Kuna kitu kimoja nimekipata kutoka kwa Mzee Barwani. Nina uhakika watu wengi hawakifahamu
Neno Hizbu anasema ni Party au chama kwa kiarabu na ililitumika kwa vile hakukuwa na mbadala
Dr Salim Ahmed Salim aliwahi kunyimwa fursa ya kuwa Rais wa JMT kwa vile tu walimtuhumu kuwa ni mwanachama wa Hizbu. Hata leo hii ukisema ni Hizbu ni kama vile unazungumzia ''uhaini'', kumbe sivyo ni neno tu 'chama''
Pili, siasa za Zanzibar zinategemea upande hasa rangi na imani. Huu ni ukweli usiokubalika lakini ni ukweli uliopo.
Ni hadi pale watu watakapokubali kukabiliana na ukweli, tatizo lililopo litakuwa na suluhisho.
Ukimsoma Mohamed Said anasema Historia ya kweli ni hii ya hawa wazee.
Ukimsoma kwa undani anazungumzia Uislam zaidi ya historia, kwa maana kwamba anaiandika au kuielezea katika jicho la Uislam. Hakuna tatio kwani kila mwandishi ana jicho lake na ni ngumu kutenga interest na uandishi
Ni kwa mantiki hiyo MS na hao wazee wa 'Umma, Hizbu' etc wanasema Nyerere alipeleka majeshi kuvamia Zanzibar akimsaidia John Okello. Kutokana na kukosa sababu kuna 'aya moja' nitaionyesha ambayo mwandishi amebabaika bila kujua anaandika nini. Hii maana yake ni kuwa mwandishi wa hiyo 'article' hakuwa na information za kutosha bali alijazwa hisia , jazba na chuki na yeye kunyanyua kalamu.
Tukirudi kwa Mohamed, hili la Zanzibar analizungumzia kwa 'jicho upande''.
Akiwa London , Muscat na kwingine atakueleza Mapinduzi ya Zanzibar ni haramu.
Hapa anasimama na Waislam katika Uislam
Akirudi Tanzania ukamuuliza , je, wanaosherehekea mapinduzi kila January 12 wanafanya haramu?
Wanafanya makosa? Nakuhakikishia Mohamed Said hatakupa jibu, atazunguka zunguka na maneno ya reja reja akitoa picha na rejea zake wakati wa safari uzunguni na uarabuni akitafuna makaimati. Hatukupa jibu.
Kubabaika kwa MS kuna shadidia hoja yangu hapo mwanzo kuwa inategemea upo upande gani.
Mathalani, ukiwa mmatumbi mwenye nywele za kipili pili ukiwa mlinzi wa bawaba, mapinduzi yalikuwa halali 'mapinduzi daima'
Ukiwa mwenye nywele za katani na unasaba wa 'falme' mapinduzi yalikuwa ni ya Nyerere na haramu
MS anajikuta ' between a rock and hard place'.
Atawakataaje Waarabu Waislam bila kuukata Uislam?
Atawaangaliaje Wamatumbi anaofanana bila kuudhi Uislam!
JokaKuu Mag3 tindo