Uchaguzi 2020 Kitakachotugharimu Upinzani kwenye huu Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Kitakachotugharimu Upinzani kwenye huu Uchaguzi

fenestra rotunda

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2015
Posts
608
Reaction score
614
Ni wazi sasa kuwa nguvu kubwa imewekwa kwenye Urais huku Ubunge na Udiwani ukiwekwa pembeni. Hili linadhihirishwa kwa jinsi matatizo ya kuenguliwa wagombea yalivyoshughulikiwa mpaka dakika ya mwisho, na vile muda wa kukata rufaa umeshaisha tayari.

Bila kuwapa support hao wagombea waliopata matatizo ni Serikali gani unaenda kuiunda? Hata ukishinda si wabunge wa chama tawala kwa idadi yao wanaweza kukupigia kura ya kutokuwa na imani na wewe na wakakutoa mapema chomboni na hivyo kukuharibia.

Kwa Uchaguzi ulivyo ni kama vile tume wanamjua mshindi, kama tuu wagombea kuenguliwa imeisha kimyakimya hivyo basi tutegemee hata kwenye matokeo ya urais mambo watakuwa hivyo hivyo na hata hiyo nguvu ya kuwekeza kwenye taasisi ya urais ikawa effortless na mkajikuta mnapoteza kotekote.

Pia, hiyo nguvu ya umma inayotegemewa kuleta haki kwenye kutangaza matokeo ya urais sio kitu cha kutegemewa saaana maana watz ni waoga ingawa hawatabiriki,kwa hiyo ni 50/50. Hii ni kwa sababu kama nguvu hii ingekuwa vivid basi walioenguliwa wote wangerudishwa.

Ni bora upinzani ungekomaa na ubunge na udiwani kwa kuwa hawa wakipita kwa wingi wanaweza leta mabadiliko hasa ya kutafuta katiba mpya na tume huru. Urais pia wangeweka nguvu ila sio kuhamisha nguvu zote huko kana kwamba tume ipo huru na italeta ushindi mezani.
 
Wewe sio mpinzani. Wewe ni mwana Lumumba ambaye umetumwa kufanya cheap propaganda humu.

Acha nikwambie, propaganda yako imeshafeli kabla haijaanza!!! Yanayotokea ni udhalimu wa CCM na vyombo vyake ila uzuri ni kuwa sasa ni baasi. Lazima tufundishane adabu mwaka huu!!
 
Ndo leo naona uzi wa mwanachadema mwenye akili kubwa.
Subiri kejeli kutoka kwa nyumbu wanyanyembe Chadema.
 
CCM wako kimya kama simba mwenda pole!

Wapinzani kelele nyingi kwenye mitandao wakati masuala muhimu katika Uchaguzi hawayajui!
 
Baada ya rufaa kukataliw a kwa dharau mabomu ya machozi au issue ya morogoro UNA SUGGEST WAFANYAJE LABDA? NJIA MBADALA NI IPI?
 
kamanda sasa umegundua kuwa ''upinzani'' hauna ngunvu ya umma, ngoja mnyooshwe mbele ya Amsterdam.
bibi bomba, kungekuwa hakuna nguvu ya umma mngeshamuengua Lissu kama mlivyokua mnajidanganya hapo Lumumba.

Tena wewe unayetegemea wingi wa kura za Pombe ndiyo uteuliwe kupitia viti maalumu jiandae kwenda kulima maharage machanga huko Songwe.
 
Wewe sio mpinzani. Wewe ni mwana Lumumba ambaye umetumwa kufanya cheap propaganda humu.

Acha nikwambie, propaganda yako imeshafeli kabla haijaanza!!! Yanayotokea ni udhalimu wa CCM na vyombo vyake ila uzuri ni kuwa sasa ni baasi. Lazima tufundishane adabu mwaka huu!!
Tunafundishana adamu humu kwenye mitandao tu, hamna tofauti na nyuki wa mashineni
 
Man
Bila kuwapa support hao wagombea waliopata matatizo ni Serikali gani unaenda kuiunda? Hata ukishinda si wabunge wa chama tawala kwa idadi yao wanaweza kukupigia kura ya kutokuwa na imani na wewe na wakakutoa mapema chomboni na hivyo kukuharibia.
Maneno haya ndiyo hoja yako ya msingi katika uzi huu
Raisi anaweza kulivunja Bunge wakati wowote kwa mujibu wa katiba endapo ataona haungwi mokono katika hoja zake.Na anaweza kuitisha uchaguzi Mpya.
Lakini
Ukweli ni kwanmba Wapinzani tunajaribu kuchezesha kete wakati tayari CCM wana Kingi,

Ni ukweli usiopingika kuwa wapinzania tuna 'pss time tuu' pasipo na tume huru ukweli unajulikana kuwa CCM wanatumia dola na tume iliyopo kubaki madarakani.

Ila uwanaume ni kujaribu sio kulala chali, CCM akijibwaga tuu tunachukua advantage.

''If you want to win the race put your legs on the track'
' lolote linaweza kutokea kwa mpinzani wako ukachukua advantage.
We vipi wewe?
 
Wewe sio mpinzani. Wewe ni mwana Lumumba ambaye umetumwa kufanya cheap propaganda humu.

Acha nikwambie, propaganda yako imeshafeli kabla haijaanza!!! Yanayotokea ni udhalimu wa CCM na vyombo vyake ila uzuri ni kuwa sasa ni baasi. Lazima tufundishane adabu mwaka huu!!
Hiyo adabu utaifundishia wapi Kwenye keybodi au
 
Back
Top Bottom