Kitabu; Usimamizi wa fedha binafsi; mwongozo wa kupata, kutunza na kuzalisha fedha ili kuwa huru

Kitabu; Usimamizi wa fedha binafsi; mwongozo wa kupata, kutunza na kuzalisha fedha ili kuwa huru

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Rafiki yangu mpendwa,

Umewahi kujiuliza kwa nini watu wawili, wanaoweza kuwa wanafanya kazi au biashara zinazofanana na kuingiza kipato sawa, mmoja anaweza kuwa vizuri kifedha na mwingine vibaya?

Au umewahi kujiuliza kwa nini watu ambao kazi zao za kila siku wanahusika na simamizi wa fedha, mfano watu wa benki na wahasibu, lakini inapokuja kwenye fedha zao binafsi wanakuwa hawana usimamizi mzuri?

Rafiki, tofauti ambazo watu wanazo kwenye fedha zinaanzia kwenye aina ya ujuzi ambao watu wanao kwenye fedha. Wanaofanikiwa kifedha wana ujuzi mwingi wa fedha kuliko ambao hawajafanikiwa.

Inapokuja kwenye fedha, kuna ujuzi wa aina tatu ambao mtu anapaswa kuwa nao ili aweze kuwa na uhuru na utulivu.

Ujuzi wa kwanza ni jinsi ya kupata fedha. Hapa lazima mtu ajue namna bora ya kuweza kuingiza kipato ambapo msingi mkuu ni kutoa thamani kubwa.

Ujuzi wa pili ni jinsi ya kutunza fedha. Hapa lazima mtu aweze kuwa na mgawanyo sahihi wa fedha zake na kutokutumia zote mpaka zikaisha.

Ujuzi wa tatu ni jinsi ya kuzalisha fedha. Hapa lazima mtu aweze kutumia fedha kuzalisha fedha zaidi, ujuzi huu ndiyo unamfikisha mtu kwenye uhuru.

Kwa bahati mbaya sana, tangu tukiwa shuleni mpaka tunaingia kwenye kazi na biashara, hatujawahi kufundishwa kwa kina hizo ujuzi zote. Na hilo ndiyo limekuwa chanzo cha changamoto nyingi tulizonazo kifedha.

Shuleni tulifundishwa mambo mengi sana, vita mbalimbali zilizotokea miaka mingi, miamba iliyo nchi za mbali, wadudu na mimea mbalimbali. Lakini kile ambacho tunahangaika nacho kila siku, yaani fedha, hatukupata nafasi ya kufundishwa kwa kina.

Rafiki, nina habari njema sana kwako kuhusu sehemu unayoweza kupata elimu sahihi ya kifedha inayokujengea ujuzi wa kupata, kutunza na kuzalisha fedha. Sehemu hiyo ni kitabu kipya kinachoitwa USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI, ambacho ni mwongozo sahihi kwa kila anayetaka kujiimarisha kwenye eneo la fedha.

USIMAMIZI-FEDHA-684x1024.jpg

NGUZO SABA ZA USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI.

Rafiki, kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI kinaeleza NGUZO SABA ambazo ndiyo zinapelekea mtu kuwa na usimamizi imara wa fedha zake binafsi na kuweza kuwa huru vile anavyotaka.

Nguzo hizo saba ni za msingi na rahisi kwa kila mtu kufanyia kazi ili kuweza kujiimarisha kwenye eneo la fedha ili kuwa huru. Nguzo hizo ni kama ifuatavyo;

Nguzo Ya Kwanza ni Kipato
Kuingiza kipato ndiyo nguzo ya kwanza na muhimu zaidi kwenye usimamizi wa fedha binafsi. Bila nguzo hii nyingine haziwezi kuwa na nguvu.

