bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Sheikh kipande uuzaji wa kitabu ni shughuli ya mchapaji na kwa kuwa kwake ni biashara atakipeleka kule kwenye wanunuzi wengi.
Kitabu kikiwa Amazon kiko kwenye soko la dunia nzima.
Mwandishi anaishia kwenye uandishi.
Nitumie stamped self-addressed A4 manila envelope nitakutumia, nadhani wanauza duka moja pale Faya.I wish hiki kitabu kingekuwa kinauzwa electronic copies
Einstein,Usisahau kumuandika JOHN OKELO kwamba ndio alimng'oa Sultan hapo Zenji na sio KARUME
Mkuu achana na majina.mengi JOHN OKELO ndio mwanamapinduzi halisi na ndiye aliemfukuza sultani.ila.alipinduliwa na Nyerere alipokuja bara. Soon ntakupa kisa chake kilichopinduliwaEinstein,
Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964 ina mengi inaelekea huyafahamu.
John Okello ni sehemu ndogo sana ya kisa hicho.
Kama ni kutaja majina kuna majina makubwa hujayasikia.
Ushasikia Kipumbwi na Sakura Tanga?
Hapo ndipo ilipokuwa kambi ya mafunzo ya Wamakonde wakata mkonge kutoka shamba la Sakura waliovushwa kwenda Zanzibar kusaidia mapinduzi.
Wahusika wakuu wa kambi hii walikuwa watendaji wa serikali ya Tanganyika, Regional na Area Commissioner wa Tanga - Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe.
Wasimamizi wa kambi - Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa.
Lakini mipango kama hii katika ardhi ya Tanganyika inahitaji mkono wa serikali na wasimamizi kutoka sehemu zote mbili - Zanzibar na Tanganyika.
Alikuwapo Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.
Kulikuwa na Wayahudi na Waalgeria.
Okello alisikika siku ya pili kufuatia mapinduzi usiku.
Soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni," utaujua ukweli kuwa Okello hakuwa chochote katika mipango ya mapinduzi ila "mascot," iliyonogesha mkasa mzima.
Nitumie stamped self-addressed A4 manila envelope nitakutumia, nadhani wanauza duka moja pale Faya.
ZNP pia alikuwepo Salim A Salim..
Ni sawa??
Einstein,Mkuu achana na majina.mengi JOHN OKELO ndio mwanamapinduzi halisi na ndiye aliemfukuza sultani.ila.alipinduliwa na Nyerere alipokuja bara. Soon ntakupa kisa chake kilichopinduliwa
Kuna kitu kimoja nimekipata kutoka kwa Mzee Barwani. Nina uhakika watu wengi hawakifahamu
Neno Hizbu anasema ni Party au chama kwa kiarabu na ililitumika kwa vile hakukuwa na mbadala
Dr Salim Ahmed Salim aliwahi kunyimwa fursa ya kuwa Rais wa JMT kwa vile tu walimtuhumu kuwa ni mwanachama wa Hizbu. Hata leo hii ukisema ni Hizbu ni kama vile unazungumzia ''uhaini'', kumbe sivyo ni neno tu 'chama''
Pili, siasa za Zanzibar zinategemea upande hasa rangi na imani. Huu ni ukweli usiokubalika lakini ni ukweli uliopo.
Ni hadi pale watu watakapokubali kukabiliana na ukweli, tatizo lililopo litakuwa na suluhisho.
Ukimsoma Mohamed Said anasema Historia ya kweli ni hii ya hawa wazee.
Ukimsoma kwa undani anazungumzia Uislam zaidi ya historia, kwa maana kwamba anaiandika au kuielezea katika jicho la Uislam. Hakuna tatio kwani kila mwandishi ana jicho lake na ni ngumu kutenga interest na uandishi
Ni kwa mantiki hiyo MS na hao wazee wa 'Umma, Hizbu' etc wanasema Nyerere alipeleka majeshi kuvamia Zanzibar akimsaidia John Okello. Kutokana na kukosa sababu kuna 'aya moja' nitaionyesha ambayo mwandishi amebabaika bila kujua anaandika nini. Hii maana yake ni kuwa mwandishi wa hiyo 'article' hakuwa na information za kutosha bali alijazwa hisia , jazba na chuki na yeye kunyanyua kalamu.
Tukirudi kwa Mohamed, hili la Zanzibar analizungumzia kwa 'jicho upande''.
Akiwa London , Muscat na kwingine atakueleza Mapinduzi ya Zanzibar ni haramu.
Hapa anasimama na Waislam katika Uislam
Akirudi Tanzania ukamuuliza , je, wanaosherehekea mapinduzi kila January 12 wanafanya haramu?
Wanafanya makosa? Nakuhakikishia Mohamed Said hatakupa jibu, atazunguka zunguka na maneno ya reja reja akitoa picha na rejea zake wakati wa safari uzunguni na uarabuni akitafuna makaimati. Hatukupa jibu.
Kubabaika kwa MS kuna shadidia hoja yangu hapo mwanzo kuwa inategemea upo upande gani.
Mathalani, ukiwa mmatumbi mwenye nywele za kipili pili ukiwa mlinzi wa bawaba, mapinduzi yalikuwa halali 'mapinduzi daima'
Ukiwa mwenye nywele za katani na unasaba wa 'falme' mapinduzi yalikuwa ni ya Nyerere na haramu
MS anajikuta ' between a rock and hard place'.
