Kitabu cha Henoko (biblia hakipo) cha kiswahili nauza 5000 Tsh

Binafsi nakisomq Kitabu Cha Enock, pia nimekisoma Kitabu Cha Japher...!

Kwa Mtu ambaye unataka sana kujua mambo ya Kiroho, hivi Vitabu vina baadhi ya vitu vitakusaidia kwenye safari Yako ya Mambo ya kiroho.

Ila Kwa Kitabu kama Cha Enock zipo sababu za Msingi hasa ambazo hata Mimi nakubari kwamba ilikua sahihi kutojumuishwa kwenye Biblia, mfano Kuna sehemu Lamech anaenda kumuomba Methuselah ambaye ni Baba yake, ili Waende ku communicate na Enock Babu ya Lameck juu ya Mtoto ambaye alizaliwa kimaajabu (Melekizedeki) kama alikua ni Mtoto wake, na kumbuka hapo Enock alikua tayari ameshakufa kitambo, means Methuselah alikua ana ujuzi wa kuongea na Spirit ya Baba yake, alikua anajua namna ya kuiita....!

So vitu kama hivyo nakubari kabisa havikua na uhalali wa kuwepo kwenye Biblia n.k

All in all ukisoma hivyo Vitabu na Kitabu kingine kama Jubilee, Kuna missed part ambazo unaziona Wazi kabisa kwenye Biblia na Majibu yake yapo humo kwenye hivyo Vitabu.

Mfano Biblia imegusia kidogo sana kuhusu Melekizedeki kwamba hakuwa na Baba Wala Mama, na kwamba alikua Kuhani Mkuu, ambaye mpaka Ibrahim alimpa sehemu ya 10, ila kwenye hivyo Vitabu unaona mwanzo wake mpaka mwisho wake.

Kwenye Biblia tunasoma tu Ibrahim anaambiwa na Mungu aondoke kwenye Nchi yake na kwenda Nchi ya Ugenini.

Ila kwenye hivyo Vitabu tunaona kuzaliwa Kwa Ibrahim, kukua kwake mpaka Mungu alipoanza kusema na yeye, tunaona Ibrahim akiishi enzi za Nimrodi, na masaibu aliyopitia Enzi za Utawala wenye Nguvu wa Nimrodi n.k

Kwenye Biblia tunasoma Kwa uchache kuhusu Nimrodi, ila kupitia hivyo Vitabu tunaona kuzaliwa Kwa Nimrodi, kumuamini Mungu mpaka kuja kuasi na kuanza kujenga ule mnara.

Kwenye Biblia hatuoni sana kuhusu Mavazi ambayo Adam na Eva walijifunika Kwa mara ya kwanza baada ya kiasi, ila kwenye hivyo Vitabu tunaona Adamu kabla ya kufa, alimkabidhi yale Mavazi Seth, Seth akakabidhi Kwa Mwanae, hivyo hivyo mpaka Kwa Enock, ni hivyo hivyo Mavazi Yale Nimrodi aliyaiba Kwa hila, na siku anayavaa, hakuwa yule Tena wa zamani n.k

So Kwa Mimi Kuna Vitu vingi vya kiroho najifunza.
 
Maelezo mazuri,nitafanya utaratibu nivisome,hivi huo mnara ni kweli ilikuwa mnara wa kwenda juu mbinguni au kuna vitu walikusudia maana sidhani kama mnara ungefika mbinguni?
 
Umemaliza mtumish
 
Shusha nondo kidogo hapo kwa rafiki yangu melikizedek alizaliwaje huyu mtumish na aliishi maisha gan
 
Maelezo mazuri,nitafanya utaratibu nivisome,hivi huo mnara ni kweli ilikuwa mnara wa kwenda juu mbinguni au kuna vitu walikusudia maana sidhani kama mnara ungefika mbinguni?
Mwanzoni Nimrodi alikua anatembea kwenye njia ya Mungu, baadaye akamwasi Mungu akaanza kupambana na Kila ambaye anajihusisha na Mungu Mkuu.

Ibrahim alinusurika kuuwawa baada ya kutoka alipokua akiishi Nuhu (Alienda kuishi Kwa Nuhu) akarudi alipozaliwa akakuta Baba yake anaabudu Masanamu, akayavunja Kwa hasira, Baba yake Ibrahim akaenda kumshitaki Kwa Nimrodi, Nimrodi akapitisha Hukumu atupwe kwenye Shimo la Moto ili afe......! Nchi Ile ikawa na Uasi mwingi na walikua na hasira na Mungu wa Israel, wakaona wanaweza kupambana naye, Kwa Vile ulikua Ufalme wenye Nguvu Enzi hizo, wakatiana Ujinga wajenge Mnara ili wafike Mbinguni wakapambane na Mungu, kwenye hivi Vitabu, wameelezea Vizuri sana, Visa vingi ambavyo kwenye Biblia vimeandikwa kifupi, wakati huko wameelezea Mwanzo mpaka mwisho wa Kila kisa.
 
