Mimi nadhani hujatumia akili yako vyema kutafuta je Mungu yupo au hayupo??!!.
Matokeo ya mambo au vitu kuwepo kwavyo na kutenda nidhamu ni ishara ya kuwepo kwa A Supreme conscious being, hii ni upembuzi wa akili ya kawaida tu bila kutumia vitabu au imani za kidini.
Hebu leo chunguza Kompyuta au programmed Robot, Vifaa hivyo vinafanya kazi kwa nidhamu iliyokusudiwa, nidhamu hiyo kaitengeneza mtu/Engineer aliyesanifu vyombo hivyo, katika utendaji kazi wa vifaa hivyo haiwezekani leo mtu azuke tu na adai kwamba kompyuta au Robot kwa utendaji kazi wake zimezuka zenyewe au zimejiunda zenyewe!!!.
Chukua mfano huo huo wa utendaji kazi wa Kompyuta na Robot na geuza huo mfano kwa ajili yako wewe mwenyewe na Mwili wako, Katika mwili wako kuna jinsia, je hiyo jinsia uliiomba wewe, yaani uliomba uzaliwe na jinsia hiyo??, au wazazi wako walitaka wewe uwe na jinsia hiyo??-- je ni nani alipanga uwe na jinsia hiyo??!!, Je, ni nani alipanga wazazi wako wawe ni hao ulionao??!!, kabila lako, race yako nk, ni nani alipanga??!!, katika mwili wako kuna mifumo ifuatayo 1-- mfumo wa upumuaji, 2-- mfumo wa umeng'enyaji, 3-- mfumo wa damu, 4--- mfumo wa fahamu, 5--mfumo kusikia, 6--- mfumo wa uzazi nk, mifumo yote hii inafanya kazi katika nidhamu kusudiwa, je ni nani aliyeweka hii nidhamu kusudiwa katika huo mwili wako na ili iweje??!! au hiyo mifumo ulijiwekea wewe mwenyewe na ukaipatia hizo nidhamu za utendaji kazi??!!--- kama Kompyuta, Robot na Magari na mitambo mbalimbali zimeundwa na Wataalamu na zina mifumo inayofanya kazi katika nidhamu kusudiwa sasa iweje upinge kwamba wewe hujaundwa na ndio maana mwilini mwako kuna mifumo inayofanya kazi kwa nidhamu tena nidhamu kusudiwa na huyo aliyekuunda??!!--- sio katika mwili wako tu bali hata katika viumbe hai wengine unaweza kujifunza kwani na wao wanavyo vitu ambavyokwavyo mtu anaweza kujifunza kwamba na wao wametengenezwa katika nidhamu ili kukidhi haja kusudiwa, haja iliyowekwa na mtengenezaji wao kwani hakuna kiumbe kilichojitengeneza chenyewe.
Kuzaliwa na kuzaana kwa viumbe hai nayo ni nidhamu iliyowekwa na huyo aliyekusudia nidhamu hiyo itende kazi kwa jinsi hiyo.
Pi Kuna mifano mingi hai kutoka katika vitu visivyokuwa hai kuhusu nidhamu ya utendaji kazi wao kiasi kwamba kwa akili ya kawaida tu mtu unajua kwamba vitu hivyo lazima vitakuwa vimetengenezwa na A supreme conscious being kwani haiingii akilini kudhani kwamba kuna kitu kinaweza kuibuka chenyewe na kutenda nidhamu fulani bila ya kuwepo na muanzilishi wa hiyo nidhamu.
Basi huyo Muanzilishi wa hizo nidhamu katika mwili wako ndiye Mwenyezi Mungu mtukufu.