Kitabu cha kabendera ni hadithi za kufikirika na sio Facts, Serikali ipeleke Shitaka Mahakamani

Makamu alinyatiwa na jiwe ili alipwe kipapa. Chukuwa hiyo mkuu.
 
What if akawa na kila ushahidi na ukawekwa hadharani?

Sio kila jambo unalikimbilia tu. Utajiaibisha mwenyewe.
 
Umethibitisha vipi kama aliua mtu Ikulu?
Likija shirika huru la uchunguzi utapata ukweli wote na zaidi. Kwa sasa huwezi kuona ushihidi huo, maana kuna mfumo unaolinda huo uovu.
 
Nani kakuambia data na evidence huwekwa kwenye kitabu...?

Mfano kwenye Biblia tunasoma simulizi ya matukio mengi sana, kwa mfano;

1. Mussa alitupa fimbo chini mbele ya Farao na waganga na wachawi wake na fimbo hiyo kugeuka nyoka. Unaiona fimbo na nyoka huyo amebandikwa kwenye maandishi hayo...?

2. Daudi alilipiga jitu kubwa liitwalo Goliath (Mfilisti) na kuliua papo hapo kwa jiwe la kombeo. Je, kwenye maandishi hayo unaona picha ya Daudi na Goliath kwani kama ushahidi...?

3. Yesu Kristo alimfufua Lazaro aliyekufa na kukaa kaburini siku 4 akawa ananuka. Unamwona Lazaro au kaburi lake limebandikwa kwenye maandishi hayo kama ushahidi..?

##Katika haya yote ni wewe kuamini au ukae hivyo na kutoamini kwako. Kwa kuwa huamini, unaweza pia kumdai ushahidi wa matukio yote haya Mungu wa mbinguni kama Tomaso aliyesema "mimi siamini kama Yesu amefufuka unless nimeona alama za misumari mwilini mwake...!!"

##Ninachotaka kukuambia ni kuwa, kusoma simulizi ya matukio kwenye maandishi ni kitu kimoja. Na ushahidi wa tukio unalolisoma hauwezi kuwekwa kwenye kitabu zaidi ya kujua wahusika wa matukio hayo nani alifanya nini...

Mfano, watu waliona tukio fulani unataka watajwe na wapigwe picha na zibandikwe kwenye kitabu? Ili wahusika wawajue na kuwatafuta wawadhuru kwa kuwa siri zao zimejulikana kupitia wao..?

##Sikiliza bwana. Erick Kabendera kaandika kitabu (Non Fiction Literature) based on true events through his private investigation. Kitu kizuri ni kwamba kuna watu wametajwa humo kwa vyeo na majina yao...

##Kama wanataka kupewa ushahidi na mwandishi (mchunguzi & mwandishi) there are two ways to get it:

1. Wameshamsikia mpiga filimbi (whistleblower). Mamlaka huru za uchunguzi (sio za serikali maana ndizo zinatuhumiwa) ziingie kazini zijichunguze ili kuuthibitisha ukweli wa haya mambo. Wakikuta ndivyo sivyo, wachukue hatua... AU;

2. Ushauri wako ufanyiwe kazi. Anayedhani ameumizwa au amethumiwa kimakosa, aende mahakamani aombe ushahidi toka kwa mwandishi na akishindwa kuthibitisha, awasafishe aliowanenea uongo na ikibidi alipe fidia ya "uharibifu wa sifa za watu..!

Na ushahidi ukithitisha kweli walihusika, wawe tayari nao kunyongwa mpaka kufa kwa sababu wao nao waliua. Bahati njema ni kuwa, mtuhumiwa mkuu John P. Magufuli yeye anatumikia adhabu ya karma (kifo) kaburini kwa sasa..!!
 
Naamini kitabu hiki kwa 90% Magufuli alifanya ushenzi mwingi sana nchi hii na wananchi wana endelea kulipa. Mfano ni wastaafu kutolipwa hela zao zote kwa mkupuo kama awali kwani Magufuli aliingilia mfuko wa pensheni na kuchota matrilioni kujenga madaraja na sasa wazee wastaafu ndio wanateseka. Hayo yatasemwa baadaye ngoja sasa tusikilize haya ya pyjama ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…