Kitakachompa urais Trump mwaka huu ni sakata la wahamiaji haramu

Kitakachompa urais Trump mwaka huu ni sakata la wahamiaji haramu

Sijui kwanini Democrats wanaweka pembeni watu wa maana.

Haiingii akilini chama chenye watu kama Bernie Sanders au Tulsi Gabbard kimpitishe akili ndogo kama Kamala tena bila kupingwa.
Kwa hiyo wewe unayekula ugali na kisamvu hapo Ukonga Mazizini ndio unafahamu kuliko wamarekani wenyewe...❗❗❗
 
Weka kwanza source ya hii habari yako. Usipende kubandika tu as if ni maandishi yako. Weka source tafadhali.
Hii sio habari mkuu ni uchambuzi.

Kama utahitaji sources nielekeze ni sehemu inahitaji clarification niongeze!
 
Habari zenu wanajamvi. Mko vizuri?

Kama unafuatilia jukwaa hili basi bila shaka utakuwa unafahamu mengi kuhusu mbio za uchaguzi zinazoendelea Marekani.

Ni Trump Vs Kamala. Hii hata watoto wa 2000 watakuwa wanafahamu.

Wengi wasichofahamu ni kuwa karibu kila opinion poll Marekani inatabiri kuwa Donald Trump anaenda kushinda uchaguzi huu.

View attachment 3085079

Kuanzia NBC, Politico, Economic Times n.k wote wanatabiri kuwa huenda Baba Ivanka ifikapo Januari 6 2025 atakuwa amekunja nne pale Oval Office, White House.

But why?

Tangu Biden aingie madarakani inakadiriwa kuwa kuna wahamiaji haramu takriban Milioni 8 wameingia nchini Marekani na kati yao Milioni 6.7 wameingia kupitia mpaka wa Southwest.

Hiyo population ni sawa na mji wa Dar Es Salaam pamoja na Mwanza ukijumlisha pamoja na hiyo imefanyika ndani ya miaka minne tu wa utawala wa Biden na Harris.

Wahamiaji hawa wamekuwa ni mwiba mkali mno kwa wamarekani ambao wamekuwa wakilalamika kuwa wahamiaji hao wengi ni majambazi, wauwaji and most of all wanachukua ajira zao kwani wanalipwa ujira mdogo mno.

View attachment 3085080

Trump analitambua hilo na ndio maana kwenye kila speech yake amekuwa akilizugumza suala la uhamiaji kwa wivu mkubwa kwani most Americans hasa wa vijijini wamechoka kuishi kwa hofu ya kuvamiwa na wahamiaji hao.

Kamala kwa upande yeye ni pro migration, the reason being wapiga kura wake wengi ni wahamiaji.

Novemba 5 inakaribia na bila shaka wamarekani wengi watamuunga mkono bwana Trump ambaye ameahidi kuwarudisha wahamiaji wote kwenye nchi zao.

Nawasilisha.

We can't wait!
Ninachofaham mimi dunia bado haiko tayari kuongozwa na 'dem'.
 
Hii sio habari mkuu ni uchambuzi.

Kama utahitaji sources nielekeze ni sehemu inahitaji clarification niongeze!
Unasema ni uchambuzi wako huku ukitaja hizo media outlets kama chanzo cha habari iliyoko kwenye “uchambuzi” wako halafu huweki source akili ya wapi ama umejifunza wapi?

Kama umesoma, hujui kitu kinaitwa “citations”?

Eti kama “sehemu nahitaji clarification”

Unaongea vitu gani?
 
Sina ninachofahamu mkuu, vipi anaendeleaje Kamala wako?
Wamarekani wamechoka na wazamiaji hivyo hii ndio karata itakayompatia Trump ushindi na wala sio swala la jinsia hivyo sasa inatakiwa kila mtu akae kwao.
 
US wote ni wahamiaji wenyeji hawapo tena, ila Trump atspita sababu kuu ni kwamba wa marekani hawawezi ku-trust a female predident.
Wenyeji bado wako, ila wamekuwa overrunned na wahamiaji, wahamiaji wamekuwa wengi kuliko wenyeji
 
Una takwimu zozote au unaongea tu kama wa kijiweni.
Kijana mdogo sana, current population ya US ni 346 million, on that native americans wako 10 million (wakaazi halisi wa bara america kabla ya wazungu kufika), ina include indians na tribes zingine and thats makes 2.9% ya raia wa marekani.

As statistics za 2023 kuna almost 47.8 million immigrants wako ndani ya US. Na hawa ni documented kuachilia mbali wanaojificha, na hiyo ni almost 14.3%.

The rest ni blacks and whites ambao wamekuwepo hapo muda mrefu kutokana na biashara ya utumwa, na mambo mengine
 
US wote ni wahamiaji wenyeji hawapo tena, ila Trump atspita sababu kuu ni kwamba wa marekani hawawezi ku-trust a female predident.
Hao wahamiaji ndiyo waliounganisha ile miji na nchi wakatengeneza nchi moja, wakaijenga mifumo ya kiulinzi, teknolojia, uchumi, elimu na kila kitu. So hao ndiyo wenye bila hao hapakuwahi kuwepo na USA.
Siku nyingine mnaposema na wao ni wahamiaji mjaribu kutumia common sense, japo kidogo tu itawasaidieni.
 
Wenyeji bado wako, ila wamekuwa overrunned na wahamiaji, wahamiaji wamekuwa wengi kuliko wenyeji
Wasichokijua, hao wanao waita wahamiaji ndiyo walioijenga USA katika kila mfumo. Wanaowaita wenyeji wao bado wanataka US yao iwe kama misitu ya Amazon, yaani wanataka kuendelea kuishi kama Wahadzabe.
USA haijawahi kukataa wahamiaji, maana wahamiaji ndiyo nguvu yao ilipo, madai ya Trump na tunaomuunga mkono ni dhidi ya Wahamiaji haramu. Utaratibu wa kujitambulisha na kuhamia upo lakini wao hawataki kuufuata.
 
Back
Top Bottom