Kitanzi kimepitwa na wakati kwanini tusitumie technology hii

Kitanzi kimepitwa na wakati kwanini tusitumie technology hii

kwa apa nchini hii adhabu haipo, wanaishiaga kubwabwaja tu mahakaman kisha mtuhumiwa anarud uraian
 
Adhabu ya kifo pekee inayotakiwa kubaki ni ya sindano ya sumu inayomfanya anayehukumiwa kusinzia na kupitiliza. Nchi zenye option ya kuchagua wengi huchagua sumu.

Ama ziwepo options zaidi ila sumu isikose. Hiyo ya kiti cha umeme ni ya zamani pia
Mnaposema "ya kizamani" mnamaanisha nini? Kwamba siku hizi haiui vizuri au?
 
Mauaji hayawezi kuisha Duniani lakini hilo haizuii wauaji pia kuuawa.

Adhabu ya kifo haizuii watu wasiendelee kuua watu ila hakuna sababu ya kuendelea kuwapa nafasi wauaji ya kuendelea kuishi wakati wao hawakujali maisha ya watu wengine.

Hatuwezi kuendelea kulipia mauaji chakula na ulinzi gerezani, waendelee kuishi. Hiyo hela inaweza kutumika kusaidia jamii ama matatizo mengine katika jamii, jamii ina changamoto nyingi sana zinazohitaji msaada, sio wauaji. Akiua, auwawe.

Watu ambao hawakujali maisha ya watu wengine, hatuna sababu ya kujali maisha yao.

Unaweza kukisia au kuwa na taarifa za idadi ya walionyongwa tokea tupate uhuru? Umejikita kwenye gharama za kuwahudumia hao wauaji ukisisitiza kunyongwa inapunguza hizo gharama. Hawanyongwi Kwa kasi kiasi hicho.
 
Mnaposema "ya kizamani" mnamaanisha nini? Kwamba siku hizi haiui vizuri au?
Inaua kwa kutesa. Lengo la kuhukumu kunyonga sio kumkomoa mkosaji ni kuzuia watu wengine kufanya kama yeye. Mtu anaua mke wake na mtoto kisa mke kagoma mume asiongeze mke wa pili, bila adhabu stahiki yatajirudia sana
 
Kuna adhabu isiyotesa? Mimi nadhani hayo mateso ni sehemu ya adhabu na inafaa.

Jambazi anaekata watu mapanga, anatakiwa apitie mateso pia. Kumuua kwa sumu, ni kumpa starehe ambayo hastahili.
 
Kuna adhabu isiyotesa? Mimi nadhani hayo mateso ni sehemu ya adhabu na inafaa.

Jambazi anaekata watu mapanga, anatakiwa apitie mateso pia. Kumuua kwa sumu, ni kumpa starehe ambayo hastahili.
Sheria haifanyi hivyo. Mtu ni gaidi kalipua bomu limeua watu 20 utafanyaje ili kufananisha madhara aliyoleta, au utaua familia yake kisa ameua watu wengi.

Mara nyingi huwezi lipiza madhara yaliyofanywa na mhukumiwa. Hukumu sio mateso
 
We jamaa hivi vitu havina uhusiano. Imagine upo kazini unapigiwa simu kuna kiumbe kaua mtoto wako

Ningekua kwenye position ya kusign utekelezaji wa hii hukumu . Ningewala vichwa sana
Ubaya wa adhabu ya kifo nauona tu pale adhabu hii pengine inapomwangukia mtu asiye na hatia I believe hili huwa linatokea ila kwa jitu linaloua kwa kudhamiria hakuna adhabu nyingine impasayo hayawani kama huyu isipokuwa adhabu ya kifo tu.
 
Hoja ya kusema adhabu ya kifo iondolewe eti iondolewe kwa kuwa haipunguzi makosa ya mauaji naona ni hoja dhaifu sheria haisemi kwamba lengo lake ni kupunguza makosa ila imesema ukifanya hivi utaadhibiwa hivi hii maana yake usifanye ambavyo imekukataza naamini hakuna mhalifu anayetegemea kukamatwa watu wanafanya uhalifu wakiamini hawatakuja kutiwa mikononi mwa dola addhabu ibaki palepale makosa kutopungua haiwezi kuwa sababu ya kuindoa sheria kwanini ubaki hai wakati unaua wenzako
 
Sheria haifanyi hivyo. Mtu ni gaidi kalipua bomu limeua watu 20 utafanyaje ili kufananisha madhara aliyoleta, au utaua familia yake kisa ameua watu wengi.

Mara nyingi huwezi lipiza madhara yaliyofanywa na mhukumiwa. Hukumu sio mateso
Yes, hatuwezi kulipiza. Lakini pia hatuwezi kuwahurumia!

Wanyongwe mpaka kufa!
 
Pamoja na uwepo wa hiyo adhabu, wauaji wameacha kutoa roho za watu?
Wakikujibu pls nipe Nami taarifa,adhabu ya kifo nitaifuta within 10mins ya Urais wangu including copral punishment kwa wanafunzi ,futilia mbali huu ni ujima, unyama na ukatili
 
Back
Top Bottom