Huu ni uswahili swahili (whatever the hell that means) tu na elimu ndogo. Huwezi kumkuta mtu aliyeelimika kama Mama Migiro akimfanyia bintiye huu ujinga ujinga. Hata wanawake wale wanaofagilia huu upuuzi ukiangalia elimu zao ndi ndogo sana.
Nyambaaaf kabisa...
Kama alivyosema SteveD, haya mambo yameya-dilute mno hata hayaleti maana, yanaelekea kwenye ukahaba zaidi kuliko ilivyotakiwa.
Mambo haya kwa waliopitia ilikuwa ni elimu ya muda mrefu, ijumuishayo maisha kwa ujumla.
Ngoja nitoboe sire kidogo:
Mafunzo ya jamii yalitolewa kila shule zinapofungwa, watoto wa walipelekwa makambini mbali na kijijini, pia wakiume walipelekwa kwao pia.
unyago wa kwanya tunaita msondo-hutu ni tubinti ambatyo hatujapevuka, elimu yao ni kuwaandaa na maisha ya kupevuka. Kuwaandaa kuupokea mpevuko.
Unyago wa pili ukishapevuka: hii ni kubwa kwa sababu binti kama unajeuri ndivyo utakavyowekwa muda mwingi mpaka urekebishike. Na wamama wanamsubiri sana binti kwenye kipindi hiki. Hivyo kila binti alijitunza na kuheshimu kila mkubwa ili tu siku yake ikifika yasije mfika. Zawadi zilitegemea pia jinsi binti unavyojitunza, heshima n.k.
Wazazi pia ilikuwa ni fahari kama binti unafikia muda huo ungali msichana(yaani bikra). I miss this education. maendeleo yameharibu taratibu zetu, siku hizi tunafunzwa na TV.
Unyago wa ndoa: huu ndiyo tunamwandaa mwali kimaisha ya ndao na kumkaribisha rasmi kundini. Atapewa A B C za jinsi ya ku-behave kwa mumewe, na in-laws.
Unyago wa mimba: bila kuchoka jamii ilimfundisha mwadada anayetarajia kupata mtoto ajitunze vipi, a-control vipi mabadiriko yanayotokea mwilini mwake n.k. bila kuleta mtafaruku kwenye ndoa yake.
kwa upande wa wanaume nao vilevile.
Sasa leo mnakutana ukumbini kwa masaa matatu mmeshamfunda mwali????? Jamani? anyway...