Kitabu cha "ushahidi kuwa Mungu hayupo na uchawi haupo" kiko njiani

Ndugu zangu wana JF, mimi ni mtanzania na ninapenda kuwafahamisha kuwa ninaandika kitabu chenye kutoa ushahidi juu ya kutokuwepo mungu wala uchawi katika dunia hii.

Najua wengi wenu mkisia mada kama hii mnapuuza na kucheka. Yawezeka vicheko vinatokana na kuelewa sana juu ya chimbuko la dhana hii ya Mungu na uchawi au kutokuelewa kabisa.

Kuelewa chimbuko ni heri lakini kutokuelewa ina maana mimi na wewe tumekalilishwa mambo tusiyojua chimbuko lake.

kwa kifupi, hakuna binadamu anayeweza kufurahia kutokuwepo kwa Mungu lakini kujiaminisha juu ya uwepo wake kama ukweli ni hayupo basi kuamini yupo hakutusaidii na kule kusema hayupo kama yupo hakutusaidii.

Zipo faida za kujua ukweli na zipo hasara za kujua ukweli lakini daima tunaimba ukweli ndiyo utatuweka huru.

Mijadala kama hii ya Uwepo au Kutokuwepo kwa Mungu imekuwepo dunia tangu kale enzi za plato lakini kiukweli ni lazima tutambue kuwa ukweli juu ya jambo hili siyo rahisi kuupata kwa kufanya malumbano ya hoja au "debate".

Ukweli juu ya jambo umekaa katika ugunzi wa siri iliyojificha nyuma ya pazia la imani ni nini?

Kosa kubwa walilolifanya mababu zetu na wanaloendelea kulifanya mpaka leo katika mambo ya imani ni kuamini sauti wasizozitambua. Kwamba anatokea binadamu mmoja anasikia sauti ikimwambia mimi ni babu yako nenda kafanye moja mbili tatu, basi binadamu huyu kuamini kuwa kweli nilikuwa nikizungumza na babu yangu na kufuata maelekezo aliyopewa ndilo kosa la kwanza.

Je kama huyu tunayesema kusikia sauti ikisema mimi ni babu yako kapewa maelekezo akafuata ni kosa, je yule anayesikia sauti ikimwambia mimi ni mtakatifu fulani au ni jina fulani lolote kubwa la kiimani nakuwa sahihi?

hapa kuna mtego ambao ni kujua je ni kitu gani kiliwasiliana na hawa na kutambua kama kweli ni hicho hicho kilichojitangaza kuwa ndicho na hiyo ndiyo siri ya ugunduzi nyuma yaimani.

yeyote asiyejua siri hiyo atabaki kutumia mambo yaleyale aliyoelezwa mtu mwingine kutetea maagizo bila kuwa na ushahidi wa kujua ni kitu gani.

Kaa Tayari kujua nyuma ya mapazia ya imani kuna nini?

lakini shaka yangu ni juu ya mitizamo ya jamii juu ya imani kwa maana hawaruhusu mtu yeyote ku challenge imani zilizopo.

Kama Diamond alifungiwa mziki wake kwa kupokea simu kanisani basi mimi najiuliza hivi kitabu changu hiki kitaruhusiwa?

Neno moja niwakumbushe watanzania ni kuwa zamani zilikuwepo imani za jadi, mababu zetu walitetea na kuzilinda imani hizo kuliko sisi tunavyofanya leo lakini leo hii imani hizo tunaziona za kipuuzi na kuziita za kishetani. Hii inatufundisha kuwa upo uwezekano wa imani tulizo nazo leo na kuziona za maana huko mbeleni kuonekana za kipuuzi hivyo tumsimpuuze yeyote mwenye kutaka kusema jambo juu ya imani zetu.
Kaburi lako ulikwisha liandaa?
 
wapi alisema yeye supreme conciuos being anaitwa mwenyezi Mungu
Mimi nadhani hujatumia akili yako vyema kutafuta je Mungu yupo au hayupo??!!.

