Kitabu cha Henoko (biblia hakipo) cha kiswahili nauza 5000 Tsh

Kitabu cha Henoko (biblia hakipo) cha kiswahili nauza 5000 Tsh

Kwahiyo Ibrahim alimuona nuhu? Na Ibrahim kumbe ni wa enzi za mnara wa Babel?
Yes, Nuhu kamlea Ibrahim coz Nimrodi alitaka kumuua Ibrahim akiwa mtoto, Waganga Walimtabilia Nimrodi kwamba Kuna mtoto atakuja kuwa mwiba Kwa Utawala wake, Nimrodi akatoa Amri Ibrahim aletwe auwawe.

Baba yake anafanya hila Kwa kumpeleka mtoto wa kijakazi wake, anauwawa, then Baba wa Ibrahim anamtorosha Ibrahim mpaka Kwa Nuhu, Mungu anaanza kuongea na Ibrahim akiwa Kwa Nuhu,
 
Nikifika hapo ntakuja kueleza kuhusu maisha yake, Bado nasoma hicho Kitabu.

Mfano tunasoma kwenye Biblia Enock akatembea na Mungu basi... Ila haisemwi hasa alitembeaje na Mungu, na kumbuka Enock alikua Binadamu kama sisi, ila ukisoma hivyo Vitabu Kwa kile Enock alifanya Kwa ajiri ya Mungu, unaelewa kweli ilikua haki yake kutoonja Mauti, Enock muda alioutumia na Mungu tu Kwa maana ya kuongea naye ni mkubwa kuliko aliotumia kufanya mambo mengine.

Kuna wakati Enock atashuka mjini kufundisha ama kuhubiri habari za Mungu, labda week 1, then akimaliza anaondoka kwenda Milimani kuongea na kukaa mbele za Mungu Mwaka mzima, baada ya mwaka atashuka mjini kuhubiri mwezi mmoja Kisha atapndoka kwenda kukaa mbele za Mungu miaka 2.

Ikafikia kipindi akija mjini, Watu Toka Mataifa wanakusanyika maelfu kumsikia, kuwaponya na kutatua changamoto zao, anapowaaga kwamba anaondoka kwenda kuwa karibu na Muumba wake, wanang'ang'ania Waende wote ili wamsindikize, anawambia Mtakufa mkisogea eneo jirani na ninapokua nakaa mbele za Mungu, Watu ni wabishi, Enzi za Enock washakufa Watu wengi pale walipomsindikiza Enock mpaka jirani na alipokua anakaa na kuongea na Mungu.

Kitabu kinasema Mungu alimwambia Kwa kazi aliyofanya hatakufa, hivyo arudi mjini akawaage Watu, so alirudi akawaaga Watu akiwaambia Mungu anamtwaa Mbinguni, kama kawaida maelfu ya Watu waliondoka nae wakisema wamsindikize na hawakurudi, walikufa walipokaribia uwepo wa Mungu....!

So Kwa habari ya Enock nikasema Yes. .. alistahili.
Mwaka 2020 niliutumia mda mwingi kukaa mbele za MUNGU niliona mengi sana

MUNGU ni mwema sana
 
Yes, Nuhu kamlea Ibrahim coz Nimrodi alitaka kumuua Ibrahim akiwa mtoto, Waganga Walimtabilia Nimrodi kwamba Kuna mtoto atakuja kuwa mwiba Kwa Utawala wake, Nimrodi akatoa Amri Ibrahim aletwe auwawe.

Baba yake anafanya hila Kwa kumpeleka mtoto wa kijakazi wake, anauwawa, then Baba wa Ibrahim anamtorosha Ibrahim mpaka Kwa Nuhu, Mungu anaanza kuongea na Ibrahim akiwa Kwa Nuhu,
Alooo

Abalikiwe MWENYEZI MUNGU aliyeziumba mbingu na inchi
 
Yes, Nuhu kamlea Ibrahim coz Nimrodi alitaka kumuua Ibrahim akiwa mtoto, Waganga Walimtabilia Nimrodi kwamba Kuna mtoto atakuja kuwa mwiba Kwa Utawala wake, Nimrodi akatoa Amri Ibrahim aletwe auwawe.

