Kitanzi cha gawio

Unapofuta shirika as if hakuna watu wenye uwezo, who loses...
 
Unapofuta shirika as if hakuna watu wa wenye uwezo, who loses...
Wao ndio wanatia hasara kuanzia CEO hadi messenger

Shirika linakabidhiwa private sector wanaojua kuzalisha kwa faida na kulipa kodi kuliko hao mabwege wategemea ruzuku ambao gharama zote zinategemea ruzuku ya Serikali au tozo

Sio kitu kikubwa .They can't unawapa Private sector local or international

Heri Upokee kodi kuliko kodi kiduchu unazopata uwapelekee wao

Kinana kaongea kitu kizito mno lakini wasomi wetu wana dharau sana kwa wanasiasa

Mwanasiasa ni chief administrative officer wa fani zote za public sector ndio maana heads wote wa public sector huchaguliwa na kuapishwa na Raisi hata kama Raisi ni darasa la Saba au form four failure
 
Tatizo ni usimamizi, mtaji, teknoloji au nini..nadhani nature ya tatizo ndio inaelekeza njia sahihi ya kurekebisha tatizo, kubinafsisha shirika wakati tatizo ni usimamizi inakuwa bora hata ungeliacha shirika km lilivyo, huwezi kuuza shirika kwa tatizo la usimamizi mbaya..tafuta wasimamizi wazuri shirika litafanya vizuri.
 
Mkuu Magufuli watamkosoa sana lakini kukosoa Magufuli kuna maeneo unahitaji maproffessor zaidi ya mia wa fani tofauti ku challenge

Kuna maeneo alikuwa mjinga hasa na kichwani hazimo

Akili yake ilikuwa kama network ya mtandao wa simu inaingia na kutoka na kutokuweko hewani.Lakini network ikidaka anashusha vitu vya uhakika ikiwemo hili la kudai Non Profit Government Companies watoe gawio kwa Serikali sababu aliwaona hawajui maana ya Non Profit government Company au organisation!!
 
Lakini shirika si mali ya CEO na wafanyakazi..wao hawana cha kupoteza, watatafuta ajira nyingine.
 
TTCL kushindwa kutoa gawio ni uzembe. Mbona makampuni kama Halotel, Airtel nk yameikuta na yanaendelea vizuri tu?
Parastatal kutengeneza faida siyo rahisi kihivyo. Wana cost structure kubwa ambayo private hawana, wana wafanyakazi wengi kwenye payroll. As well as bureaucracy kwenye maamuzi ni ndefu kuweza kuleta efficiency na profitability.
 
Tanesco. Mfano kulikuwa shida kubwa ya wasimamizi. Serikali ikampeleka Dr Idris Rashid mchumi aliyekuwa Governor wa benki kuu sio engineer wa umeme aka turn around Tanesco

Kulipa bili tu tulikuwa tunaenda kushinda siku nzima Tanesco kulipia bili ya elfu mbili!!

Sasa hao waliopo wanashindwa nini kufanya aliyofanya DR Idris Rashidi mkurugenzi mkuu wa Tanesco ambaye hajawahi kanyaga hata Veta kusoma umeme wakati toka uhuru Tanesco ilikuwa na mainjinia wa Umeme hadi wenye PhD kuanzia Tanesco hadi wizarani?
 
Parastatal kutengeneza faida siyo rahisi kihivyo. Wana cost structure kubwa ambayo private hawana, wana wafanyakazi wengi kwenye payroll. As well as bureaucracy kwenye maamuzi ni ndefu kuweza kuleta efficiency na profitability.
Faida/profitability ipi? Cash..km ni cash, kwa nini yaandikishwe km non profit entities..sidhani km faida inapaswa iwe interms of cash.
 
Unaweza ukaweka hapa annual accounts za BICO ili tuone kweli kama walikuwa na uwezo wa kutoa gawio. Sio kila kitu unachoambiwa ni SBU (Strategic Business Unit) kina productivity.

Vitu vingine viko kupunguza gharama tu ya kuchonga vipuli kwenye private sector
 
Walimpataje Dr. Idris..dawa ni ku-liberalize recruitment process kwa Bodi na management ya mashirika.
 
Faida/profitability ipi? Cash..km ni cash, kwa nini yaandikishwe km non profit entities..sidhani km faida inapaswa iwe interms of cash.
Mashirika ya Umma yapo kwa mujibu wa Public Corporation Act ya 1967. Wala siyo Non Profit Organisation. Kasome hiyo Act kwanza ndiyo uulize swali lako vizuri.
 
