Kitabu cha Enock (Henoko)

Kitabu cha Enock (Henoko)

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ukisoma kitabu cha Enoko, anasimulia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, jinsi alivyotokewa na malaika wawili, na kama ilivyo kwa malaika wote wanapowatokea wanadamu huanza na neno “Usiogope”.

Kwa nini?

Ni kwa sababu malaika ana muonekano wa kutisha, kwa binadamu, huwezi kuwa kawaida tu unapomuona malaika ametokea mbele yako, ndiyo maana husema usiogope.

Aliambiwa Mariamu Magdalena pia.

Enoko alianza kuwaelezea malaika ambao walikwenda chumbani kwake wakati amelala.

Kwanza walikuwa wakubwa, wenye mbawa lakini sura zao zilikuwa na mng’ao mkubwa kama jua lakini macho yao yalikuwa yanawaka kama taa.

Katika maisha yake, anasema hakuwahi kuwaona viumbe wakubwa namna hiyo.

Lipsi zao zilikuwa na moto, mbawa zao zilikuwa na mchanganyiko wa rangi mbili, zambarau na dhahabu inayong’aa kupita kawaida, mikono yao ilikuwa ni meupe kama theluji.

Hebu fikiria unakutana na kiumbe kama hicho, hutoogopa? Ndiyo maana walimwambia kwanza, usiogope.

Anasema malaika hao walisimama pembeni ya kitanda chake na kumuita kwa jina lake, Enoko akainuka na kuwaangalia.

Enoko aliogopa, anasema uso wake ulitetemeka mno lakini malaika mmoja akamwambia: “Usiogope”.
Walimwambia walitumwa na Mungu kumchukua na kumpeleka mbinguni, kwa yote ambayo angekutana nayo huko basi angewaambia watoto wake, wajukuu na vizazi vyote mbeleni.

Anasema hakutaka kuwapinga, akatoka na kwenda kuonana na watoto wake, Mathusal, Regim na Gaidad, akawaambia kuhusu malaika hao na kile walichomwambia, baada ya hapo, wakamchukua na kuanza kupaa naye kwa kumbeba kwenye mbawa zao.
20241025_045538.jpg
 
Sehemu ya pili
Malaika wale walimchukua mpaka juu kabisa, na tazama akaanza kuingia kwenye mbingu ya kwanza. Hapa akakutana na bahari kubwa, anasema ukubwa wa bahari ile ni tofauti na bahari ambayo sisi tunayo hapa duniani.

Niliwaambia hii dunia imezungukwa na kioo kikubwa sana kinachoitwa firmament ambapo juu yake kuna maji mengi. Ukisoma kitabu cha Mwanzo, kinasema kipindi cha Nuhu milango ya mbinguni ikafunguliwa na maji kujaa duniani.

So hiyo milango ipo wapi? Ndiyo kwenye hiyo firmament ambayo wanasayansi walijaribu kuivunja kwenye mission za mbalimbali ili watoke nje waone kuna nini, ila hawakufanikiwa.

So juu ya hiyo firmament, kwenye hayo maji mengi aliyoyaona Enoko ndiyo mbingu ya kwanza.

Anasema ilikuwa ni bahari kubwa ambayo hakuna mfano wake.

Anasema baada ya kuiona hiyo bahari kubwa, akashangaa kuwaona malaika mia mbili wakija kule walipokuwa, malaika hawa ndiyo ambayo wanazitawala nyota zote.

Hapa kuna malaika wa aina mbili, wale wanaopaa juu ya bahari na wale ambao wanapita hata ndani ya bahari lakini kwa pamoja kuna wakati unafika na kuungana pamoja.

Wakati anaangalia mbele, macho yake yakatua kwenye nyumba moja kubwa ambayo imetengenezwa kwa barafu tu, malaika wengine walikuwa wakiruka na kwenda kwenye nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni ya kupendeza mno machoni mwake.
20241025_050050.jpg
 
Sehemu ya tatu
Pia akaonyeshwa nyumba nyingine nzuri, ilikuwa ni ya kumeremeta kana kwamba ilijengwa kwa kutumia mafuta. Nyumba hii ilikuwa na maua mengi mazuri ambayo hata mengine hayapo hapa duniani.

Mbali na hilo, pia kulikuwa na malaika wakubwa waliokuwa wakiilinda nyumba hiyo.
Mimi kama Nyemo mnajiuliza: “Malaika hao wanailinda nyumba hiyo dhidi ya nani? Sijui”.
20241025_050322.jpg

Enoko anaendelea kusema kwamba malaika wale wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili na huko akakutana na haya mambo.

Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wamening’inizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.

Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja.

Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika.

Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.

Baada ya hapo Enoko anasema baada ya kuyaona hayo yaliyokuwepo kwenye mbingu ya kwanza, sasa malaika hao wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili.
 
Sehemu ya nne
Enoko akauliza hawa ni akina nani?

Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuning’inizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.

Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani.

Swali ninalojiuliza ni moja.

Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.

Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: “Mtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!”

Enoko akawa anawajibu: “Mimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?”

Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu.

Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.
Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.

Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.

Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.

Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.

Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.

Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.

Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehan
20241025_050628.jpg
amu ilipo.
.
 
Sehemu ya tano
20241025_032315.jpg

Enoko anasema alipopelekwa huko, aliogopa kwa kuwa ilionekana kuwa sehemu iliyojaa mateso makubwa ambayo hakuwahi kuyaona. Mwanga pekee uliokuwa ukipatikana ni wa moto ambao ulikuwa unaunguza kila kilicho humo.

Pia kulikuwa na mto, huu haukuwa wa maji bali mto wa moto. Kulikuwa na moto kila kona. Ila mbali na moto huo, pia kulikuwa na barafu kila sehemu. Yaani kulikuwa na mateso ya aina mbili ambayo watu walikuwa wakiyapata. Ya kuunguzwa sana na moto lakini pia ya kupigwa na baridi kali kiasi cha kuganda kabisa.

Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Watu walikuwa wakilia kwa majuto lakini pia walilia kwa sababu ya kiu kali waliyokuwanayo.

Pia kulikuwa na malaika asiyekuwa na huruma hata kidogo, aliyeogopwa, mwenye hasira na alishika silaha kubwa kwa ajili ya kuwatesea watu.

Enoko akasema: “Hii sehemu imejaa mateso makubwa mno” na malaika akamwambia: “Hii ni sehemu ya watu waliotenda maovu duniani, watu ambao hawakumuheshimu Mungu sehemu ya wachawi, waovu, wabakaji, wala rushwa, matapeli na wengineo.”

Baada ya kuyaona hayo yote, malaika wale wakanichukua na kunipeleka mbingu ya nne.
Mwisho.
Credit: Paul Bonaventura Twitter X
 
Kitabu cha henoko sio cha Biblia ni mafundisho ya mashetani
KIpo ktk biblia za kale..... kabla kuchujwa.....i.e Ahmaric bible......መጽሐፍ ቅዱስ · ኦሪት ዘፍጥረት · ኦሪት ዘጸአት · ኦሪት ዘሌዋውያን · ኦሪት ዘኍልቍ · ኦሪት ዘዳግም · መጽሐፈ ኢያሱ ወልደ ነዌ · መጽሐፈ መሣፍንት · መጽሐፈ ሩት ...
 
Kwani ni Enocko au Enock?

Halafu fungueni hizo code. Zimekuwa ngumu sana.
 
KIpo ktk biblia za kale..... kabla kuchujwa.....i.e Ahmaric bible......መጽሐፍ ቅዱስ · ኦሪት ዘፍጥረት · ኦሪት ዘጸአት · ኦሪት ዘሌዋውያን · ኦሪት ዘኍልቍ · ኦሪት ዘዳግም · መጽሐፈ ኢያሱ ወልደ ነዌ · መጽሐፈ መሣፍንት · መጽሐፈ ሩት ...
Biblia agano la kale wanayo wayahudi ambao ndio agano la kale linawahusu inaitwa Jewish Bible na ndio Biblia original na ya kale kuliko zote ipo hadi leo na haina hicho kitabu cha Henoko
Hiyo Biblia haijawahi chujwa na awaye yeyote iko hivyo hivyo hakuna aliyewahi kaa kuchuja wala kuamua kitabu kipi kiwepo na kipi kisiwepo

Na kanisa lilichukua hiyo Biblia ya agano kale kama vitabu vilivyo na kuviingiza kwenye Biblia ya sasa yenye vitabu 66

Agano la kale tumerithi toka Jewish Bible kama ilivyo na wayahudi ndio wanaitumia hadi leo

Hizo porojo za kusema kuna mtu alikaa kuchuja vitabu vya agano la kale ni uongo
 
Kitabu cha henoko sio cha Biblia ni mafundisho ya mashetani
Umekisoma?