Matokeo ya mambo au vitu kuwepo kwavyo na kutenda nidhamu ni ishara ya kuwepo kwa A Supreme conscious being, hii ni upembuzi wa akili ya kawaida tu bila kutumia vitabu au imani za kidini.

Hebu leo chunguza Kompyuta au programmed Robot, Vifaa hivyo vinafanya kazi kwa nidhamu iliyokusudiwa, nidhamu hiyo kaitengeneza mtu/Engineer aliyesanifu vyombo hivyo, katika utendaji kazi wa vifaa hivyo haiwezekani leo mtu azuke tu na adai kwamba kompyuta au Robot kwa utendaji kazi wake zimezuka zenyewe au zimejiunda zenyewe!!!.

Chukua mfano huo huo wa utendaji kazi wa Kompyuta na Robot na geuza huo mfano kwa ajili yako wewe mwenyewe na Mwili wako, Katika mwili wako kuna jinsia, je hiyo jinsia uliiomba wewe, yaani uliomba uzaliwe na jinsia hiyo??, au wazazi wako walitaka wewe uwe na jinsia hiyo??-- je ni nani alipanga uwe na jinsia hiyo??!!, Je, ni nani alipanga wazazi wako wawe ni hao ulionao??!!, kabila lako, race yako nk, ni nani alipanga??!!, katika mwili wako kuna mifumo ifuatayo 1-- mfumo wa upumuaji, 2-- mfumo wa umeng'enyaji, 3-- mfumo wa damu, 4--- mfumo wa fahamu, 5--mfumo kusikia, 6--- mfumo wa uzazi nk, mifumo yote hii inafanya kazi katika nidhamu kusudiwa, je ni nani aliyeweka hii nidhamu kusudiwa katika huo mwili wako na ili iweje??!! au hiyo mifumo ulijiwekea wewe mwenyewe na ukaipatia hizo nidhamu za utendaji kazi??!!--- kama Kompyuta, Robot na Magari na mitambo mbalimbali zimeundwa na Wataalamu na zina mifumo inayofanya kazi katika nidhamu kusudiwa sasa iweje upinge kwamba wewe hujaundwa na ndio maana mwilini mwako kuna mifumo inayofanya kazi kwa nidhamu tena nidhamu kusudiwa na huyo aliyekuunda??!!--- sio katika mwili wako tu bali hata katika viumbe hai wengine unaweza kujifunza kwani na wao wanavyo vitu ambavyokwavyo mtu anaweza kujifunza kwamba na wao wametengenezwa katika nidhamu ili kukidhi haja kusudiwa, haja iliyowekwa na mtengenezaji wao kwani hakuna kiumbe kilichojitengeneza chenyewe.

Kuzaliwa na kuzaana kwa viumbe hai nayo ni nidhamu iliyowekwa na huyo aliyekusudia nidhamu hiyo itende kazi kwa jinsi hiyo.

Pi Kuna mifano mingi hai kutoka katika vitu visivyokuwa hai kuhusu nidhamu ya utendaji kazi wao kiasi kwamba kwa akili ya kawaida tu mtu unajua kwamba vitu hivyo lazima vitakuwa vimetengenezwa na A supreme conscious being kwani haiingii akilini kudhani kwamba kuna kitu kinaweza kuibuka chenyewe na kutenda nidhamu fulani bila ya kuwepo na muanzilishi wa hiyo nidhamu.

Basi huyo Muanzilishi wa hizo nidhamu katika mwili wako ndiye Mwenyezi Mungu mtukufu.
 
Logic ndio yakufuatwa kinyume cha logic ni illogic, je tufuate illogic??!!.