Parastatal kutengeneza faida siyo rahisi kihivyo. Wana cost structure kubwa ambayo private hawana, wana wafanyakazi wengi kwenye payroll. As well as bureaucracy kwenye maamuzi ni ndefu kuweza kuleta efficiency na profitability.
Uongo

Mfano TTCL nini kiliwashinda wasiingie solo la Simu za mkononi wakati ilikuwa kampuni ya simu pekee Tanzania?

Nini kikiwadanya UDA walishika solo lote la abiria Dar es salaam wapite na daladala kupata faida na wao wafe?

Nini kiliwafanya National Milling Corporation wauza unga wote wa mahindi,ngano nk wafe washindwe kujiendesha kibiashara wakati walikuwa wao peke yao sokoni hadi wabinafsishwe Bakheresa awe Bilionea kwa bidhaa zile zile za National Milling ?
TEMESA kivuko cha kigamboni wameshindwa kuendesha pamoja na kuwa soko liko kibao hadi kupewa Bakheresa!! Wasomi Temesa qako kibao lakini hopeless
 
Marehemu kafa na chake pigana upate chako, Mashirika yalijiendesha kwa hasara lakini lita moja ya mafuta ya kula ilikuwa 3500, Sabuni B29 ilikuwa 300, Mchele kg ilikuwa 1000 Hadi 1300, Diesel na Petrol sitasema chochote, kubadilisha gesi ilikuwa 21000 Hadi 22000, Watanzania ni mashuuhuda wa mengi.
 
Mashirika ya Umma yapo kwa mujibu wa Public Corporation Act ya 1967. Wala siyo Non Profit Organisation. Kasome hiyo Act kwanza ndiyo uulize swali lako vizuri.
Kuna wengine wanajidai hivyo kuwa wao kazi yao kutoa huduma sio kuzalisha faida
Kuwa ok tulianzishwa kwa sheria lakini Sisi sio Profit Making organisations wa kutoa gawio kwa Serikali
 
Dawa ni kushindanisha watu nafasi zote za kuongoza mashirika, mtu ahojiwe strategy yake kwa shirika husika ili apimwe kwa hayo..that's all.

Anachokifanya ni kujifurahisha tuu, otherwise tuaminishwe kuwa ni magazeti ya udaku
 
Mashirika ya Umma yapo kwa mujibu wa Public Corporation Act ya 1967. Wala siyo Non Profit Organisation. Kasome hiyo Act kwanza ndiyo uulize swali lako vizuri.
Ok naondoa hiyo non profit organisation, faida/profitability unamaanisha cash..? Mfano hapo nyuma uliwahi sikia shirika km Air Tanzania au hata ATCL ya sasa wamepata faida unayosema?
 
Lakini shirika si mali ya CEO na wafanyakazi..wao hawana cha kupoteza, watatafuta ajira nyingine.
Uendeshaji shirika ni team work

Sio kazi ya CEO pekee

Usawa huu wa Ukosefu wa ajira shirika likifutwa kila mfanyakazi atajinyea kuanzia CEO hadi messenger
Nani yuko tayari kuchukua mfanyakazi toka Non performing government
Company? Au Private Company?thubutu!!!

Hata mimi kwenye genge langu la kuuza nyanya na vitunguu sikuajiri hata uwe na digriii zote duniani kutoka best universities in the world
 
Hicho alichosema Rais nina mashaka nacho, tafsiri ni nyingi sana..kwamba pamoja na kudanganya kutoa gawio feki, hawa CEO bado wanafaa, kwamba yeye Rais ni observer wa kutuambia wananchi kasoro za mashirika lakini yeye hahusiki na lolote whether yafanye udanganyifu, au hata yafe ni sawa tu..mishahara na stahiki zote kwa watumishi wa mashirika haya yasiyo na tija kwa nchi yeye haimuhusu hata km ni kodi za wananchi zinalipwa kwa watumishi wasio na faida kwetu..vinginevyo asingetoa hii statement.
 
Unapofuta shirika as if hakuna watu wenye uwezo, who loses...
Wao ndio wanatia hasara kuanzia CEO hadi messenger ndio maan linapata loss

Shirika linakabidhiwa private sector wanaojua kuzalisha kwa faida na kulipa kodi kuliko hao mabwege wategemea ruzuku ambao gharama zote zinategemea ruzuku ya Serikali au tozo

Sio kitu kikubwa .They can't unawapa Private sector local or international

Heri Upokee kodi kuliko kodi kiduchu unazopata uwapelekee wao

Kinana kaongea kitu kizito mno lakini wasomi wetu wana dharau sana kwa wanasiasa

Mwanasiasa ni chief administrative officer wa fani zote za public sector ndio maana heads wote wa public sector huchaguliwa na kuapishwa na Raisi hata kama Raisi ni darasa la Saba au form four failure au kasoma madrasa tu hana elimu dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…