MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
- Thread starter
- #601
Mkuu idea Nzuri. Mods wanatakiwa wawe waelewa wanaweza kuachana thread yako ijitegemee na kuweka links kwenye ya related threads ndani ya thread kama further JF references.Wasalaaam ndugu zangu, natumai wote ni wazima.
Leo hii naanzisha huu uzi kwa dhumuni zuri na maalumu la kusambaza maarifa kwa wanajukwaa hili na pengine watu wengine wa nje ya jukwaa hili.
Mpango ni kurusha vitabu mbalimbali kwenye jukwaa hili ambavyo vitaweza kuwasaidia watu na kuweza kuwapanua uwezo wa kiakili endapo utakuwa umesoma vitabu vizuri na bado unavyo itakuwa ni vema ukirushe kwenye uzi huu ili watu mbalimbali wasome na waelewe.
Natumai watu wa kada mbalimbali watapita na hakuna mtu ambaye atakosa cha kujifunza hapa. Sasa vitabu vinaweza kuja kwa mfumo wa PDF, MOBI, EPUB etc. Na kama utakuwa na hard copy basi watu wanaweza kukutafuta kama tu mtakuwa mekubaliana.
Natanguliza shukrani zangu.
Mimi naanza na kitabu kizuri sana ambacho kimenisadia kwenye kukuza uwezo wa kufikiri mambo kwenye biashara. Kinaitwa "The Go Giver" nashauri mtu akipata muda akisome.
Kama kimenisaidia basi natumai hata wewe kitakusaidia.
Kwa kifupi kinaelezea jinsi gani ambavyo mtu anaweza kufanya biashara kubwa lakini bado biashara hiyo itaipa jamii inayomzunguka faida.
Tofauti na mawazo ambayo wafanya biashara wengi na wajasiriamali wanakuwa nayo kwamba biashara ni faida tu na utafanya biashara sehemu yenye faida tu.
Kinaanza na mtu moja alikuwa ni kijana mdogo anafanya kazi kwenye kampuni fulani huko MAREKANI sasa akawa anahangaika sana kupata utajiri wa haraka. Kila siku alikuwa na mipango mikubwa ya biashara lakini hafanikiwi. Siku moja akapata nafasi kukaa na tajiri mkubwa huko MAREKANI na akaambiwa sifa ya kuwa Tajiri ni lazima ujifunze kutoa kwa watu kabla ya kutanguliza faida.
Mbeleni kinaonyesha jamaa analalamika kwamba ukifanya biashara kwa huruma huwezi kutajirika hata siku. Lakini akakutana na tajiri mwingine ambaye alimueleza vilevile. Na mwishowe akaja kujua kama matajiri wakubwa wote wanakuwa na sifa zinazofanana.
Young Malcom.
CC: UncleBen , FisadiKuu , MSEZA MKULU , Consigliere
Hivi vitu useful vinatakiwa kuachwa viwe vingi mbona thread za siasa Sijui tundu lissu huwa hata kumi. Otherwise create title unique kidogo uwe kama unaadress issue mpya. Hicho kitabu nitakipitia