katika kupata mchapaji.

Mchapaji wa kwanza alikipokea na baada ya kukisoma tukazungumza kuhusu kitabu chenyewe na maudhui yake.

Alichonifahamisha kwanza ni kuwa mswada ni mzuri sana lakini bado msaada haujakamilika unahitaji kufanyiwa kazi zaidi kama nitakuwa tayari kupokea ushauri wake.

Huyu mchapaji kwa kweli alinisaidia kupita kiasi hadi mswada ukakamilika.

Kwa bahati mbaya sana hakuweza kuchapa kitabu changu na alikaa na mswada wangu kwa karibu miaka saba.

Nikawaonyesha Oxford University Press, Nairobi (.OUP).

Wahariri wa OUP walitoa taarifa kuwa kitabu ni kizuri lakina OUP hawatoweza kukichapa kwa kuwa maudhui ya kitabu ni nyeti sana kwa serikali ya Tanzania na kwa walio madarakani.

Lakini OUP nawashukuru kwa kitu kimoja.

Walinielekeza kwa wachapaji Uingereza ambao waliniambia wao kazi kama yangu ndiyo shughuli yao.

Hakika kitabu kikachapwa mwaka wa 1998.

Kitabu kilipotoka na kufika Dar es Salaam kutoka London kishindo chake kilikuwa kikubwa sana.

Kama ulivyosema ilikuwa ''kazi kweli kweli.''
 
Mlio jaaliwa kutumiwa kwa njia ya WhatsApp, kipandisheni hapa
 
Tunasubir.niliwah kusoma hiki kitabu kwa bahat tu.katika kupekura vitabu vya bro zaman kidogo 2017 nipo form 5 .kwanza nilisoma nikashtukaa!!!!
Maaana niliyosoma humo ilikua sijawah kuyasoma popotee.with evidence.
So sikuwez kukimaliza.
Natumai kupata pdf hapa
 
Tunasubir.niliwah kusoma hiki kitabu kwa bahat tu.katika kupekura vitabu vya bro zaman kidogo 2017 nipo form 5 .kwanza nilisoma nikashtukaa!!!!
Maaana niliyosoma humo ilikua sijawah kuyasoma popotee.with evidence.
So sikuwez kukimaliza.
Natumai kupata pdf hapa
Julai...
Nipatie Whatsapp nitakurushia In Shaa Allah.
 
Back
Top Bottom