Kwenye kuingiza kipato, kuna njia kuu tatu ambazo mtu anaweza kutumia;

1. Kuajiriwa, ambapo mtu unauza muda, ujuzi na uzoefu wako kwa watu wengine na kulipwa mshahara.

2. Kujiajiri, ambapo mtu anafanya mambo yake peke yake.

3. Kufanya biashara, ambapo mtu anatumia rasilimali za wengine kuingiza kipato kikubwa.

Kwenye nguzo ya kipato, msingi mkuu ni THAMANI. Unalipwa kulingana na thamani unayotoa kwa wengine. Ukiweza kutoa thamani kubwa zaidi, unalipwa zaidi.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kuingiza kipato kikubwa, cha uhakika na chenye ukuaji endelevu. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Pili ni Akiba
Akiba ni sehemu ya kipato unayoitenga kwa sababu maalumu. Huwa kuna akiba za aina mbili ambazo kila mtu anapaswa kuziweka.

1. Akiba ya dharura, hii ni kwa ajili ya mambo yasiyotegemewa kutokea, ili yasikuvuruge.

2. Akiba ya malengo, hii ni kwa ajili ya kutekeleza malengo ambayo mtu anayo kwenye maisha, kama ujenzi, manunuzi ya mali binafsi na shughuli fulani za msingi.

Msingi mkuu wa akiba ni TABIA. Kuweka akiba hakutegemei kipato alichonacho mtu, bali tabia aliyonayo. Ukiwa na tabia ya kuweka akiba, utaweka hata kama kipato ni kidogo. Hivyo unapaswa kujijengea tabia ya kuweka akiba bila kujali kipato unachokuwa nacho.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kuweka akiba kwenye kipato chochote ulichonacho na kujizuia usitumie akiba tofauti na kusudi. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Tatu Ni Matumizi
Matumizi ni maeneo ambayo fedha zetu zinakwenda ili kukamilisha maisha yetu. Hapa ndipo sehemu kubwa ya kipato huwa inaenda. Huwa kuna aina tatu za matumizi ambazo mtu unapaswa kuzijua ili kusimamia vizuri fedha zako;

1. Matumizi ambayo ni mahitaji (needs), haya ni lazima uyakamilishe ili maisha yaweze kwenda.

2. Matumizi ambayo ni matakwa (wants), haya siyo ya lazima, lakini yanafanya maisha kuwa rahisi zaidi.

3. Matumizi ambayo ni anasa (luxuries), haya ni kwa ajili ya burudani na kujisikia vizuri.

Msingi mkuu kwenye matumizi ni kuyadhibiti yasizidi kipato. Na zaidi, akiba inapaswa kuanza kabla ya matumizi. Kwa wengi wanapoingiza kipato wanatumia kwanza na kikibaki ndiyo wanaweka akiba, lakini tunajua kwamba kipato hakijawahi kutosheleza matumizi.

Kanuni sahihi kwenye kipato, akiba na matumizi ni; KIPATO – AKIBA = MATUMIZI. Yaani unapoingiza kipato, unapaswa kutenga akiba kwanza kabla ya kufanya matumizi.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kudhibiti matumizi yako yasizidi kipato. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Nne ni Madeni
Madeni yamekuwa yanatokana na mtu kutumia fedha ambazo hana, hivyo kupaswa kuzilipa kwa gharama za ziada. Madeni huwa yapo ya aina mbili;

1. Madeni mabaya, ambapo unalipa kwa gharama kubwa wakati hayajaongeza kipato chako.

2. Madeni mazuri, ambapo unalipa kwa gharama, lakini yanakuwa yamekuingizia faida kubwa kuliko kile unacholipa.

Msingi mkuu kwenye madeni ni kuondoka kwenye madeni mabaya na kubaki kwenye madeni mazuri. Ipo mikakati sahihi ya kukusaidia kwenye hilo.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye madeni mabaya na kuwa na madeni mazuri yatakayokunufaisha. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Tano Ni Matoleo
Japokuwa unahangaika na fedha binafsi, lakini manufaa ya fedha zako siyo kwa ajili yako tu, bali ni kwa ajili ya watu wengine. Unawajibika kutoa fedha zako kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine. Zipo njia tatu za kuwa na matoleo ya fedha zako;

1. Sadaka, haya ni matoleo ya kiimani, kulingana na imani ya mtu kuna sadaka mbalimbali za kutoa, kwa mfano fungu la kumi.