Shusha nondo kidogo hapo kwa rafiki yangu melikizedek alizaliwaje huyu mtumish na aliishi maisha gan
Kwenye Kitabu Cha Japher kinaeleza Lameck alikua Mchungaji, akitumia muda wake madhabahuni, angeenda huko kwenye madhabahu na kukaa mwaka mzima akimtumikia Mungu, Kuna siku anarudi, akamkuta Mke wake ni Mjamzito wa Mimba kubwa tu.

Akamwambia wakati Mimi naenda kumtumikia Mungu wewe ukaamua kunisaliti!?
Mke akaapa kwamba yeye hajatembea nje ya Ndoa, ameshangaa kujiona Mjamzito, Lameck hamuamini, na Kwa vile alikua Mtumishi wa Mungu, Kuna maneno akaongea kama Laana Kwa mke wake, akaondoka kwenda Kwa Baba yake Methuselah, akamwelezea kile kilichotokea, Methuselah akarudi na Mwanae Lameck ili atatue tatizo, walipoingia ndani wakakuta Mke wa Lameck kafa, kalala Chali kitandani, na lile Tumbo la Ujauzito halipo Tena, ila wanashangaa kumkuta mtoto kakaa kitandani, mtoto wa Umri kama miaka 2, Mtoto mwenyewe ndiyo Melekizedeki aliyekuja kuwa Kuhani Mkuu ambaye Biblia inamtaja kama asiye na Baba Wala Mama, asiye na Mwanzo Wala mwisho......!

Babaye Lameck anamwambia Mwanae Kwa namna Mungu alivomletq huyu mtoto, watu wa Jamii yetu wakisikia watamuua, akamwambia Amtoe, ampeleke Kwa Nuhu, wakati huo Nuhu alikua anaishi mji mwingine, so Melekizedeki kalelewa na Nuhu.

Wakati Nuhu anajenga Safina Malaika alikuja Kwa Nuhu, akamwambia Mungu amenituma nije kumchukua mtoto, Kwa kile anachokwenda kuifanya hii Dunia hataki huyu Mtoto ashuhudie, ila nitamrudisha kwako baada ya gharika so Nuhu alikubari, Malaika akaondoka na Melekizedeki na baada ya gharika alimrudisha, Nuhu alimlea Melekizedeki mpaka alipokua mkubwa akaanza kumtumia Mungu kama Kuhani wake...!
 
Asante sana mtumish

Katika kuishi kwa melikizedek maisha yake yalikuwaje

Je Kuna chochote ambacho anaelezewa juu ya maisha yake binafis
 
Kwahiyo Ibrahim alimuona nuhu? Na Ibrahim kumbe ni wa enzi za mnara wa Babel?
 
Asante sana mtumish

Katika kuishi kwa melikizedek maisha yake yalikuwaje

Je Kuna chochote ambacho anaelezewa juu ya maisha yake binafis
Nikifika hapo ntakuja kueleza kuhusu maisha yake, Bado nasoma hicho Kitabu.

Mfano tunasoma kwenye Biblia Enock akatembea na Mungu basi... Ila haisemwi hasa alitembeaje na Mungu, na kumbuka Enock alikua Binadamu kama sisi, ila ukisoma hivyo Vitabu Kwa kile Enock alifanya Kwa ajiri ya Mungu, unaelewa kweli ilikua haki yake kutoonja Mauti, Enock muda alioutumia na Mungu tu Kwa maana ya kuongea naye ni mkubwa kuliko aliotumia kufanya mambo mengine.

Kuna wakati Enock atashuka mjini kufundisha ama kuhubiri habari za Mungu, labda week 1, then akimaliza anaondoka kwenda Milimani kuongea na kukaa mbele za Mungu Mwaka mzima, baada ya mwaka atashuka mjini kuhubiri mwezi mmoja Kisha atapndoka kwenda kukaa mbele za Mungu miaka 2.

Ikafikia kipindi akija mjini, Watu Toka Mataifa wanakusanyika maelfu kumsikia, kuwaponya na kutatua changamoto zao, anapowaaga kwamba anaondoka kwenda kuwa karibu na Muumba wake, wanang'ang'ania Waende wote ili wamsindikize, anawambia Mtakufa mkisogea eneo jirani na ninapokua nakaa mbele za Mungu, Watu ni wabishi, Enzi za Enock washakufa Watu wengi pale walipomsindikiza Enock mpaka jirani na alipokua anakaa na kuongea na Mungu.

Kitabu kinasema Mungu alimwambia Kwa kazi aliyofanya hatakufa, hivyo arudi mjini akawaage Watu, so alirudi akawaaga Watu akiwaambia Mungu anamtwaa Mbinguni, kama kawaida maelfu ya Watu waliondoka nae wakisema wamsindikize na hawakurudi, walikufa walipokaribia uwepo wa Mungu....!

So Kwa habari ya Enock nikasema Yes. .. alistahili.
 
Mimi naamini ni kitabu halali kuwepo kwenye biblia na mpaka sasa kwenye biblia kipo ila wajanja walikitoa ila walishindwa kutoa maandiko yake. Kama walikua na nia ya kukitoa basi wangetoa na maandiko yake yaliyo wekwa kwenye biblia.
 
Bro remember the name mtumish Beira boy nitag kila hatua ya uzuri wa hicho kitabu

Usiache mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…