Logic ni kwamba hakuna kitu chenye kutenda kinidhamu na kikose muumbaji au mtengenezaji wake aliyekiwekea hiyo nidhamu ili kikidhi haja kusudiwa.---- hiyo ndio point ya kutafakari.
kwahiyo unataka kusema hata hiyo supreme conciuos being kwa kuwa ina nidhamu mana ke ina mtengenezaji wake?
 
w
Siku zote sifa ya moto ni kuunguza na kamwe huwezi kupanua fikra zako kwa kusema kwamba moto siku moja utaacha kuunguza na ndivyo hivyo kwamba kitu chochote kinachotenda ndani ya realm of disciples hicho ni lazima kiwe kimetengenezwa na A conscious disciplined being and not the otherwise, kwa upande wa yule aliyetuumba/aliyetutengeneza sisi binadamu (the most complicated disciplined machine) nk, ndiye huyo aitwaye Mungu, hivyo Mungu yupo, na lazima awe Supreme.
api alisema yeye aitwe au anaitwa mungu
 
Kitabu chako ni objective au subjective?
 
Ndugu zangu wana JF, mimi ni mtanzania na ninapenda kuwafahamisha kuwa ninaandika kitabu chenye kutoa ushahidi juu ya kutokuwepo mungu wala uchawi katika dunia hii.

Najua wengi wenu mkisia mada kama hii mnapuuza na kucheka. Yawezeka vicheko vinatokana na kuelewa sana juu ya chimbuko la dhana hii ya Mungu na uchawi au kutokuelewa kabisa.

Kuelewa chimbuko ni heri lakini kutokuelewa ina maana mimi na wewe tumekalilishwa mambo tusiyojua chimbuko lake.

kwa kifupi, hakuna binadamu anayeweza kufurahia kutokuwepo kwa Mungu lakini kujiaminisha juu ya uwepo wake kama ukweli ni hayupo basi kuamini yupo hakutusaidii na kule kusema hayupo kama yupo hakutusaidii.

Zipo faida za kujua ukweli na zipo hasara za kujua ukweli lakini daima tunaimba ukweli ndiyo utatuweka huru.

Mijadala kama hii ya Uwepo au Kutokuwepo kwa Mungu imekuwepo dunia tangu kale enzi za plato lakini kiukweli ni lazima tutambue kuwa ukweli juu ya jambo hili siyo rahisi kuupata kwa kufanya malumbano ya hoja au "debate".

Ukweli juu ya jambo umekaa katika ugunzi wa siri iliyojificha nyuma ya pazia la imani ni nini?

Kosa kubwa walilolifanya mababu zetu na wanaloendelea kulifanya mpaka leo katika mambo ya imani ni kuamini sauti wasizozitambua. Kwamba anatokea binadamu mmoja anasikia sauti ikimwambia mimi ni babu yako nenda kafanye moja mbili tatu, basi binadamu huyu kuamini kuwa kweli nilikuwa nikizungumza na babu yangu na kufuata maelekezo aliyopewa ndilo kosa la kwanza.

Je kama huyu tunayesema kusikia sauti ikisema mimi ni babu yako kapewa maelekezo akafuata ni kosa, je yule anayesikia sauti ikimwambia mimi ni mtakatifu fulani au ni jina fulani lolote kubwa la kiimani nakuwa sahihi?

hapa kuna mtego ambao ni kujua je ni kitu gani kiliwasiliana na hawa na kutambua kama kweli ni hicho hicho kilichojitangaza kuwa ndicho na hiyo ndiyo siri ya ugunduzi nyuma yaimani.

yeyote asiyejua siri hiyo atabaki kutumia mambo yaleyale aliyoelezwa mtu mwingine kutetea maagizo bila kuwa na ushahidi wa kujua ni kitu gani.

Kaa Tayari kujua nyuma ya mapazia ya imani kuna nini?

lakini shaka yangu ni juu ya mitizamo ya jamii juu ya imani kwa maana hawaruhusu mtu yeyote ku challenge imani zilizopo.

Kama Diamond alifungiwa mziki wake kwa kupokea simu kanisani basi mimi najiuliza hivi kitabu changu hiki kitaruhusiwa?

