UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Hilo swali ulilong'ang'ania la kuuliza uchawi ni nini? Mwenyewe uliniambia kwamba hausemi kuwa haijulikani uchawi ni nini bali unataka tu definition ya uchawi kutoka kwetu sisi. Kuna definition nyingi tu za neno uchawi na nilishakwambia hata sisi tunaoamini uchawi tunatofautiana kwenye definition ya uchawi, sasa kama lengo lako ni kujadili definition za neno uchawi bora useme ili tuingie huko tujadili maana ya uchawi.Nimeuliza hivi.
Toa definition ya uchawi.
Mpaka sasa hujatoa.
Pia nikauliza hivi.
Hicho unachofikiri ni uchawi unahakikishaje kuwa ni uchawi kweli na si kitu kingine tofauti na uchawi ambacho hujakielewa vizuri tu?
Hujajibu.
Uchawi ni nini?
Hicho unachokiita uchawi unahakikishaje ni uchawi kweli na si kitu tofauti tu ambacho labda hujakielewa vizuri tu?
1)Ni kweli kuna baadhi ya vitu naweza kudhania au kusema kitu fulani ni uchawi kwa mtazamo wangu tu binafsi lakini kumbe ikawa si uchawi kikawa kitu chengine, ni sawa na kudhania mtu ana malaria kumbe ana homa tu, kwahiyo vipimo ndio vitafanya tupate kujua ukweli kama ni kweli malaria au kitu kingine na kwenye uchawi ni hivyo hivyo kuna njia ama ujuzi wa kuweza kufahamu jambo au tatizo fulani ni uchawi ama kitu kingine.
2) Kwanini nifikirie tu hicho kinachoitwa kuwa ni uchawi kwamba kinaweza kuwa si uchawi bali ni kitu chengine hali ya kuwa sijui hicho kitu chengine ni kitu gani wala sikielewi? Ni wazi mpaka niwe na sababu za kufanya nifikiri hivyo, wewe unayepinga uwepo wa uchawi unayo sababu ya kufikiri hivyo kwa mambo ambayo yenye kuhusishwa na uchawi na ambayo huyaelewi kwa sababu hauamini uchawi.