Hand...
''Kazi kweli kweli.''
Hakika kitabu hiki ilikuwa kazi kubwa zaidi si katika kuandika bali katika kupata mchapaji.
Mchapaji wa kwanza alikipokea na baada ya kukisoma tukazungumza kuhusu kitabu chenyewe na maudhui yake.
Alichonifahamisha kwanza ni kuwa mswada ni mzuri sana lakini bado msaada haujakamilika unahitaji kufanyiwa kazi zaidi kama nitakuwa tayari kupokea ushauri wake.
Huyu mchapaji kwa kweli alinisaidia kupita kiasi hadi mswada ukakamilika.
Kwa bahati mbaya sana hakuweza kuchapa kitabu changu na alikaa na mswada wangu kwa karibu miaka saba.
Nikawaonyesha Oxford University Press, Nairobi (.OUP).
Wahariri wa OUP walitoa taarifa kuwa kitabu ni kizuri lakina OUP hawatoweza kukichapa kwa kuwa maudhui ya kitabu ni nyeti sana kwa serikali ya Tanzania na kwa walio madarakani.
Lakini OUP nawashukuru kwa kitu kimoja.
Walinielekeza kwa wachapaji Uingereza ambao waliniambia wao kazi kama yangu ndiyo shughuli yao.
Hakika kitabu kikachapwa mwaka wa 1998.
Kitabu kilipotoka na kufika Dar es Salaam kutoka London kishindo chake kilikuwa kikubwa sana.
Kama ulivyosema ilikuwa ''kazi kweli kweli.''