Neno moja niwakumbushe watanzania ni kuwa zamani zilikuwepo imani za jadi, mababu zetu walitetea na kuzilinda imani hizo kuliko sisi tunavyofanya leo lakini leo hii imani hizo tunaziona za kipuuzi na kuziita za kishetani. Hii inatufundisha kuwa upo uwezekano wa imani tulizo nazo leo na kuziona za maana huko mbeleni kuonekana za kipuuzi hivyo tumsimpuuze yeyote mwenye kutaka kusema jambo juu ya imani zetu.
Stop using expired weeds bro🤪🤪🤪
 
bahati mbaya sana mimi sijasoma lugha kama somo mama hivyo tafsiri yangu ya "kuelimika" haiko katika utaalamu wa lugha bali uwezo wa kuchakata mambo mbalimbali yaliyoko katika jamii na kuyapa mantiki.

Utaalamu wa lugha nauchukilia kama "background knowledge" ambayo haina nguvu sana katika hoja
Unaandika na kuongea halafu unasema hujasoma hivyo una uhuru wa kuropoka na kujiandikia utakavyo bila kufuata kanuni ya uandishi?

Una tatizo bwashee, kumbuka wasomaji na wasikilizaji ni watu wenye uelewa mkubwa kuliko wewe, so ukishindwa kufuata kanuni za kisomi nenda karopoke chumbani kwa kwako kwa ajili yako peke yako na ujiaandikie mwenyewe.
 
Katika tumbo la mama kulikuwa na watoto wawili. Mmoja akamuuliza mwenzake: “Je, unaamini maisha baada ya kujifungua?” Yule mwingine akajibu, “Kwa nini, bila shaka. Lazima kuwe na kitu baada ya kujifungua. Labda tuko hapa kujitayarisha kwa kile tutakachokuwa baadaye.” "Upuuzi," wa kwanza alisema. "Hakuna maisha baada ya kujifungua. Je, hayo yangekuwa maisha ya aina gani?” Wa pili akasema, "Sijui, lakini kutakuwa na mwanga zaidi kuliko hapa. Labda tutatembea kwa miguu yetu na kula kutoka kwa midomo yetu. Labda tutakuwa na hisia zingine ambazo hatuwezi kuelewa sasa. Wa kwanza akajibu, “Huo ni upuuzi. Kutembea haiwezekani. Na kula kwa midomo yetu? Kichekesho! Kamba ya umbilical hutoa lishe na kila kitu tunachohitaji. Lakini kamba ya umbilical (kondo la nyuma) ni fupi sana.

Maisha baada ya kujifungua yanapaswa kutengwa kimantiki.” Wa pili alisisitiza, "Nadhani kuna kitu na labda ni tofauti na ilivyo hapa. Labda hatutahitaji kamba hii ya mwili tena." Wa kwanza akajibu, “Upuuzi. Na zaidi ya hayo, ikiwa kuna uhai, basi kwa nini hakuna mtu aliyewahi kurudi kutoka huko? Kujifungua ni mwisho wa maisha, na katika baada ya kuzaa hakuna ila giza na ukimya na usahaulifu. Haitupeleki popote.” “Sawa, sijui,” akasema wa pili, “lakini hakika tutakutana na Mama naye atatutunza.”

Wa kwanza akajibu “Mama? Unamwamini Mama kweli? Hiyo inachekesha. Kama mama yupo, yuko wapi sasa hivi?" Wa pili akasema, “Anatuzunguka pande zote. Tumezungukwa naye. Sisi ni wake. Ni ndani Yake tunaishi. Bila Yeye, ulimwengu huu haungekuwepo na tusingekuwepo." Alisema wa kwanza: "Kweli, simuoni, kwa hivyo ni sawa kwamba Yeye hayupo." Ambayo wa pili alijibu, "Wakati mwingine, unapokuwa kimya na ukizingatia na kusikiliza, unaweza kuona uwepo Wake, na unaweza kusikia sauti Yake ya upendo, ikiita kutoka juu." Labda hii ilikuwa moja ya maelezo bora ya dhana ya MUNGU.

View attachment 2240141
komenti bora kabisa,uzi ufungwe
 
Mimi nadhani hujatumia akili yako vyema kutafuta je Mungu yupo au hayupo??!!.

