Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Hizi zote ni hadith tu, hakuna ukweli wowote.
 
So hapo unamaanisha time ya raisi ikipeleka matokeo ya utafiti kwa raisi hayawi sawa kwa sababu raisi hajaenda kushuhudia data zikikusanywa?
And Again Tume ya Rais Samia Lets say Ikitumwa kuchunguza utafiti kuhusu Maisha ya Kinjikitile ngwale na ikaja ikasema maisha hayo ndyo maisha halisi ya Kinjikitile hata kama watakusanya Data 100 Lazma kutakuwa na Uongo mwingi sana kwenye Tafiti hizo..

Umewahi kusoma Kuhsu Research Unafahamu Vitu vimavyoharibu Ubora wa Data??
Vipi kuhusu Muda Unfahamu inavyoharibu ubora wa Data??

Kwahyo huwezi kuamini Research itakayofanywa Kwa tukio Lilifanyika Miaka 90 mpaka 100 Iliopita Halafu ukasema Litakuwa Statistical Correct...

kwangu mimi nikiona Unatetea Reseach yakokwa nguvu zote Nitasema wewe Ni unaleta Frauds..
 
Dr mbona unafanya academic intimidation? Kwamba nimewahi kusoma research? Sijui ubora wa data!
Mimi nasimama ktk hoja kuwa Luka aliandika ripoti na tunaona usahihi wa ripoti yake kwa kutumia vyanzo vingine. Hajuwa among the 12. Hata huyo Theofilo alikuwa hai.
Pia, maandishi yake hayajapingwa na watafiti wengine au waandishi wengine waliondika kipindi na baada ya Luka kuandika. Hapa namaanisha mitume na wanafunzi wengine wa Yesu. Je yanarandana na gospel nyingine au yanapingana?
Kuhusu research au usahihi wa data uliougusia. Utafiti hupigwa kwa utafiti. Kauli hii ni maarufu sana katika ulimwengu wa watafiti. Sasa lete maandiko au utafiti wa waliokuwepo pamoja na Luka wakisema Luka alikosea ukoo wa Yesu au mstari huu au andiko hiki au tendo hiki halikutendwa.
Yeye mwenyewe ( Luka) anasema mambo yaliyitendwa katikati Yao yaani pamoja na kiongozi wa kiserikali anayeitwa Theofilo halafu huyu mtawala akubali kama mjinga tuu! Hapana maana yake na yeye alikuwa na vyanzo vya kuprove andikonla Luka.
Leo atokee mtu anayejiita mtafiti wa mambo ya kele sijui biblia aseme kitabubcha Luka kiondolewe nafkiri atakuwa anakosea.
 
Sorry Kama umehisi Nimefanya Academic Intimidation!..

Sikutaka Nifike Kwenye Kuchambua Context na contents za Kitabu cha Luke lakini kwakuwa UmeInsist ok lets Go to the mission...

SASA KWAKUWA UMETAKA UCHAMBUZI SASA SOMA KWA UMAKINI HAPA CHINI, KABLA YA KUJIBU HOJA


Tuanze Na The adressee Of the Book of Luke..


(Mwandikiwa wa Kitabu cha Luke) ambaye alikuwa Theophilo au Theophilus Mwana wa Ananus Mtukufu...

Kama Unasoma Extra biblical History Utagundua kwamba Theophilus amefariki Mwaka 47 AD (Ambaye alikuwa high priest wa Jerusalem from 37-41 AD, ambaye alikuwa mtoto wa Annas (Anna) na Shemeji yake Caiaphas (Kayapha)..)

Na ikumbukwe amefariki miaka kumi au kumi na kitu Tangu Yesu afariki na Ikumbukwe Kitabu cha Luka kimeandikwa Mwaka 90s AD mpaka 100s AD..
Miaka 40 mpaka 50 baada ga Kufariki kwa Theophilus..

Sasa Kama Kitabu cha Luka Kimeandikwa Miaka 50 Baada ya kufariki kwa Theophilus unahisi Ni theophilus Gani aliyekuwa anaandikiwa Ambaye alikuwa kwenye Position ya Uongozi enzi hizo??
huoni kama Ni fabricated Story???

Japo some Churches Historian wana identifies Theophilus kama later high priest yaani Mattathias ben Theophilus, ambaye yeye alitumikia from 65 to 66.

wakisema kwamba Luka alimtaja priest Joseph ben Caiaphas simply kwa "Caiaphas". yaani Kayapha...Thus, the reasoning goes, Luke used this pattern when addressing Theophilus.

Lakini Bado Huyo Theophilus mwingine na Yeye alifariki miaka ya 73 AD Kabla ya Uandishi wa Kitabu cha Luka..

Umesema Kuhusu Context Za kitabu cha luka Ni sawa na Context Zingine za Vitabu vyenzake Vya Injili (Synoptic Gospel)? Sidhani....Kwakuwa umeenda kwenye Contradictory facts na nilikuwa sitaki tufike huku haya sawa..

Tuangalie Context Moja Pendwa UKOO WA YESU Kwenye Injili mbili LUKE NA MATHAYO.Kila mmoja kaeleza

Baba Yake na Yusuph
(ambaye ni Babu yake na Yesu)..

Ukisoma kwenye Mathayo Alikuwa anaitwa Yakobo (Mathayo 1:16) na ukisoma kwa Luka aliitwa ni Eli (Luka 3:23)..
From There the whole Clan ikapotea kabisa..
From eli to Zerubabeli.. Yaani namaanisha Ukoo wote wa Mathayo na ukoo wa Yesu wa Luka uko tofauti mpaka Kwa Zerubabeli....

