SoC03 Kitambulisho cha Taifa kiboreshwe ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali

Stories of Change - 2023 Competition

Rs MI

Senior Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
185
Reaction score
591
Nakala.png

Kitambulisho cha taifa hutumika kuthibitisha uraia wa mwananchi kwenye taifa husika. Lakini namna ulimwengu unavyoshuhudia ukuaji wa kasi kwenye sekta ya teknolojia ni vizuri kuboresha kitambulisho cha taifa kwa kukiwezesha kubeba taarifa nyinginezo muhimu pamoja na nyaraka za mhusika. Itasaidia katika kuepuka changamoto zitokanazo na njia za utunzaji wa taarifa za mhusika.

Tanzania kitambulisho cha taifa hubeba taarifa kama, majina ya wazazi wake, eneo alipozaliwa, eneo alipokua wakati anaomba kitambulisho, kazi yake, tarehe ya kuzaliwa na jinsia. Ila kupitia ulimwengu huu wa teknolojia kitambulisho cha taifa kiongezewe taarifa na nyaraka za raia ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Kuwezesha jambo hili itabidi kutengeneza mfumo maalumu utakaobeba taarifa na nyaraka za kila raia mwenye kitambulisho cha taifa. Mfumo huo utabeba taarifa za mhusika kutoka taasisi mbalimbali, kwa maana hiyo hautaathiri/kuzuia kazi za taasisi hizo. Taarifa hizi zitahifadhiwa kwa mfumo wa akaunti za watu kama ilivyo kwa mitandao ya kijamii. Mfano mtandao wa Jamii forum unavyobeba akaunti za watumiaji wake, ila utofauti ni kwamba kwenye mfumo huu haitakua rahisi kwa mtu/watu kuona taarifa zao au za wengine isipokua kwa kibali maalumu.

Nyaraka zipi zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kitaweza kubeba nyaraka zifuatavyo za mhusika; pasipoti, leseni ya udereva, Cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, vyeti vya vifo vya wazazi na watoto, vyeti vya taaluma, leseni za fani mbalimbali, tiketi za safari za mhusika, hati miliki za mali mbalimbali kama nyumba au shamba na cheti cha ndoa. Nyaraka hizi zitajumuishwa kwenye kitambulisho cha taifa kama nakala laini (soft copy) zitakazohifaziwa kwenye akaunti ya mhusika kwenye mfumo maalumu utakaoundwa kwaajili ya jambo hili kwenye kila idara/taasisi husika.

Taarifa zipi nyingine zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kiwezeshwe kubeba taarifa nyinginezo muhimu za mhusika kama; taarifa za mpiga kura, taarifa za kibenki, historia ya uhalifu, kazi yake, namba ya mlipa kodi, historia za maeneo aliyowahi kufika, hali yake kiafya na pia historia ya matibabu aliyopokea kwenye vituo vya afya.

Ni kwa namna gani taarifa na nyaraka hizo zitaweza kubebwa kwenye kitambulisho cha taifa?
Nyaraka na taarifa za mhusika hazitoonekana kwenye kitambulisho halisi bali zitaonekana kupitia vifaa vya kidigitali kama simu janja na kumpyuta ila kwa msaada wa kitambulisho halisi. Inaweza kua kupitia namba za kitambulisho au kuingiza/kusugua kitambulisho husika kwenye kifaa maalumu kitakachoweza kusoma taarifa za mhusika kutoka idara/tasisi mbalimbali zilizounganishwa na kitambulisho hicho au kuskani kupitia msimbo (QR code) utakaochapishwa kwenye kitambulisho hicho.
Kitambulisho cha taifa.png
Kwa maana hiyo kitambulisho hiki itabidi kuboreshwa na kukifanya cha kidigitali zaidi (kitambulisho cha kielektroniki) kwa minajili ya kuendana na mfumo huu. Picha ya chini ni mfano wa kitambulisho cha kidigitali.
Mbele.png

Nyuma.png

Je, ni faida zipi zitapatikana kupitia maboresho haya?
  • Kupunguza mzigo wa kubeba nyaraka nyingi na kupunguza upotevu wa muda,
Kitambulisho hiki kitakapobeba nyaraka nyinginezo za mhusika, ikiwemo leseni, vyeti, bima na nyinginezo, itasaidia kutobeba nyaraka nyingi zitakapohitajika sehemu/eneo fulani.