Baba yake anafanya hila Kwa kumpeleka mtoto wa kijakazi wake, anauwawa, then Baba wa Ibrahim anamtorosha Ibrahim mpaka Kwa Nuhu, Mungu anaanza kuongea na Ibrahim akiwa Kwa Nuhu,
Ibrahim,Nuhu na Nimrod walikua kipindi kimoja?
 
Mimi naamini ni kitabu halali kuwepo kwenye biblia na mpaka sasa kwenye biblia kipo ila wajanja walikitoa ila walishindwa kutoa maandiko yake. Kama walikua na nia ya kukitoa basi wangetoa na maandiko yake yaliyo wekwa kwenye biblia.
Sio kitabu halali, na ndio maana kipo kama cha hadithi tu,

Wayahudi ambao ndio walikabidhiwa MAUSIA ya Mungu na wakayatunza ,hawajawahi kukiweka kwenye TANAKJ, Yesu anakuja wayahudi Wana maandiko hiko kitabu na wenzake kina makabayo havikuhesabiwa ni vitabu vya uvuvio
 
Kitabu cha Henoko (biblia hakipo) cha kiswahili nauza 5000 Tsh. Tuma pesa M-PESA kwenda namba 0756704145 nicheki WhatsApp nikutumie kitabu au kama una email natuma
Umetafsiri kwa Chatgpt au una kile cha mkenya aliyetafsiri vibaya? Malizeni kwanza biblia, Henoko msome ukiisha ijua biblia.
 
Umetafsiri kwa Chatgpt au una kile cha mkenya aliyetafsiri vibaya? Malizeni kwanza biblia, Henoko msome ukiisha ijua biblia.
Nimetafsiri mwenyewe kwa mbinu zangu hakuna Cha chatGPT Wala mkenya kipo vizuri jipatie kopi 0756704145, Bei 5000
 
Mwanzoni Nimrodi alikua anatembea kwenye njia ya Mungu, baadaye akamwasi Mungu akaanza kupambana na Kila ambaye anajihusisha na Mungu Mkuu.

Ibrahim alinusurika kuuwawa baada ya kutoka alipokua akiishi Nuhu (Alienda kuishi Kwa Nuhu) akarudi alipozaliwa akakuta Baba yake anaabudu Masanamu, akayavunja Kwa hasira, Baba yake Ibrahim akaenda kumshitaki Kwa Nimrodi, Nimrodi akapitisha Hukumu atupwe kwenye Shimo la Moto ili afe......! Nchi Ile ikawa na Uasi mwingi na walikua na hasira na Mungu wa Israel, wakaona wanaweza kupambana naye, Kwa Vile ulikua Ufalme wenye Nguvu Enzi hizo, wakatiana Ujinga wajenge Mnara ili wafike Mbinguni wakapambane na Mungu, kwenye hivi Vitabu, wameelezea Vizuri sana, Visa vingi ambavyo kwenye Biblia vimeandikwa kifupi, wakati huko wameelezea Mwanzo mpaka mwisho wa Kila kisa.
Asante,kuna umuhimu wa kusoma
 
Binafsi nakisomq Kitabu Cha Enock, pia nimekisoma Kitabu Cha Japher...!

Kwa Mtu ambaye unataka sana kujua mambo ya Kiroho, hivi Vitabu vina baadhi ya vitu vitakusaidia kwenye safari Yako ya Mambo ya kiroho.

Ila Kwa Kitabu kama Cha Enock zipo sababu za Msingi hasa ambazo hata Mimi nakubari kwamba ilikua sahihi kutojumuishwa kwenye Biblia, mfano Kuna sehemu Lamech anaenda kumuomba Methuselah ambaye ni Baba yake, ili Waende ku communicate na Enock Babu ya Lameck juu ya Mtoto ambaye alizaliwa kimaajabu (Melekizedeki) kama alikua ni Mtoto wake, na kumbuka hapo Enock alikua tayari ameshakufa kitambo, means Methuselah alikua ana ujuzi wa kuongea na Spirit ya Baba yake, alikua anajua namna ya kuiita....!

So vitu kama hivyo nakubari kabisa havikua na uhalali wa kuwepo kwenye Biblia n.k

All in all ukisoma hivyo Vitabu na Kitabu kingine kama Jubilee, Kuna missed part ambazo unaziona Wazi kabisa kwenye Biblia na Majibu yake yapo humo kwenye hivyo Vitabu.