Ukisoma Biblia kwny agano la kale wanaeleza habari za Henoko.

Biblia inakiri kwamba hakufa, bali alinyakuliwa, na hii ni baada ya kufanya maajabu hadi Mungu 'akazima fegi'!.

Kwa kifupi ilikuwa ni hivi...

Kwanza, Henoko (Enock) ni kizazi cha 7 toka kwa Adamu lakini Henoko alipokuwa mkubwa alimkuta Adamu akiwa hai.

Siku moja alimuuliza Adamu, ''Babu nasikia zamani ulikuwa unaongea na Mungu moja kwa moja, kwa nini siku hizi hatuongei nae?''

Adamu akamjibu ni kwa sababu tumekuwa na dhambi nyingi. Henoko akasema, ''mimi sina dhambi, na kuanzia leo nitaanza kuongea nae''

Henoko akatenga muda wa kuongea na Mungu kila siku.

Akawa anaenda sehemu, anaanza kuongea na Mungu, kama vile anaongea tu na rafiki yake. Atamueleza matatizo yake, mawazo yake, mambo aliyofanya na atakayofanya, atamuomba ushauri nk nk, yaani anakuwa anaongea peke yake kama anapiga stori na mtu kwa muda mrefu.

Ataongea kisha atasema, ''Haya Mungu kwa heri, kawasalimie huko mbinguni''.

Au ataenda kidogo kisha atasema ''Mungu samahani kuna kitu nimesahau kukwambia''. Atarudi sehemu aliyokuwa, kisha ataongea alichosahau!

Henoko alifanya hivyo kila siku kwa muda mrefu sana bila kuacha.

Hatimae Mungu aliliona hilo tukio, akawaambia Malaika, ''Kuna mtu huko duniani anafanya kituko, akiendelea hivi, nitafanya kitu ambacho sijawahi kufanya''

Henoko alifanya hivyo kila siku, bila kuchoka, kusahau au kuahirisha kwa muda wa miaka 300. (Miaka mia tatu).

Na ulipofika mwaka wa 300, Mungu aliamua kumnyakua.
 
Biblia agano la kale wanayo wayahudi ambao ndio agano la kale linawahusu inaitwa Jewish Bible na ndio Biblia original na ya kale kuliko zote ipo hadi leo na haina hicho kitabu cha Henoko
Hiyo Biblia haijawahi chujwa na awaye yeyote iko hivyo hivyo hakuna aliyewahi kaa kuchuja wala kuamua kitabu kipi kiwepo na kipi kisiwepo

Na kanisa lilichukua hiyo Biblia ya agano kale kama vitabu vilivyo na kuviingiza kwenye Biblia ya sasa yenye vitabu 66

Agano la kale tumerithi toka Jewish Bible kama ilivyo na wayahudi ndio wanaitumia hadi leo

Hizo porojo za kusema kuna mtu alikaa kuchuja vitabu vya agano la kale ni uongo
Siyo kuchuja agano la kale tu, hata agano jipya.

Biblia haikushushwa kama Quruani.
Biblia imeandikwa kwa mfumo wa filtration. Kuchuja.

Maandishi yalikuwa yanakutwa kwenye magome ya miti, kwny ngozi za wanyama nk, yanakusanywa na kuamuliwa kipi ni sahihi.

Kuna mambo mengi yaliachwa, kwa mfano barua aliyoiandika Ponsio Pilato akijuta kumhukumu yesu kifo, Ni barua genuine, lakini haimo kwny vitabu vya Biblia.
 
Biblia agano la kale wanayo wayahudi ambao ndio agano la kale linawahusu inaitwa Jewish Bible na ndio Biblia original na ya kale kuliko zote ipo hadi leo na haina hicho kitabu cha Henoko
Hiyo Biblia haijawahi chujwa na awaye yeyote iko hivyo hivyo hakuna aliyewahi kaa kuchuja wala kuamua kitabu kipi kiwepo na kipi kisiwepo

Na kanisa lilichukua hiyo Biblia ya agano kale kama vitabu vilivyo na kuviingiza kwenye Biblia ya sasa yenye vitabu 66

Agano la kale tumerithi toka Jewish Bible kama ilivyo na wayahudi ndio wanaitumia hadi leo

Hizo porojo za kusema kuna mtu alikaa kuchuja vitabu vya agano la kale ni uongo
Biblia ya sasa ina kitabu cha JUdith? au TObit?
Pia kuna Maccabees 1 na Maccabees 2
 
Back
Top Bottom