Halikadhalika itamwezesha mhusika kutoa pesa benki pamoja na kufanya malipo ya kiserikali na kibinafsi kupitia kitambulisho chake cha taifa.
  • Kurahisisha upelelezi matukio ya uhalifu,
Kitambulisho kitabeba historia za uhalifu za mhusika kutoka mahakamani na vyombo vya usalama (kama askari wa barabarani), hii itasaidia kugundua iwapo mtuhumiwa/mhusika ni mhalifu wa mara nyingi au mara chache. Pia kupitia historia za safari za mhusika iwapo alitumia vyombo vya usafiri vinavyotoa tiketi itajulisha kama mhusika alifika eneo la uhalifu.

Zaidi itatokea ulazima wa kutumia kitambulisho hiki kwenye huduma mbalimbali jambo ambalo itakua rahisi kutambua eneo ambalo mtu yupo pindi atakapotumia kitambulisho chake ikiwa anatafutwa kutokana na kutoroka baada ya kufanya uhalifu.
  • Kupunguza ughushi wa nyaraka,
Itawawia vigumu kughushi nyaraka kama vyeti vya taaluma au vyeti vya kuzaliwa, hati na leseni mbalimbali, kutokana na nyaraka zitakapowekwa kwenye mfumo huo hazitoweza kubadilishwa isipokua kupitia mamlaka rasmi.
  • Kupatiwa msaada wa kimatibabu kwa urahisi na ufanisi,
Kitakapobeba historia za matibabu na hali ya afya ya mhusika itasaidia mhusika kupata msaada wa haraka wa matibabu hata atakapokua hajitambui (amepoteza fahamu) lakini ana kitambulisho chake cha Taifa. Pia itasaidia kujua matibabu aliyopatiwa kwenye vituo vingine vya afya hapo kabla ili kuepuka mkanganyiko katika utoaji wa matibabu.
  • Kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji wa mapato.
Kutokana na kubeba namba ya mlipa kodi na pia kuwezeshwa kufanyia malipo itakua rahisi kwa upande wa serikali kukusanya mapato.

Je, Changamoto zipi zinaweza kuukumba mfumo huu?
  • Udukuzi wa taarifa,
Kukikosekana ulinzi imara wa mfumo huu, itakua rahisi kwa wadukuzi kupata taarifa nyingi za mlengwa kwa urahisi na muda mfupi kutokana taarifa nyingi kubebwa ndani yake.
  • Uvujishaji wa taarifa kupitia watumishi wasio waadilifu,
Watumishi wasio waadilifu waliopo kwenye sekta rasmi huweza kuvujisha taarifa za mhusika kutokana na uwezo wa kuona taarifa hizo.

Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizi?
  • Kutengeneza ulinzi imara wa kidigitali,
Kupitia kushirikiana wataalamu mashuhuri wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mfumo huu kuukinga kutokana na wadukuzi watakaojaribu kuingilia mfumo huu.
  • Kutengeneza sheria itakayowashughulikia vikali watakaobainika kudukua au kuvujisha taarifa zozote za raia,
Itasaidia watumishi kutokuvujisha taarifa na pia wadukuzi kutokujaribu kuingilia mfumo huu pindi watakaposhuhudia wengine waliojaribu/waliofanya hivyo wakiadhibiwa.
  • Kila sekta kupewa idhini ya kuona taarifa wanazoshabihiana nazo tu,
Itaongeza usiri katika taarifa na kupunguza uvujaji wa taarifa za raia.
  • Taasisi kutokua na uwezo wa kuingia kwenye baadhi ya taarifa za mhusika bila idhini yake,
Taasisi itakapohitaji kuona baadhi ya taarifa za mhusika itambidi mhusika athibitishe kukubali kupitia kuweka nywila yake au alama zake za vidole.
  • Kuwapatia raia elimu,
Itaepusha sintofahamu zitakazoweza kutokea kutokana na kutokua ufahamu kuhusu mfumo huu. Itasaidia raia kuendana na mfumo huu kwa wepesi na muda mfupi.

