Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
SAKATA LENYEWE NI HIVI:
Juzi nilipata safari ya peke yangu! Niliporudi nilimkuta NO! niliwafumania mume huyo chumbani kwetu akiwa na mwanamke kitandani kwetu...(you know what they were doing)!!!
Ni kama nilipatwa na shoti ya umeme kwa dakika kadhaa...nilichoweza kufanya ni kutoa simu yangu ya kiganjani na kuwapiga picha kadhaa. Nikaondoka kabisa maeneo yale na kwa kweli mpaka sasa ninalala kwa ndugu zangu!
Sijui nitaanzaje kulala tena ktk kile kitanda chetu na nihisi raha kama zamani!
Huwa ninaenda kuchukua vifaa ninavyohitaji, na nilimuuliza kwa nini anafanya vile, anajibu oo eti bahati mbaya shetani kanipitia!!! kakupitia in our bed!!!
Wana JF, uamuzi ninaoona unafaa ni kumtaliki, kwa sababu amekuwa akinidangaya kwa kisingizio kuwa eti ana presha!
Lkn kabla sijachukua hatua hii nimeona bora nipate ushauri wenu!
Please!!!
Kwa kweli hili jambo linauma sana na linaweza kukufanya na wewe upate hio BP kama yeye usipokuwa mwangalifu.
Hapa nafikiri ndio "end of the road" katika mapenzi yenu. Hili halihitaji mjadala hata kama wewe ndie unamtegemea yeye ukizingatia kwamba kwa sasa unaishi kwa nduguzo na hii inaonesha kwamba hata wewe huna mahala pako na hili ni tatizo kubwa kwenu ninyi wanawake.
Nasema hivyo kwa sababu kama wewe ndie unamtegema yeye basi anafanya hivyo akitegema kwamba wewe hautakuwa na mahala pa kujisitiri na mwisho utarudi kwake.
Pia kitendo cha kuwa unarudirudi pale na kumuuliza kwamba kwa nini alifanya hivyo naona hapa unafanya mchezo wa baba na mama. Ondoa nguo zako na kila kitu chako na endapo mungu amekupangia kupata mume mtaeelewana basi utapata.
Mwisho napenda kuona unajitahidi uwe na angalau kachumba ka kupanga na uchakarike na shughuli zilizo halali ili uweze kuishi kwa raha na jaribu kumsahau kabisa huyu jamaa.
Mimi nikiwa mwanamme sikushauri ili unifuate nisemayo bali nakupa mwanga wa kufikiri na kujua kuwa unaweza uka-stand kwa your own feet na kuendela na maisha yako, ikitokea Mungu kakupa pande utapat mwanamme mzuri kwako.