Ndugu zangu wana JF, mimi ni mtanzania na ninapenda kuwafahamisha kuwa ninaandika kitabu chenye kutoa ushahidi juu ya kutokuwepo mungu wala uchawi katika dunia hii.
Najua wengi wenu mkisia mada kama hii mnapuuza na kucheka. Yawezeka vicheko vinatokana na kuelewa sana juu ya chimbuko la dhana hii ya Mungu na uchawi au kutokuelewa kabisa.
Kuelewa chimbuko ni heri lakini kutokuelewa ina maana mimi na wewe tumekalilishwa mambo tusiyojua chimbuko lake.
kwa kifupi, hakuna binadamu anayeweza kufurahia kutokuwepo kwa Mungu lakini kujiaminisha juu ya uwepo wake kama ukweli ni hayupo basi kuamini yupo hakutusaidii na kule kusema hayupo kama yupo hakutusaidii.
Zipo faida za kujua ukweli na zipo hasara za kujua ukweli lakini daima tunaimba ukweli ndiyo utatuweka huru.
Mijadala kama hii ya Uwepo au Kutokuwepo kwa Mungu imekuwepo dunia tangu kale enzi za plato lakini kiukweli ni lazima tutambue kuwa ukweli juu ya jambo hili siyo rahisi kuupata kwa kufanya malumbano ya hoja au "debate".
Ukweli juu ya jambo umekaa katika ugunzi wa siri iliyojificha nyuma ya pazia la imani ni nini?
Kosa kubwa walilolifanya mababu zetu na wanaloendelea kulifanya mpaka leo katika mambo ya imani ni kuamini sauti wasizozitambua. Kwamba anatokea binadamu mmoja anasikia sauti ikimwambia mimi ni babu yako nenda kafanye moja mbili tatu, basi binadamu huyu kuamini kuwa kweli nilikuwa nikizungumza na babu yangu na kufuata maelekezo aliyopewa ndilo kosa la kwanza.
Je kama huyu tunayesema kusikia sauti ikisema mimi ni babu yako kapewa maelekezo akafuata ni kosa, je yule anayesikia sauti ikimwambia mimi ni mtakatifu fulani au ni jina fulani lolote kubwa la kiimani nakuwa sahihi?
hapa kuna mtego ambao ni kujua je ni kitu gani kiliwasiliana na hawa na kutambua kama kweli ni hicho hicho kilichojitangaza kuwa ndicho na hiyo ndiyo siri ya ugunduzi nyuma yaimani.
yeyote asiyejua siri hiyo atabaki kutumia mambo yaleyale aliyoelezwa mtu mwingine kutetea maagizo bila kuwa na ushahidi wa kujua ni kitu gani.
Kaa Tayari kujua nyuma ya mapazia ya imani kuna nini?
lakini shaka yangu ni juu ya mitizamo ya jamii juu ya imani kwa maana hawaruhusu mtu yeyote ku challenge imani zilizopo.
Kama Diamond alifungiwa mziki wake kwa kupokea simu kanisani basi mimi najiuliza hivi kitabu changu hiki kitaruhusiwa?
Neno moja niwakumbushe watanzania ni kuwa zamani zilikuwepo imani za jadi, mababu zetu walitetea na kuzilinda imani hizo kuliko sisi tunavyofanya leo lakini leo hii imani hizo tunaziona za kipuuzi na kuziita za kishetani. Hii inatufundisha kuwa upo uwezekano wa imani tulizo nazo leo na kuziona za maana huko mbeleni kuonekana za kipuuzi hivyo tumsimpuuze yeyote mwenye kutaka kusema jambo juu ya imani zetu.