Matokeo ya mambo au vitu kuwepo kwavyo na kutenda nidhamu ni ishara ya kuwepo kwa A Supreme conscious being, hii ni upembuzi wa akili ya kawaida tu bila kutumia vitabu au imani za kidini.

Hebu leo chunguza Kompyuta au programmed Robot, Vifaa hivyo vinafanya kazi kwa nidhamu iliyokusudiwa, nidhamu hiyo kaitengeneza mtu/Engineer aliyesanifu vyombo hivyo, katika utendaji kazi wa vifaa hivyo haiwezekani leo mtu azuke tu na adai kwamba kompyuta au Robot kwa utendaji kazi wake zimezuka zenyewe au zimejiunda zenyewe!!!.

Chukua mfano huo huo wa utendaji kazi wa Kompyuta na Robot na geuza huo mfano kwa ajili yako wewe mwenyewe na Mwili wako, Katika mwili wako kuna jinsia, je hiyo jinsia uliiomba wewe, yaani uliomba uzaliwe na jinsia hiyo??, au wazazi wako walitaka wewe uwe na jinsia hiyo??-- je ni nani alipanga uwe na jinsia hiyo??!!, Je, ni nani alipanga wazazi wako wawe ni hao ulionao??!!, kabila lako, race yako nk, ni nani alipanga??!!, katika mwili wako kuna mifumo ifuatayo 1-- mfumo wa upumuaji, 2-- mfumo wa umeng'enyaji, 3-- mfumo wa damu, 4--- mfumo wa fahamu, 5--mfumo kusikia, 6--- mfumo wa uzazi nk, mifumo yote hii inafanya kazi katika nidhamu kusudiwa, je ni nani aliyeweka hii nidhamu kusudiwa katika huo mwili wako na ili iweje??!! au hiyo mifumo ulijiwekea wewe mwenyewe na ukaipatia hizo nidhamu za utendaji kazi??!!--- kama Kompyuta, Robot na Magari na mitambo mbalimbali zimeundwa na Wataalamu na zina mifumo inayofanya kazi katika nidhamu kusudiwa sasa iweje upinge kwamba wewe hujaundwa na ndio maana mwilini mwako kuna mifumo inayofanya kazi kwa nidhamu tena nidhamu kusudiwa na huyo aliyekuunda??!!--- sio katika mwili wako tu bali hata katika viumbe hai wengine unaweza kujifunza kwani na wao wanavyo vitu ambavyokwavyo mtu anaweza kujifunza kwamba na wao wametengenezwa katika nidhamu ili kukidhi haja kusudiwa, haja iliyowekwa na mtengenezaji wao kwani hakuna kiumbe kilichojitengeneza chenyewe.

Kuzaliwa na kuzaana kwa viumbe hai nayo ni nidhamu iliyowekwa na huyo aliyekusudia nidhamu hiyo itende kazi kwa jinsi hiyo.

Pi Kuna mifano mingi hai kutoka katika vitu visivyokuwa hai kuhusu nidhamu ya utendaji kazi wao kiasi kwamba kwa akili ya kawaida tu mtu unajua kwamba vitu hivyo lazima vitakuwa vimetengenezwa na A supreme conscious being kwani haiingii akilini kudhani kwamba kuna kitu kinaweza kuibuka chenyewe na kutenda nidhamu fulani bila ya kuwepo na muanzilishi wa hiyo nidhamu.

Basi huyo Muanzilishi wa hizo nidhamu katika mwili wako ndiye Mwenyezi Mungu mtukufu.
We ndio unamuongezea nguvu kwenye hoja ya mtoa mada kuonesha jinsi gani Mungu hawezi kuwepo
 
Kitabu chako ni objective au subjective?
Kitabu hiki ni moja ya vitabu bora kuwahi kutokea katika kuchalenji imani

Naweza kusema ni objective maana kinatoa facts na siyo kutumia hisia.

Zimekuwepo arguments nyingi za uwepo au kutokuwepo kwa hicho kitu kinachoitwa ulimwengu wa roho na hii ni completely new new materials ambazo hazikuwepo.

