Kuhusu nilipo Bold 👆🏽 Mbona hata katika Biblia kuna tukio la mtu aliyeenda kwa mtaalamu ili kuwasiliana na aliyekufa, Mfalme Sauli aliyekwenda kwa mwanamke wa Endori mchawi/mtaalamu wa pepo, ili kujaribu kuwasiliana na Nabii Samweli ambaye alisha kufa.
1 Samweli 28:7
“Sauli akawaambia watumishi wake, ‘Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea ili niulize kwake".
Na Roho ya Samweli ikaonekana kwenye andiko hili
1 Samweli 28:12-15 (SUV):
12) Na yule mwanamke alipomwona Samweli, akapiga kelele kwa sauti kuu; yule mwanamke akamwambia Sauli, Kwa nini umenidanganya? Maana wewe ndiwe Sauli.
13) Mfalme akamwambia, Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu akitoka katika nchi.
14) Akamwambia, Anafanana na nini? Akasema, Ni mzee anayetoka juu, amefunikwa joho. Sauli akatambua ya kuwa ni Samweli, akainama kifudifudi, akasujudu.
15) Samweli akamwambia Sauli, Kwa nini umenisumbua kwa kunileta juu?
Ni sahihi Mkuu..... Sio mara ya kwanza Kwa Spirit za Watu waliokufa kuja Duniani, sio wakati huu tu, ilitokea Toka Enzi za Biblia, ama Kwa kuitwa ama Kwa hizo Spirit kuja zenyewe.
Zilikuja Kwa Yesu mwenyewe, Spirit za Mussa na Eliya, Kwa Sauli kama ulivyonukuhu (Kwa kuitwa) na maeneo mengine.
Ila wakati Yesu yupo kwenye maombi zile Spirit zilikuja Zenyewe, na wote tunafahamu Elia na Mussa walikua ni Watumishi wa Mungu, ni hivyo hivyo Kwa Enock, Lameck hata Methuselah, ila inapotokea Kwa Mganga wa Kienyeji kuipandisha Spirit ya Mtumishi wa Mungu inaleta Udadisi.
Africa hapa ni mambo ya kawaida haya, tunaita Mila na Desturi, ila point ya Msingi nadhani baada ya kuzipandisha hizo Spirit Nini hufatia....!? Kuziabudu, kuzipa majukumu ya Mungu, that's why Vile Biblia imesema hakuna uhusiano na waliokufa, inazuia Watu kufanya mambo wakijua ni Kwa ajiri ya Mungu kumbe Shetani anatumia njia hiyo hiyo Kwa ajiri ya utukifu wake mwenyewe.
South Africa Kuna tatizo, wameingiza Upagani kwenye Ukristo, watu wanaenda Kwa Waganga wakaitwa Manabii, ila hawana Makanisa, na wanatumia Biblia, Maji, Chumvi na wengine wanatumia Madawa Toka Kwa Miti maarufu, Hawa Wana uwezo kuita Spirit za Marehemu zikija kujibu maswali ama kutoa Suluhu za Matatizo ya Mtu ama familia, na wanasema Kwa Nini Kwa Yesu ionekane ni sawa, kwetu Waafrika iwe tatizo, wanasema mbona Alifanya Sauli na Spirit ya Samweli ikaja, Kwa Nini wao iwe tatizo.
Ukiangalia wao wanazitumia hizo Spirit kujaribu kutatua changamoto za familia, na sote tunajua nyumba ya Spirit chafu Kuna Majini ama Mapepo, so Watu kujikuta kuabudu Shetani bila kujua....! Kwa kujua yote hayo Biblia imekataza Watu wa Mungu ku communicate na waliolala.