Hivyo basi, ulimwengu wa kidigitali utumike vyema kuboresha kitambulisho cha taifa ili kufaidika nao. Zipo faida nyinginezo zitakazotokana na mfumo huu kama utunzaji wa mazingira, kutokana na matumizi ya karatasi zitokanazo na miti yatapungua kutokana na nyaraka nyingi kuhifadhiwa kwenye mfumo huu. Ni jambo rahisi kufanikisha jambo hili iwapo tu serikali itatambua faida zake na kuamua kuwekeza jitihada zake kwenye kuwezesha jambo hili ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Angalizo: Kila taasisi itabaki kama kawaida na kazi yake ila taarifa zake zitaonekana au kufanya kazi kupitia kitambulisho cha taifa.

Upvote 760
Dah. Nlikuwa nasoma nikawa nangoja nifike kipengele changuii. Dah na kweli kipo ndani.
Hili andiko naunga mkono na lipite. Nliwah kuwa na wazo hili.
Pale africa ya kusini ukifanya kosa wakichukua alama zako za vidole hata ukikimbia siku ukishuka uwanja wa ndege ukigusa masgine zao wakati wana kukagua tuuu wanafahamu na wanaanza na wewee.

Hospitali hivyo hivyooo
 
Itakua jambo zuri sana na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhalifu.
 
Karibuni, kupigia kura chapisho hili gusa alama ya ^ iliyopo mwishoni mwa andiko upande wa kulia.
Wazo lako ni zuri lakini faida kubwa itakuwa ni kwa mamlaka za kiutawala na wala si kwa raia.Nadhani watu wengi hupenda kubaki na taarifa zao muhimu za siri.Kama ulivyoonesha wasi wasi wako kuhusu udukuzi.Hilo jambo lipo na kila tunavyoendelea wadukuzi wanaongezeka kutokana na kuongezeka idadi ya wasomi wa taaluma ya teknohama.
Kuwazuia inakuwa ni kazi kweli. Afadhali waisihie kujua tarehe yako ya kuzaliwa tu kuliko kuona taarifa zako za benki na afya yako na mengineyo muhimu.
Upande mwengine napenda kujua faida ya sisi kukupigia kura.Jee kuna malipo unataraji kulipwa kutokana na andiko hili au ni kwa ajili ya nini.Vyenginevyo ungewacha tu hicho kialama cha kupiga kura kwani atakayependezewa atakupenda tu na hiyo itakuwa ni uhakika kuliko kupenda bila kukusudia.
 
Dah. Nlikuwa nasoma nikawa nangoja nifike kipengele changuii. Dah na kweli kipo ndani.
Hili andiko naunga mkono na lipite. Nliwah kuwa na wazo hili.
Pale africa ya kusini ukifanya kosa wakichukua alama zako za vidole hata ukikimbia siku ukishuka uwanja wa ndege ukigusa masgine zao wakati wana kukagua tuuu wanafahamu na wanaanza na wewee.

Hospitali hivyo hivyooo
Mimi kama niliwahi kukosa huko nyuma na nikatubu sipendi mtu anifuatefuate tena na kunikumbusha mambo yale.Sasa huu utaratibu hauna msamaha.
Na kama nimekwenda pahala nje ya nchi nimeona kuna fursa nyingi nikapenda nami nifaidike hapo halafu nitulie nimalizie umri wangu.Nitapenda kama kuna uwezekano wa kuficha mikasa yangu ya nyuma basi nifanye hivyo na sitapenda watu wa hapo wanitafutie visa tunakokuita kufukua makaburi.
 
Kuna watu wanafanya matukio makubwa kama kuua/kubaka na wanapokimbilia eneo lingine inakua vigumu kuwapata. Kwa hiyo unamaanisha mpaka wao wanahitaji kusamehewa na kutokuchukuliwa hatua zozote za kisheria?
 
Mkuu, nitoe taarifa tu hapa; kitambulisho cha taifa kinazo taarifa za vyeti vya kuzaliwa pamoja na taaluma hadi cheti cha mlipa kodi inategemea tu aliyekuandikisha kama alikuwa active.

Binafsi wakati najiandikisha nilipeleka faili lenye vyeti vyangu vyote vika scaniwa walitaka hadi vya wazazi nikawa sina.

Lakini hapo hapo kituoni tulikuwa wwngi ila wengi hawakuchukulia serious, wakaenda bila hivyo viambatanisho.