Tegemea kushikwa na butwaa
 
We ndio unamuongezea nguvu kwenye hoja ya mtoa mada kuonesha jinsi gani Mungu hawezi kuwepo

Mungu yupo na kuna sababu nyingi za kutibitisha uwepo wake na moja ni hiyo.
 
Labda hizo zingine ambazo hujaziweka pengine zinaweza zikawa na nafuu ila sio kwa hoja hiyo uliyoiweka
 
kuna langua

je kama kiarabu hawana herufi ndogo wala kubwa manake hayo masharti hayawahusu??kwenye matamshi M na m kuna tufauti?? nani aliyesema M ni herufi kubwa kuliko m au ni kikundi ch watu tu pengine walikua wamelewa? leo wakiamua M iwe ndogo na m indio iwe kubwa masharti yatabadilika na huyo Mungu atachukia??
Hapa hatuandiki kiarabu bali Kiswahili
 
bahati mbaya sana mimi sijasoma lugha kama somo mama hivyo tafsiri yangu ya "kuelimika" haiko katika utaalamu wa lugha bali uwezo wa kuchakata mambo mbalimbali yaliyoko katika jamii na kuyapa mantiki.

Utaalamu wa lugha nauchukilia kama "background knowledge" ambayo haina nguvu sana katika hoja
OK sawa basi kwa mtazamo huo hatuwezi kuwa na mjadala kati yetu
 
Unaandika na kuongea halafu unasema hujasoma hivyo una uhuru wa kuropoka na kujiandikia utakavyo bila kufuata kanuni ya uandishi?

Una tatizo bwashee, kumbuka wasomaji na wasikilizaji ni watu wenye uelewa mkubwa kuliko wewe, so ukishindwa kufuata kanuni za kisomi nenda karopoke chumbani kwa kwako kwa ajili yako peke yako na ujiaandikie mwenyewe.
Lakini amesema hajasomea utaalamu wa lugha, au mimi sijamuelewa?
 
OK sawa basi kwa mtazamo huo hatuwezi kuwa na mjadala kati yetu
😳😳😳 kiongozi unataka kutunyima uhondo wa 'nondo' kwasababu tu ya unayebishana nae kutokuwa mtaalamu wa lugha?!!!!! Yaani masuala sijui ya 'capital and small letters, question marks, colon, semi colon, apostrophe' n.k ndiyo yakufungishe mjadala?!!!!

Nakusihi jikite kwenye kueleweka au kutokueleweka kwake kwenye anachoongea; usitunyime uhondo sisi wengine tunaojifunza kuzungumza kimantiki!
 
[emoji15][emoji15][emoji15] kiongozi unataka kutunyima uhondo wa 'nondo' kwasababu tu ya unayebishana nae kutokuwa mtaalamu wa lugha?!!!!! Yaani masuala sijui ya 'capital and small letters, question marks, colon, semi colon, apostrophe' n.k ndiyo yakufungishe mjadala?!!!!

Nakusihi jikite kwenye kueleweka au kutokueleweka kwake kwenye anachoongea; usitunyime uhondo sisi wengine tunaojifunza kuzungumza kimantiki!
Hivyo vitu ndio vinatengeneza maana kusudiwa na ndio maana hata wewe umevitumia ..Alama moja ndogo sana inaweza kubadili kila kitu..
Angalia umuhimu wa hizo alama kwenye maandishi kwa kusoma mfano huu.. Huyu jamaa alinusurika kifo kisa tu matumizi ya alama ya mkato

Hakimu kwenye hukumu yake alihitimisha kwa kuandika
Hang him not, let him go!
Kumbe alitaka kumaanisha
Hang him, not let him go!

Tunafeli katika maisha kwa kudharau vitu vidogo vidogo kama hivi kumbe ndio vinatengeneza tafsiri kusudiwa.. Kama mtu si mtaalam wa lugha imanaanisha basi huyo hajaelimika ..
 
Back
Top Bottom