Mfano Biblia imegusia kidogo sana kuhusu Melekizedeki kwamba hakuwa na Baba Wala Mama, na kwamba alikua Kuhani Mkuu, ambaye mpaka Ibrahim alimpa sehemu ya 10, ila kwenye hivyo Vitabu unaona mwanzo wake mpaka mwisho wake.

Kwenye Biblia tunasoma tu Ibrahim anaambiwa na Mungu aondoke kwenye Nchi yake na kwenda Nchi ya Ugenini.

Ila kwenye hivyo Vitabu tunaona kuzaliwa Kwa Ibrahim, kukua kwake mpaka Mungu alipoanza kusema na yeye, tunaona Ibrahim akiishi enzi za Nimrodi, na masaibu aliyopitia Enzi za Utawala wenye Nguvu wa Nimrodi n.k

Kwenye Biblia tunasoma Kwa uchache kuhusu Nimrodi, ila kupitia hivyo Vitabu tunaona kuzaliwa Kwa Nimrodi, kumuamini Mungu mpaka kuja kuasi na kuanza kujenga ule mnara.

Kwenye Biblia hatuoni sana kuhusu Mavazi ambayo Adam na Eva walijifunika Kwa mara ya kwanza baada ya kiasi, ila kwenye hivyo Vitabu tunaona Adamu kabla ya kufa, alimkabidhi yale Mavazi Seth, Seth akakabidhi Kwa Mwanae, hivyo hivyo mpaka Kwa Enock, ni hivyo hivyo Mavazi Yale Nimrodi aliyaiba Kwa hila, na siku anayavaa, hakuwa yule Tena wa zamani n.k

So Kwa Mimi Kuna Vitu vingi vya kiroho najifunza.
Dah,
Kweli elimu ni kama Bahari
 
Asante,kuna umuhimu wa kusoma
Sahihi.....! Sio Kwa Lengo la kukitumia kufundisha coz Neno la Mungu limekua limited tayari Toka Kwa Biblia, ila Kwa faida Yako mwenyewe, hivi Vitabu vinawafaa sana Pastors, Apostles, Prophets na wengine.

Kuna Vitu vya kujifunza coz Visa vyote vimeandikwa Kwa marefu sana, na visa vilevile na Wahusika walewale wa kwenye Biblia.
 
Ibrahim,Nuhu na Nimrod walikua kipindi kimoja?
Nuhu alikua Mzee zaidi kuliko wote hao Kwa Mujibu wa hivyo Vitabu.

The book of Japher kinaeleza wakati Ibrahim anamuaga Nuhu ili kurudi mji alipozaliwa alikua na Miaka 50 anasemwa alikua Bado Kijana Mdogo Kwa Umri huo coz zamani hizo watu waliishi miaka 900, 800, 700...!

Ibrahim anazaliwa Nimrodi alikua Mfalme, mpaka anapotoka Kwa Nuhu kurudi Kwa Baba yake, Bado Nimrodi alikua Mfalme...!

Kwa mfano Enock alikua kizazi Cha 7 Toka Adam, na Kitabu kinasema Enock alimuona Adam Kwa macho akiwa Bado Kijana Mdogo.
 
Kitabu cha Henoko (biblia hakipo) cha kiswahili nauza 5000 Tsh. Tuma pesa M-PESA kwenda namba 0756704145 nicheki WhatsApp nikutumie kitabu au kama una email natuma
Ni kile kilichofutwa na wanadamu kinachohusu malaika waliozaa na binadamu?!

Vipo viwili lete tuvisome
 

Attachments

  • ab1c897ad3075981109995c337ef4e62_1755623497045.mp4
    4.8 MB
Henoko kinadai kwamba malaika walianguka wakaoa wanawake na kuzaa majitu, jambo linalopingana na Yesu mwenyewe aliyesema malaika hawaozi wala kuolewa (Mathayo 22:30).
Mkuu,
Mbona hayo yamo ndani ya Biblia na ndiyo sababu moja wapo ya gharika?

Mwanzo 6:
4 Nao Wanefili<br> walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

5 BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

6 BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.

8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
 
Back
Top Bottom