Atawakataaje Waarabu Waislam bila kuukata Uislam?
Atawaangaliaje Wamatumbi anaofanana bila kuudhi Uislam!
JokaKuu Mag3 tindo
That is possible wakiamua. Mbona kila kitabu kinapatikana electronicallyI wish hiki kitabu kingekuwa kinauzwa electronic copies
..nadhani ndugu zetu walikuwa na tatizo la Uafrika vs Uarabu.
..tatizo hilo pia likahamia ktk vyama vyao vya siasa vilivyokuwepo kabla ya Mapinduzi.
..pia chaguzi zao wakati wote zimekuwa za ushindani mkubwa na washindi wamekuwa wakipata ushindi "mwembaamba."
..Mapinduzi pamoja na mambo mengine yalichochewa na figisu na rafu walizokuwa wakifanyiana Waznz wakati wa uchaguzi.
..Malengo ya Mapinduzi yanaweza kuwa mazuri kabisa, ila tatizo ni mauaji na ukatili uliofanyika wakati na baada ya Mapinduzi.
..mimi naamini Mohamed Said ameungana na upande ambao uliathiriwa vibaya na mambo ya kikatili yaliyofanywa na wanamapinduzi.
..vilevile naamini figisu zinazoendelea ktk kila uchaguzi wa Znz zinatokana na nia ya wahusika kuficha na kulinda maovu yaliyofanywa baada ya Mapinduzi.
NB:
..Sultani wa Zanzibar alikuwa ni ceremonial figure kwa muda mrefu tangu wakati wa Muingereza. Wanaodai kwamba Mapinduzi yalikuwa ni kumpindua Sultani naamini hawako sahihi.
Naona kama sasa wameamua kuzika yale yaliyopita. Wakiamua hivyo na kuanza kuendeleza pemba kama Unguja, Zanzibar itakuwa nchi ya neema kweli kweli. Mtaji wa kuzima kila linaloendelea wanaoutoa ni wao wenyewe wazenj, maana bado wana roho ya kulipizana visasi
Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar mnaibumbabumba kumuondoa Okelo ila inafahamika kuwa ndio.aliongoza mapinduzi na kujitangaza rais wa Zanzibar baadae akaja bara, mwalimu Nyerere akafanya mpango, wa kumpindua, wakati anarudi zenji, kwa ndege, wakawashusa delegates wake na yeye akabaki kwenye ndege akapelekwa Kenya na hakurusiwa kurudi tena Zenji.Einstein,
Vipi niachane na haya majina ilahali baadhi yao nimewaona kwa macho yangu wakifanyiwa mahojiano na Dr. Harith Ghassany mimi nikiwapo kama Mtafiti Msaidizi wake wakati anatafiti historia hii?
Nilikuwa msaidizi wake kuanzia 2003 had 2010 kitabu kilipochapwa Marekani.
Ikiwa una taarifa zinazotofautiana na historia katika kitabu cha Dr. Ghassany nitafurahi kusoma.
Angalia picha hiyo hapo chini: kushoto ni Mohamed Omari Mkwawa (Tindo) jina alilopewa na Mzee Karume wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar, Maulidi Shein na mimi.
Dr. Ghassany ndiye aliyepiga picha hii.
Haya yalikuwa mahojinao ya mwisho Dar es Salaam kabla ya kukamilisha utafiti.
View attachment 1691694
Einstein,Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar mnaibumbabumba kumuondoa Okelo ila inafahamika kuwa ndio.aliongoza mapinduzi na kujitangaza rais wa Zanzibar baadae akaja bara, mwalimu Nyerere akafanya mpango, wa kumpindua, wakati anarudi zenji, kwa ndege, wakawashusa delegates wake na yeye akabaki kwenye ndege akapelekwa Kenya na hakurusiwa kurudi tena Zenji.
Ziko articles zinazozungumzia hii
JK,..nadhani ndugu zetu walikuwa na tatizo la Uafrika vs Uarabu.
..tatizo hilo pia likahamia ktk vyama vyao vya siasa vilivyokuwepo kabla ya Mapinduzi.
..pia chaguzi zao wakati wote zimekuwa za ushindani mkubwa na washindi wamekuwa wakipata ushindi "mwembaamba."
..Mapinduzi pamoja na mambo mengine yalichochewa na figisu na rafu walizokuwa wakifanyiana Waznz wakati wa uchaguzi.
..Malengo ya Mapinduzi yanaweza kuwa mazuri kabisa, ila tatizo ni mauaji na ukatili uliofanyika wakati na baada ya Mapinduzi.
..mimi naamini Mohamed Said ameungana na upande ambao uliathiriwa vibaya na mambo ya kikatili yaliyofanywa na wanamapinduzi.
..vilevile naamini figisu zinazoendelea ktk kila uchaguzi wa Znz zinatokana na nia ya wahusika kuficha na kulinda maovu yaliyofanywa baada ya Mapinduzi.
NB:
..Sultani wa Zanzibar alikuwa ni ceremonial figure kwa muda mrefu tangu wakati wa Muingereza. Wanaodai kwamba Mapinduzi yalikuwa ni kumpindua Sultani naamini hawako sahihi.