Nadhani wanaokwenda kujiandikisha sasa hivi, wajitahidi sana kuwa na taarifa zao kamili na viambatanishi. Na hili lipo wazi sema tu tafsiri ndio inasumbua na waandikishaji wengi walifanya kazi ya uandikishaji hovyo, wengi majina yalikosewa na vijana wengi hawakuelezwa taarifa muhimu za kuambatanisha.

Ilikuwa ni kama bora liende tu.
 
Basi ni vizuri likatiliwa mkazo zaidi
 
Unakuta mtu mmoja amebeba kitambulisho cha taifa, kitambulisho cha mpiga kura, bima ya afya na pia leseni wakati ni jambo linalowezekana kwa taarifa zote hizo kujumuishwa kwenye kitambulisho kimoja tu cha Taifa na kumpunguzia mzigo mtu huyu.
Uko sahihi kbs mkuu, hongera sana kwa andiko lako zuri kbs
 
mkuu andiko lako ni zuri sana ila kwa tarifa ambazo unataka ziwepo kwenye kitambulisho cha taifa kitaondoa dhana zima ya privacy, pamoja na maendeleo ya kidigitali kuna watu na viatu, embu imagine mtu mwenye cheo mmekorofishana akishika kitambulisho chako ana details zote za maisha yako...nini kitatokea?

mimi naomba kuchangia zaidi, na nadhani ndio kinachofanyika, ni hivi hizi taarifa zote zipo captured na taasisi tofauti, ukienda bima, wana taarifa zako za afya hata kama ulipimwa tezi dume kwa dole inaonekana, ukienda rita mambo yote ya mirathi,kifo, uzazi n.k, ukienda TRA na Brela biashara ziko wazi, ukienda ardhi viwanja, nyumba na mashamba wazi wazi vinaonekana kwa namba yako ya taifa ujue, ...taarifa pekee mtu mwingine bila kujali taasisi anatakiwa kuona ni kama zinavyoonekana kwenye kitambulisho kwa muda huu. mtu akitaka taarifa nyingine akazifuate kwenye mamlaka husika. Hivyo nadhani Vitambulisho vya taifa vipo sawa na serikali ingeweza basi kwenye kitambulisho ionekane picha na jina pamoja na barcode tuu, ambazo zinaweza kuwa scanned na taasisi za serikali tuu ku access taarifa kama umri, ulipozaliwa na signature
 
Ni kweli Mkuu, ila ndio maana nimeshauri walau kila sekta ipewe idhini ya kuona taarifa wanazoshahibiana nazo. Mfano kama ni hospitali basi wawe na uwezo wa kuona taarifa za afya tu, kama kama ni benki wataziona za benki tu.

Kiufupi ni kwamba kila mamlaka itabaki kusimamia taarifa zake ila utofauti ni kwamba zitawezeshwa kuonekana kupitia kitambulisho cha taifa kwenye taasisi mbalimbali pale zitakapohitajika.

Mfano unapoenda hospitali (kwa wenye bima) hawatakua na haja ya kupewa kitambulisho cha bima tena bali kupitia kitambulisho chake cha taifa hospitali husika itaweza kuona bima ya mhusika na kumhudumia.
 
View attachment 2621440
Kitambulisho cha taifa hutumika katika kuthibitisha uraia wa mwananchi kwenye taifa husika. Lakini namna ulimwengu unavyoshuhudia ukuaji wa kasi kwenye sekta ya teknolojia ni vizuri kuboresha kitambulisho cha taifa kwa kukiwezesha kubeba taarifa nyinginezo muhimu pamoja na nyaraka za muhusika. Itasaidia katika kuepuka changamoto zitokanazo na njia za utunzaji wa taarifa za mhusika.

