Kitabu cha Henoko ni maandiko ya kale ambayo yamejaa hadithi na maono ya ki-apocalyptic, lakini hakikujumuishwa katika Biblia kwa sababu kuu ya msingi kwamba hakina uhalali wa kimungu.
Ingawa kinadai kuandikwa na Henoko, ambaye Biblia inamtaja kuwa “alitembea na Mungu” (Mwanzo 5:24), wataalamu wanaonesha kilitungwa na waandishi wa baadaye waliotumia jina lake ili kukipa uzito.
Hii inafanya kitabu hiki kuonekana kama bandia, tofauti na vitabu vya Biblia ambavyo uandishi wake ulitambuliwa na kuthibitishwa katika historia ya imani ya Wayahudi na Wakristo.
Kuna pia tatizo la mafundisho yanayopingana na Biblia.
Henoko kinadai kwamba malaika walianguka wakaoa wanawake na kuzaa majitu, jambo linalopingana na Yesu mwenyewe aliyesema malaika hawaozi wala kuolewa (Mathayo 22:30).
Kitabu hiki kinataja majina ya malaika yasiyopatikana katika maandiko matakatifu, na kutoa maelezo ya mbingu, sayari na jehanamu kwa mtindo wa hadithi na sayansi ya kale, ambayo mara nyingi yanapingana na uumbaji ulivyoelezwa katika Biblia. Haya yote yalionekana kama kuongeza hadithi na falsafa za kibinadamu ndani ya neno la Mungu.
Viongozi wa kanisa la mwanzo waliona hatari kubwa ya kuliruhusu kusomeka kama neno la Mungu kwa sababu lingeweza kupotosha imani ya waamini.
Ndiyo maana Wayahudi hawakukiweka katika Tanakh, Wakristo wengi pia hawakulijumuisha kwenye Agano Jipya, isipokuwa Kanisa la Ethiopia pekee.
Kwa kuwa msingi wa Biblia ni kuwa maandiko yote yamevuviwa na Roho Mtakatifu bila kuchanganywa na mawazo ya kibinadamu, Kitabu cha Henoko kilionekana kutofaa, kwa kuwa kilibeba mchanganyiko wa kweli kidogo na hadithi nyingi.
YESU ALISEMA WOKOVU WATOKA KWA WAYAHUDI KWASABABU WAO NDIO WALIPEWA MAUSIA YA MUNGU (YWHW)