Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Watu kadhaa wameniuliza ukweli kuwa kuundwa kwa Yanga mwaka wa 1936 ilikuwa mbinu ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Haya nimeambiwa yameandikwa katika kitabu cha historia ya Yanga ambacho kimetolewa hivi majuzi.
Jibu langu kwao ni kuwa ushahidi wa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika hauonyeshi hivyo.
Historia ya TANU inaanza na historia ya African Association mwaka wa 1924 katika mazungumzo ya Kleist Sykes na Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Achimota College, Ghana.
Dr. Aggrey alimshauri Kleist Sykes Waafrika wa Tanganyika waunde chama chao kama walivyofanya Wazungu (European Association) na Waasia (Indian Association).
Mwaka wa 1929 African Association ikaundwa waasisi wakiwa Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Humbi Ziota, Raikes Kusi na Watson Watts.
Mwaka wa 1948 African Association ikabadili jina lake ikawa Tanganyika African Association (TAA) Thomas Saudtz Plantan akiwa President na Clement Mohamed Mtamila Secretary.
Mwaka wa 1950 yakafanyika mapinduzi yaliyowatoa viongozi hawa madarakani kwa nguvu.
Serikali ikaamrisha TAA ifanye uchaguzi wa viongozi.
Uchaguzi ukawaingiza madarakani Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdul Sykes (Secretary).
Uongozi huu ukaunda TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Kamati hii kwa msaada wa Mwanasheria Earle Seaton ndiyo iliyofungua mawasiliano na UNO kuhusu Tanganyika kama nchi inayotawaliwa chini ya udhamini wa Uingereza.
Kamati hii kupitia juhudi za Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ndiyo iliyomuingiza Julius Nyerere katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953 na mwaka wa 1954 TANU ikaundwa Nyerere akiwa President.
Kwa kifupi hivi ndivyo TANU ilivyoundwa na hii ndiyo historia yake.
Kuwa Yanga iliasisiwa mwaka wa 1936 kudai uhuru hili halina ushahidi wowote.
Atakae kujua zaidi kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika atazame video hiyo hapo chini:
View: https://youtu.be/b0wV_rF1W20?si=c_f8lKCVXRqd_GGE