Tanzania kitambulisho cha taifa hubeba taarifa kama, majina ya wazazi wake, eneo alipozaliwa, eneo alipokua wakati anaomba kitambulisho, kazi yake, tarehe ya kuzaliwa na jinsia. Ila kupitia ulimwengu huu wa teknolojia kitambulisho cha taifa kiongezewe taarifa na nyaraka za raia ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Ili kuwezesha jambo hili itabidi kutengenezwa mfumo maalumu utakaobeba taarifa na nyaraka za kila raia mwenye kitambulisho cha taifa. Mfumo huo utabeba taarifa za mhusika kutoka taasisi mbalimbali, kwa maana hiyo hautaathiri/kuzuia kazi za taasisi hizo. Taarifa hizi zitahifadhiwa kwa mfumo wa akaunti za watu kama ilivyo kwa mitandao ya kijamii. Mfano mtandao wa Jamii forum unavyobeba akaunti za watumiaji wake, ila utofauti ni kwamba kwenye mfumo huu haitakua rahisi kwa mtu/watu kuona taarifa zao au za wengine isipokua kwa kibali maalumu.

Nyaraka zipi zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kitaweza kubeba nyaraka zifuatavyo za mhusika; pasipoti, leseni ya udereva, Cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, vyeti vya vifo vya wazazi na watoto, vyeti vya taaluma, leseni za fani mbalimbali, tiketi za safari za muhusika, hati miliki za mali mbalimbali kama nyumba au shamba na cheti cha ndoa. Nyaraka hizi zitajumuishwa kwenye kitambulisho cha taifa kama nakala laini (soft copy) zitakazohifaziwa kwenye akaunti ya mhusika kwenye mfumo maalumu utakaoundwa kwaajili ya jambo hili.

Taarifa zipi nyingine zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kiwezeshwe kubeba taarifa nyinginezo muhimu za muhusika kama, taarifa za mpiga kura, taarifa zake za kibenki, historia yake ya uhalifu, kazi yake, namba ya mlipa kodi, historia za maeneo aliyowahi kufika, hali yake kiafya na pia historia ya matibabu aliyopokea kwenye vituo vya afya.

Ni kwa namna gani taarifa na nyaraka hizo zitaweza kubebwa kwenye kitambulisho cha taifa?
Nyaraka na taarifa za mhusika hazitaonekana kwenye kitambulisho halisi bali zitaonekana kupitia vifaa vya kidigitali kama simu janja na kumpyuta ila kwa msaada wa kitambulisho halisi. Inaweza kua kupitia namba za kitambulisho au kuingiza/kusugua kitambulisho husika kwenye kifaa maalumu kitakachoweza kusoma taarifa zilizopo ndani ya kitambulisho hicho au kuskani kupitia ‘QR code’ zitakazochapishwa kwenye kitambulisho hicho.
Kwa maana hiyo kitambulisho hiki itabidi kuboreshwa na kukifanya cha kidigitali zaidi (kitambulisho cha kielektroniki) kwa minajili ya kukiimarisha kuendana na mfumo huu. Picha ya chini ni mfano wa kitambulisho cha kidigitali.
View attachment 2621444
View attachment 2621446

Je, ni faida zipi zitapatikana kupitia maboresho haya?
  • Kupunguza mzigo wa kubeba nyaraka nyingi na kupunguza upotevu wa muda,
Kitambulisho hiki kitakapobeba nyaraka nyinginezo za mhusika, ikiwemo leseni, vyeti, bima na nyinginezo, itasaidia kutokubeba nyaraka nyingi zitakapohitajika sehemu/eneo fulani. Pia itamwezesha mhusika kutoa pesa benki kupitia kitambulisho chake cha taifa.

Pia kitambulisho hiki kiwezeshwe kufanya malipo ya kiserikali na malipo binafsi jambo litakalorahisisha ulipaji wake.
  • Kurahisisha upelelezi matukio ya uhalifu,
Kitambulisho kitabeba historia za uhalifu za mhusika kutoka mahakamani na vyombo vya usalama, hii itasaidia kufahamu kama mtuhumiwa ni mhalifu wa mara nyingi au mara chache. Pia kupitia historia za safari za mhusika iwapo alitumia vyombo vya usafiri vinavyotoa tiketi itajulisha kama muhusika alifika eneo la uhalifu.
Pia itatokea ulazima wa kutumia kitambulisho hiki kwenye huduma mbalimbali jambo ambalo itakua rahisi kutambua eneo ambalo mtu yupo pindi atakapotumia kitambulisho chake ikiwa anatafutwa kutokana na kufanya uhalifu.
  • Kupunguza ughushi wa nyaraka,
Itawawia vigumu kughushi nyaraka kama vyeti vya taaluma au vyeti vya kuzaliwa, hati na leseni mbalimbali. Hii ni kutokana nyaraka hizi zitakapowekwa kwenye mfumo huo hazitoweza kubadilishwa isipokua kupitia mamlaka rasmi.
  • Kupatiwa msaada wa kimatibabu kwa urahisi na ufanisi,
Kitakapobeba historia za matibabu na hali ya afya ya mhusika itasaidia mhusika kupata msaada wa haraka wa matibabu hata atakapokua hajitambui (amepoteza fahamu) lakini ana kitambulisho chake cha Taifa. Pia itasaidia kujua matibabu aliyopatiwa kwenye vituo vingine vya afya hapo kabla ili kuepuka mkanganyiko katika utoaji wa matibabu.
  • Kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji wa mapato.
Kutokana na kubeba namba ya mlipa kodi na pia kuwezeshwa kufanyia malipo itakua rahisi kwa upande wa serikali kukusanya mapato.