2. Misaada kwa wenye uhitaji, hapa mtu anakuwa na mchango kwa wale wenye uhitaji.

3. Kodi, hapa mtu unachangia maendeleo ya nchi kupitia ulipaji wa kodi mbalimbali.

Msingi mkuu wa utoaji ni kupeleka sehemu ya fedha zako kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya utoaji utakavyokufaisha zaidi wewe unayetoa kuliko hata wanaopokea. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Sita Ni Uwekezaji
Uwekezaji ni kuifanya fedha ikufanyie kazi na kukuletea faida, bila wewe kuhusika moja kwa moja. Hii ni nguzo muhimu kwa mtu kuelekea kwenye uhuru, ambapo anaweza kuzalisha kipato bila kulazimika kuwepo moja kwa moja. Uwekezaji upo wa aina nyingi, lakini aina tatu ni za msingi mtu kufanya;

1. Uwekezaji kwenye masoko ya mitaji. Hapa inahusisha mifuko ya pamoja ya uwekezaji, hatifungani na soko la hisa. Ni uwekezaji rahisi ambao kila mtu anaweza na anapaswa kufanya.

2. Uwekezaji kwenye vito vya thamani. Hivi ni vitu ambavyo thamani yake inakua muda unavyokwenda, mfano madini, sarafu maalumu, michoro n.k. Ni maeneo ya kuweka fedha isipoteze thamani.

3. Uwekezaji kwenye ardhi na mali. Hapa ardhi na mali zinazotokana na uendelezaji wa ardhi zinaongeza thamani na kuweza kuingiza kipato.

Msingi mkuu wa uwekezaji ni kuanza mapema na kufanya kidogo kidogo kwa msimamo bila kuacha.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kufanya uwekezaji utakaokuwezesha kuingiza kipato bila kufanya kazi moja kwa moja. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Nguzo Ya Saba Ni Ulinzi
Unaweza kupambana sana kujijenga kifedha, halafu likatokea tukio ambalo linaangusha kila kitu ulichojenga. Ni muhimu kuwa na ulinzi ambao utakulinda kifedha, ili jambo lolote linapotokea lisikuangushe. Kwenye ulinzi wa kifedha, bima inahitajika. Kuna bima za aina tatu ambazo mtu unapaswa kuwa nazo ili kujikinga na majanga mbalimbali;

1. Bima ya afya, ambayo itakukinga na gharama kubwa za afya zinazoweza kukuteteresha.

2. Bima ya mali, ambayo itakukinga na upotevu wa mali ulizonazo pale yanapotokea majanga mbalimbali.

3. Bima ya maisha, ambayo itakinga kipato chako na kusaidia wategemezi wako pale unaposhindwa kufanya hivyo au unapofariki.

Msingi mkuu wa ulinzi ni kuhakikisha janga lolote likitokea halikuangushi kabisa.

Ndani ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI utajifunza jinsi ya kulinda fedha zako zisiathiriwe na majanga mbalimbali. Hakikisha unapata nakala yako ya kitabu kujijenga imara kifedha.

Rafiki, misingi hii saba pamoja na hatua za kuchukua kwenye kuijenga imeelezwa vizuri sana kwenye kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI. Hakikisha unapata nakala yako ili ujiimarishe kifedha na kuwa huru.

JINSI YA KUPATA KITABU CHA USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI.
Rafiki, kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy) na unaweza kukipata popote ulipo Tanzania na nchi za jirani.

Kwa Dar Es Salaam unaletewa kitabu ulipo na kwa mikoani na nchi jirani unatumiwa kwa njia ya basi.

Bei ya kitabu kwa sasa ni Tsh elfu ishirini (20,000/=) tu. Hapa unakwenda kupata thamani kubwa sana kwa kiasi hicho cha fedha utakachowekeza.

Kujipatia nakala yako ya kitabu wasiliana na namba ya simu; +255 752 977 170 sasa.

Karibu sana ujipatie nakala yako ya kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI, uweze kujiimarisha kifedha ili kuwa na maisha huru.

Karibu upate muhtasari wa kitabu cha USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini.


View: https://youtu.be/mh2ZOz4aPVw

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
 
Nimeisoma nikaja nikaangalia muda tangu mada imetumwa nikajisemea moyoni ingekua mada ilee.....
 
Back
Top Bottom