Na hata Tukianza Kumchambua Ukoo Huo nataka Uwe makini Hapa uweke Akili zako zote hapa..(Si Unamtetea Luka?)..


Hakuna Doubt kwamba Zerubabeli Baba yake Alikuwa Sheatiel (Luka 3:27)..


Lakini Nasikitika kukwambia Kwamba Zerubabeli (Zorobabel) hakuwahi kuwa na Mtoto anaitwa Rhesa wakati wowote ule kama Alivyotuambia Luka..

Soma (1 Mambo ya Nyakati 3:19-20.) Unakuta kwamba Zerubabel alikuwa na watoto watano ila Rhesa sio Miongoni mwa wanae..
Kulikuwa na Meshulamu,Hanania,Shelomithi,Hashuba,oheli,berekia,hasadia,Yushab-Hesedi...


Ambapo kama Msomi mzuri wa Luka 3:27 Utagundua Kwamba Rhesa hakuwa miongoni mwa watoto wa Zerubabeli sasa Luka alimtoa wapi????

Na utagundua kwamba hata Baba yake na Sheatiel kama alivyotajwa kwenye Luka 3:27 Kuwa ni Neri kitu ambacho sio kweli Tukirudi Agano la kale 1 Mambo ya nyakati 3 Na hata kwenye Mathayo 1..

Kwa Mujibu wa Mathayo 1:12 Baba yake na Sheatiel alikuwa anaitwa Yekonia..


Na hata kwenye 1 Mambo ya Nyakati 3:17..
Baba yake na sheatiel alikuwa yekonia Na sio Neri kama Luka alivyosema..



Sasa Jiulize kuwa Huyo Neri Luka alimpata wapi..

Hata hivyo tukienda kuhusu Mwana wa Daudi wote wanafahamu kuwa Yesu Ni Mwana wa Daudi ils swali ni kwamba kwa Mwana yupi wa Daudi ukoo wa Yesu unaandikwa???


Ukisoma kwa Luka 3:31 Atakuwambia Nathan (Kitu ambacho Sio Cha kweli) Ndyo Mtoto wa Daudi Ukoo wa Yesu Ulipotokea..


Ukoo wa Yesu Unatoka kwa Suleiman Mtoto wa Daudi kama Alivyotabiriwa..na kama Alivyosema Mathayo 1:6-7


Sasa sijui kama umeweza Kusoma na Kuchunguza Context ya Hivyo vitu..

Na ukaona kuwa Luka ni just Fabricated story ilichukua Maarifa yake kutoka Q Sources na Mark sources na Kuongeza Maarifa yske yake yasiyo ya Kweli ...

Nakukaribisha kwa Hoja Yakinifu Mkuu..
Kama utahitaji hoja Zaidi Niambie..

Ila tambua Kwamba Luka Ni kitabu Kinachopotosha na hakikustahili kuwa kwenye Biblia
 
Sasa hapa umekuja na hoja ambayo kwangu Sasa ni assignment ya kufanyika kazi. Hii ndo hoja ambayo Ina mashiko kabisaa na nakubali kuwa hii kitu siwezi kukataa walankukubali maana Sina taarifa ya awali. Naifanya kama assignment ni consult madesa niifatile hii issue.
With thanks
 
Tukipata mijadala kama hii Hapa JF kila wiki nitatamba kitaa
 
Lakini kitabu cha mwanzo kinaeleza tulio la MALAIKA kuzaa na Wana WA binadamu wakazaliwa wanefili ingawaje Biblia imefupisha Sana
Ni kweli kabisa Kuna malaika walifanya uasi kuingiliana na binadamu wakazaliwa hao wanefili wenye maumbo makubwa mwanzo 6 malaika hao wametajwa kama Wana wa Mungu

Majibu utayapata ukisoma 2 Petro 2:4 adhabu waliyoipata Hawa malaika waasi
 
Ni kweli kabisa Kuna malaika walifanya uasi kuingiliana na binadamu wakazaliwa hao wanefili wenye maumbo makubwa mwanzo 6 malaika hao wametajwa kama Wana wa Mungu

Majibu utayapata ukisoma 2 Petro 2:4 adhabu waliyoipata Hawa malaika waasi

Sahihi Kwa Mujibu wa Biblia
 
Ni kweli kabisa Kuna malaika walifanya uasi kuingiliana na binadamu wakazaliwa hao wanefili wenye maumbo makubwa mwanzo 6 malaika hao wametajwa kama Wana wa Mungu

Majibu utayapata ukisoma 2 Petro 2:4 adhabu waliyoipata Hawa malaika waasi
Kwahyo malaika wanazaa na kuoa na kufanya mapenzi???

Ukipata Muda Nijibu tafadhali
 
Sasa kwaniniMkuu Mimi sijui
Lakini Lucifer Baadhi ya simulizi zinaeleza kuwa yeye hahusiki na mambo ya ushawishi na kudanganya.
Ila Samael aliumbwa Kwa Kazi hiyo.

Kilichomuangusha Lusifa ni majivuno na kiburi
Ila aliyemdanganya Eva ni Samael
Sasa kwanini huyo malaika amefanya tuje kuishi maisha magumu kiasi hichi duniani, nilidhani shetani ndiye aliye fanya eva na Adam wale tunda,kumbe ni malaika wa Mwenyezi Mungu.
Au nime elewa vibaya
 
Hiko kitabu.nakipataje mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…