Je, Changamoto gani zinaweza kuukumba mfumo huu?
  • Udukuzi wa taarifa,
Kukikosekana ulinzi imara wa mfumo huu, itakua rahisi kwa wadukuzi kupata taarifa nyingi za mlengwa kwa urahisi na muda mfupi kutokana taarifa nyingi kubebwa ndani yake.
  • Uvujishaji wa taarifa kupitia watumishi wasio waadilifu,
Watumishi wasio waadilifu waliopo kwenye sekta rasmi huweza kuvujisha taarifa za mhusika kutokana na uwezo wa kuona taarifa hizo.

Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizi?
  • Kutengeneza ulinzi imara wa kidigitali,
Kupitia kushirikiana wataalamu mashuhuri wa ndani na nje ya nchi watakaokua wanasimamia mfumo huu ili kuukinga kutokana na wadukuzi watakaojaribu kuingilia mfumo huu.
  • Kutengeneza sheria itakayowashughulikia vikali watakaobainika kudukua au kuvujisha taarifa zozote za raia,
Itasaidia watumishi kutokuvujisha taarifa na pia wadukuzi kutokujaribu kuingilia mfumo huu pindi watakaposhuhudia wengine waliojaribu/waliofanya hivyo wakiadhibiwa.
  • Kila sekta kupewa idhini ya kuona taarifa wanazoshabihiana nazo tu,
Itaongeza usiri katika taarifa na kupunguza uvujaji wa taarifa za raia.
  • Taasisi kutokua na uwezo wa kuingia kwenye baadhi ya taarifa za mhusika bila idhini yake,
Taasisi itakapohitaji kuona baadhi ya taarifa za mhusika itambidi mhusika athibitishe kukubali kupitia kuweka nywila yake au alama zake za vidole.
  • Kuwapatia raia elimu,
Itaepusha sintofahamu zitakazoweza kutokea kutokana na kutokua ufahamu kuhusu mfumo huu. Pia itasaidia raia kuendana na mfumo huu kwa wepesi na muda mfupi.

Hivyo basi, ulimwengu wa kidigitali utumike vyema kuboresha kitambulisho cha taifa ili kufaidika nao. Pia zipo faida nyinginezo zitakazotokana na mfumo huu kama utunzaji wa mazingira. Hii ni kutokana kwamba matumizi ya karatasi zitokanazo na miti yatapungua kutokana na nyaraka nyingi kuhifadhiwa kwenye mfumo huu. Ni jambo rahisi kufanikisha jambo hili iwapo tu serikali itatambua faida zake na kuamua kuwekeza jitihada zake kwenye kuwezesha jambo hili ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Angalizo: Kila taasisi itabaki kama kawaida na kazi yake ila taarifa zake zitaonekana au kufanya kazi kupitia kitambulisho cha taifa.

Una hoja muhimu sana, usikilizwe!
 
Kupata kitambulisho chenye picha, jina na tarehe ya kuzaliwa tu, inawachukua NIDA zaidi ya miaka mitano.
Kwa hiyo kutoa kitambulisho chenye taarifa zote hizo, NIDA watahitaji si chini ya miaka 60.

Kwa maana hiyo, wengine watapatiwa vitambulisho vyao wakiwa paradiso au jehanamu.
 
Back
Top Bottom