Kitakachokufanya uone mambo ni rahisi ni "Imani" wakati "Akili" itakufanya uone mambo ni magumu

Kitakachokufanya uone mambo ni rahisi ni "Imani" wakati "Akili" itakufanya uone mambo ni magumu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Leo sina mengi ya kuandika,

Watoto wanaimani kuliko watu wazima. Sio ajabu wakaona mambo ni rahisi. Imani ndio kitu pekee kitakachokufanya uone maisha ni Rahisi. Ukiona unayaona maisha ni magumu basi elewa tayari ushaanza kukomaa kiakili. Hiyo ni ishara Namba moja ya mtu aliyekomaa.

Mtu mwenye akili haamini kuwa mambo huja kirahisi. Hivyo ni ngumu sana kumtapeli kwani naamini katika mambo rahisi/njia ya mkato. Wakati mtu mwenye akili ndogo yeye huona mambo katika urahisi, hivyo ni rahisi kutapeliwa.

Angalia akili za watoto, Angalia akili za wanafunzi au wanachuo wengi wao huongozwa na Imani zaidi kuliko akili. Hivyo wanafikiri kirahisi rahisi.

Kuongozwa na Imani ni kujidanganya, kujitapeli wakati kuongozwa na akili ni kuishi maisha halisi, na ni rahisi kufanikiwa.

Matapeli iwe WA Kisiasa, Kidini au kibiashara wanatumia Akili zao kuzichota Imani za watu kuwapa matumaini, faraja na matatajio ya uongo. Ukienda Kwa mganga WA kienyeji au mchungaji wa uongo atahakikisha hutumii Akili yako kutafakari Ila ataichochea Imani yako ili uwe kama mwendawazimu. Atakuaminisha vitu vya Uongo.

Kitu pekee ambacho watakudhibiti ni matumizi ya akili yako. Ogopa mtu yeyote asiyetaka kuipa akili yako nafasi ya kutafakari, ogopa Sana mtu wa namna hiyo. Huyo ni Tapeli.

Nilisema sitaandika Sana.

Niwatakie maandalizi Mema ya SABATO.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom