Kitandani kwetu...

Kitandani kwetu...

SAKATA LENYEWE NI HIVI:
Juzi nilipata safari ya peke yangu! Niliporudi nilimkuta NO! niliwafumania mume huyo chumbani kwetu akiwa na mwanamke kitandani kwetu...(you know what they were doing)!!!
Ni kama nilipatwa na shoti ya umeme kwa dakika kadhaa...nilichoweza kufanya ni kutoa simu yangu ya kiganjani na kuwapiga picha kadhaa. Nikaondoka kabisa maeneo yale na kwa kweli mpaka sasa ninalala kwa ndugu zangu!
Sijui nitaanzaje kulala tena ktk kile kitanda chetu na nihisi raha kama zamani!
Huwa ninaenda kuchukua vifaa ninavyohitaji, na nilimuuliza kwa nini anafanya vile, anajibu oo eti bahati mbaya shetani kanipitia!!! kakupitia in our bed!!!
Wana JF, uamuzi ninaoona unafaa ni kumtaliki, kwa sababu amekuwa akinidangaya kwa kisingizio kuwa eti ana presha!
Lkn kabla sijachukua hatua hii nimeona bora nipate ushauri wenu!
Please!!!

Kwa kweli hili jambo linauma sana na linaweza kukufanya na wewe upate hio BP kama yeye usipokuwa mwangalifu.

Hapa nafikiri ndio "end of the road" katika mapenzi yenu. Hili halihitaji mjadala hata kama wewe ndie unamtegemea yeye ukizingatia kwamba kwa sasa unaishi kwa nduguzo na hii inaonesha kwamba hata wewe huna mahala pako na hili ni tatizo kubwa kwenu ninyi wanawake.

Nasema hivyo kwa sababu kama wewe ndie unamtegema yeye basi anafanya hivyo akitegema kwamba wewe hautakuwa na mahala pa kujisitiri na mwisho utarudi kwake.

Pia kitendo cha kuwa unarudirudi pale na kumuuliza kwamba kwa nini alifanya hivyo naona hapa unafanya mchezo wa baba na mama. Ondoa nguo zako na kila kitu chako na endapo mungu amekupangia kupata mume mtaeelewana basi utapata.

Mwisho napenda kuona unajitahidi uwe na angalau kachumba ka kupanga na uchakarike na shughuli zilizo halali ili uweze kuishi kwa raha na jaribu kumsahau kabisa huyu jamaa.

Mimi nikiwa mwanamme sikushauri ili unifuate nisemayo bali nakupa mwanga wa kufikiri na kujua kuwa unaweza uka-stand kwa your own feet na kuendela na maisha yako, ikitokea Mungu kakupa pande utapat mwanamme mzuri kwako.
 
Pole sana dada yangu,

Ndoa ni ngumu sana na ndoa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, sio wanaume tu wanayofanya haya mambo hata wanawake wapo wanaofany vitu hivi.

Mimi ninachokushauri usisikirize nini watu wanasema, kwa sababu uzito wa penzi ulilonalo kwa mumeo unalijua wewe, uongea na moyo wako na usikirize unakuambia nini.

Na kama utaamua kumsamehe basi hata hicho kitanda hutakiwi kukilalia tena, toa na mnunue kingine. hakifai tenda.

Ingekuwa ni sisi wanaume ni wagumu sana wa kusamehe, hata tukisema tumesamehe hatuchelewi kulipiza.

Pia dada yangu kama unampenda mume wako ni bora usikirize moyo wako, usije kumuacha mumeo wakati bado unampenda then baadae mnaanza kuibana.

Ni hayo tu kwa leo.
 
...ni kweli, ila kwa "maoni yangu", anauma zaidi yule mume alokutoa kwenu ukiwa bado 'mbichi', humjui mw'ume -aka-bikra, naye ni msafi wa matendo na tabia, kinyume na hapo kuna "too many skeletons in the closet" - siri nyingi zilizofichika!, ambazo kwa kumshauri mwezetu aachane na mumewe ni makosa.
 
Pole sana dada kwa hayo yaliyokupata,

Mimi ninachojua maandiko (Biblia) inasema Mungu anakuchukia kuachana (I hate divorce," says the LORD God of Israel (Malachi 2:16)),kama ni ndoa ya Kikristo tunajua ni mke/mume mmoja tuu hata kifo kiwatenganishe.Isitoshe dada kama mna watoto watapata shida sana mama, mvumilie mumeo huku ukimwombea ili kulea watoto wenu.

Ushauri: Kama bado unampenda mumeo nakushauri mkapime magonjwa yatokanayo na hayo na kama yeye (mumeo) anaonyesha kuregret kitendo alichofanya, msamehe muanze maisha upya.

Muhimu: Mwombe Mungu sana aondoe roho ya tamaa aliyo nayo mumeo, haya yote yanawezekana kwa kumwamini Bwana Yesu kama Mwokozi. MUNGU ANAWEZA YOTE usife moyo.
 
Naam kama nyote mkiamua kuendelea na ndoa yenu, basi kupima magonjwa yote ya zinaa yanayosababishwa na kujamiina ikiwemo ukimwi ni muhimu kabla ya kujaribu tena kuijenga ndoa yenu upya. Najua ni rahisi mno kusema namtaliki, lakini usichukue uamuzi wa haraka na usifanye uamuzi huo pekee yako. Kila la heri.
 
Wewe nenda kapime uanze kutumia msaada wa Bush. Mijanaume mingine hii mizinzi kwa nini mnaolewa nayo?
 
Wewe nenda kapime uanze kutumia msaada wa Bush. Mijanaume mingine hii mizinzi kwa nini mnaolewa nayo?
Love doesn't ask why!? Kama bado yuko moyoni jaribu tena kujifanyia self assesment ujue mnapungukiwa na nini katika mahusiano yenu and once you know that you'll be able to set strategies to accomplish whatever decision you'll take!!!

Love is blind!Mwenye mapenzi chongo huita kengeza

Was ammended to Love isn't blind...it is the lovers who are blind!

Have courage and be wise!!
 
Aise wewe dada pole sana. Yaani jamaa anakula mzigo laivu..harafu alikuwa anakunyima....thats most unafair..Pole sana. Cha kufanya kwanza kaa chini utulie, usichukue maamuzi yoyote kwa sasa maana hasira ni mbaya na hiki kitendo alichokufanyia ni kibaya. Do you have children? kama unao wafikirie pia.

Ila wanaume na sisi....unakula mzigo kwenye matrimonial BED? it sucks!
 
Love doesn't ask why!? Kama bado yuko moyoni jaribu tena kujifanyia self assesment ujue mnapungukiwa na nini katika mahusiano yenu and once you know that you'll be able to set strategies to accomplish whatever decision you'll take!!!

Was ammended to Love isn't blind...it is the lovers who are blind!

Have courage and be wise!!

How can one be a lover without love?
If
Love makes Lovers
Lovers make themselves blind
Love makes Lovers Blind
 
Pole sana dada yangu,

Ndoa ni ngumu sana na ndoa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, sio wanaume tu wanayofanya haya mambo hata wanawake wapo wanaofany vitu hivi.

Mimi ninachokushauri usisikirize nini watu wanasema, kwa sababu uzito wa penzi ulilonalo kwa mumeo unalijua wewe, uongea na moyo wako na usikirize unakuambia nini.

Na kama utaamua kumsamehe basi hata hicho kitanda hutakiwi kukilalia tena, toa na mnunue kingine. hakifai tenda.

Ingekuwa ni sisi wanaume ni wagumu sana wa kusamehe, hata tukisema tumesamehe hatuchelewi kulipiza.

Pia dada yangu kama unampenda mume wako ni bora usikirize moyo wako, usije kumuacha mumeo wakati bado unampenda then baadae mnaanza kuibana.

Ni hayo tu kwa leo.

Ingawa jina lako Domo Kaya, umeongea sense sana.
Nimependa hako kapicha kako. Huyo mchumba kapendeza sana.
 
Unajua ingekua unyumba ulikuwepo na hakuna uongo kua ana pressure, I would say msamehe na muendelee na maisha maana wanaume uzinzi ni hulka zao na nyumba ndogo kwao ni sifa. lakini sasa ukijumlisha na unyumba ulikua hupati kwa kisingizio cha pressure halafu suddenly on your own bed with another woman. tena huko ndio anashughulika proper kuliko hata akiwa na wewe, hapa ni ngumu. kama unaweza kujitegemea ukiishi mwenyewe, ondoka my dear, maisha ni ya kupita na hatuishi mara mbili. huyo hana shida na wewe my dear. kwenye mapenzi unyumba hamnyimani. ikishafikia hatua hichi kitu hakipo, hakuna ndoa hapo, maana hata mkikwaruzana how do you reconcile jamani. kaanze maisha mbele ya safari, utashangaa kwanza utakavyofungukiwa.
ndoa za mateso zinarudisha maendeleo nyuma maana kutwa unawaza mapenzi ya kulazimisha badala ya kifikiria mambo ya maendeleo. utamsahau tu, kwani yeye ndio mungu wako my dear.
Naamini kweli mlipendana na ndio maana mkaoana, lakini kumbuka mapenzi huisha. si kwake tu hata kwako yangeweza kwisha siku moja pia. ndio maana wenzetu wana ndoa za mikataba, na ukiangalia sana wenzetu ni asilimia ndogo ya wanao cheat kwenye ndoa zao tofauti na waafrika.

Wandugu,

Nimewasoma!!!

Kiukweli tulikuwa tunapendana sana,so much so I was so blind to notice any signs!!!

Kusamehe "saba mara sabini" (hasa kwa wakristo) nadhani ni jambo la kheri, lkn kwa sasa kwa mimi ni gumu jamani, moyo wangu bado mzito sana tuuu sitaweza angalau kwa sasa, nahisi kukosewa heshima, nahisi aibu kwangu licha ya kwamba naye pia ametahayari!!! Mpaka najiuliza hivi nimepungukiwa nini mtoto wa watu mie...
Hebu niambieni, mkono wako unaotumia kula msosi, ukinyewa na mtu kama mumeo/mkeo/mtoto/etc, je utaukata???

Nadhani labda nifanye subira, jazba zipungue ndio nitafanya uamuzi. (Wajua kinachoniuma ni the fact that he screwed her in our bed! He didnt give a damn about our bed!! No respect at all!!I know that married men (majority) do cheat, but do it somewhere far! (Im not asking you to do it that way, dont cheat coz kuna kuumbuka...)

SANDA MATUTA,asante kwa ushauri wako!
lakini usitake kutisha watu na methali zako!
Marriage life is like a plant! Waweza kukua na kustawi vizuri,na either kutoa matunda au usitoe. Waweza kukua kidogo ukanyauka! Waweza kufa kabisa!
All in all unapopanda mbegu, mara nyingi tunategemea uote, ukue, ustawi vizuri ,na mwisho utoe matunda na mbegu nyingine!
Au sio jamani!?
...................
 
Dada divorce is always a choice. Mimi ni mwanaume lakini kama nikijiiba pembeni nishamwambia bibie kwamba chukua kilocho chako.

Hakuna ndoa hapo ndani mamaaa. Nenda zako
 
Uasherati umekuwepo toka dunia ilivyoumbwa ,tena mwanzilishi ni mwanamke kwa bahati mbaya. Hiyo ndio dhambi tulyozaliwa nayo.
Pengine hujui asilimia kubwa ya wanaume hufanya hivi, na hata wanawake yawezekana ikawa zaidi. Mume akienda safari yeye hujivinjari ndani kwao na serengeti boys . Kwa hiyo sio jambo la ajabu ila ni kwa kuwa lilifanyikia kitandani mwako tu.Haijalishi wapi limefanyikia kwa sababu kitendo ni hicho hicho.Ndio maana huitwa uasherati na dhambi. Na mtu akifanya dhambi apewe nafasi ya kutubu na kuomba msamaha. Kama binadamu usipoweza kumsamehe mwenzio tena umpaendae je wadhani Mungu atafikiriaje kukusamehe wewe siku yako ya adhabu? " EE MWALIMU , UNASEMA TUWASAMEHE WENZETU, JE MTU AKINIKOSEA NIMSAMEHE MARA NGAPI? ...........SABA SABINI.
Pole kwa kuumwa roho, lakini ndio hivyo. Hata ukimwacha ataoa mwingine na ndipo itakuuma zaidi hasa kama bado mnapendana.
 
Juzi nilipata safari ya peke yangu! Niliporudi nilimkuta NO! niliwafumania mume huyo chumbani kwetu akiwa na mwanamke kitandani kwetu...(you know what they were doing)!!!

Ni kama nilipatwa na shoti ya umeme kwa dakika kadhaa...nilichoweza kufanya ni kutoa simu yangu ya kiganjani na kuwapiga picha kadhaa. Nikaondoka kabisa maeneo yale na kwa kweli mpaka sasa ninalala kwa ndugu zangu!
Sijui nitaanzaje kulala tena ktk kile kitanda chetu na nihisi raha kama zamani!

Palloma, pole sana na huo mkasa uliokupata. JAMBO FORUM ni familia, usikonde tutakupa ushauri wa bure sisi wenye uzoefu wa muda mrefu katika ndoa. Naungana na wenzangu ambao wametoa michango ya mawazo yenye lengo la kujenga na si kubomoa. Ushauri wangu,ni kwa ni kuwa kama una nia ya kudumisha ndoa yako kwa manufaa ya watoto wenu (kama munao)ni kuwa haya masuala uyajadili kwa kina na mumeo na umwambie akuombe radhi na kuahidi kuwa mwaminifu. Akileta za kuleta peleka swala hili katika kikao cha ndugu au viongozi wa dini. Na kama katika kikao hicho atakataa kuomba radhi achana naye anza maisha yako. Akikuomba radhi, mwambie mununue kitanda kipya cha muundo tofauti na cha awali na mukipange orientation tofauti na hapo awali, akarabati hicho chumba (kupaka rangi mpya, kubadili curtain, taa nk) na ndipo angalau utapata raha kuingia na kulala humo. Kikubwa kushinda yote, mwambie mumeo amurudie na kumwogopa MWENYEZI MUNGU na aachane na zinaa, na wewe katu usije lipiza kisasi kwa kuzini. Yangu hayo tu dada Palloma. Nawasilisha!!!
 
Palloma,

Pole sana kwa hilo dada yangu, ila naomba ujisaulishe hayo yote, unajua unapokuwa umefanyiwa surgery zile dawa za usingizi hukufanya kama han...kwa muda, yawezekana alikuwa hajihisi kufanya na wewe akaona ajaribu kwa mwingine

Lakini pia wanawake wengine huwa ni ving'ang'anizi sana, yawezekana mumeo aling'ang'aniwa mpaka kikaeleweka, hebu umeshawahi kuona mwanamke anavyomlilia ampendaye? hakika huwa ni baraa isiyokuwa na mfano,ukikataa basi atayalembua hayo macho huku michozi ikimtiririka, hoooo!!!!!! mwishowe mwanaume anaona bora aondoe lile zogo, naomba umsamehe sana kwani yeye binafsi hata kwa sasa anayajutia aliyoyafanya.
 
Your husband ana katatizo kadogo sana! Yaani akiwa na pressure inaamka akila tundi na wewe na siyo mwingine? Labda kuna tatizo lingine ambalo hujalisema. Lakini hata hivyo sioni sababu ya yeye kutumia kitanda chenu!
 
Kwa kifupi huyo mwanaume hakutaki kama alifikia hatua ya kulala na mwanamke ndani ya nyumba yenu na kama hiyo haitoshi kitanadani kwenu mmmmh! hiyo haijakaa vizuri AKUFUKUZAE............... green right
 
Pole sana dada

Nataka kukuhakikishia kuwa hilo lililokufika wewe wapo wenzio waliofikwa na mkasa kama huo pia. Na pengine mkasa mkubwa zaidi yako kwa mfano mumeo kazaa na ndugu yako toka nitoke. Ni kweli fumanizi ya kushuhudia kwa macho inauma. Nakushauri uwe mvumilivu na mtulivu kwa sasa. Kwa kuwa huyo mwanamke si ndugu yako huna sababu ya kuvunja ndoa yako. Mumeo kajidhalilisha mwenyewe, kajiondolea uaminifu kwako, kapunguza mapenzi yako kwake.

Usimpe nafasi mwanamke mwenzako kukuchukulia mume kirahisi. Rudi nyumbani kwako. kama hali ya uchumi inaruhusu badilisha chumba chako kuanzia kitanda, mapazia hadi mashuka, na hata rangi ya chumba. Huyo bwana akitaka amfuate huyo hawara yake huko nje lakini siyo ndani ya nyumba yako.

Mwisho, usimpe tunda kirahisi bila kujua afya zenu. Na ikithibitika ni salama mpe adhabu ya kondom mpaka atakapokuhakikishia usalama wako na uridhike na hilo.
 
Back
Top Bottom