Kitendawili cha BAKWATA na Serikali BAKWATA na Waislam 1968 - 2024

Kitendawili cha BAKWATA na Serikali BAKWATA na Waislam 1968 - 2024

Inside 10,
Angalia kitabu hicho hapo chini kitakusaidia:

View attachment 3154178
Ok leo nimekuelewa kimbe unaposema kanisa, unamanisha kanisa katoliki Tanzania...
Huwa unanitatiza nashindwa kuelewa ni kkkt, anglican, sabato, moravian n.k

Swali la pili.. kuna sehemu umesema bakwata wakapewa pesa na kanisa.. sasa aliyetoa hiyo pesa ni nani?! Askofu, padri ? Tupe ushahidi
 
Ok leo nimekuelewa kimbe unaposema kanisa, unamanisha kanisa katoliki Tanzania...
Huwa unanitatiza nashindwa kuelewa ni kkkt, anglican, sabato, moravian n.k

Swali la pili.. kuna sehemu umesema bakwata wakapewa pesa na kanisa.. sasa aliyetoa hiyo pesa ni nani?! Askofu, padri ? Tupe ushahidi
Inside 10,
Mimi huwa sijiingizi katika mabishano.

Nilikuwapo katika mkutano ule pale Diamond Jubilee Hall.

Nimeueleza wote katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Inside 10,
Mimi huwa sijiingizi katika mabishano.

Nilikuwapo katika mkutano ule pale Diamond Jubilee Hall.

Nimeueleza wote katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kupenda kwangu kujua au kuuliza swali nikuoenda mabishano?!
Basi kama ni hivyo tuishie hapa, na kama hutaki maswali uwe unaenda kuwamezesha hizi stori hukohuko mtoro, kichangani n.k.
 
Ndio, huoni mpaka leo tunaishi kama ndugu
Sylver5,
Makala ndefu lakini jitahidi uisome yote:

MNA NINI NDANI YA KITABU CHA SHEIKH PONDA?
Ili kitabu kiwe kitabu lazima kiwe na elimu mpya yaani ile ambayo jamii haijui.
Hii elimu mpya ndiyo roho, moyo na maisha ya kitabu kwani kitabu kina maisha na kifo kama binadamu.

Kitabu kikikosa vitu hivyo kinaweza kufa mapema au kikafa katika kuzaliwa yaani kitabu kinaingia katika mzunguko tayari kisha kufa.

Katika miaka ya hivi karibuni kuanzia mwaka wa 2010 Tanzania imeshuhudia kuchapwa vitabu muhimu sana vya historia.

Kitabu cha kwanza kilikuwa, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' cha Dr. Harith Ghassany (2010), ''Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar,'' cha Hashil Seif (2017), ''Maisha Yangu Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?'' Khamis Abdullah Ameir (2022).

Hivi ni vitabu kuhusu historia ya Zanzibar.

Nashukuru kuwa nimehusika katika vitabu hivyo vyote hapo juu kwa njia moja au nyingine.

Tanzania Bara waandishi wa vitabu vilivyochapwa kuhusu historia ya Tanganyika ni ''My Life My Purpose,'' cha Benjamin William Mkapa (2019), ''Julius Nyerere A Biography,'' kitabu kilichaondikwa na Issa G. Shivji, Saida Yahya Othman na Ngwa'nza Kamata (2021) kuhusu maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; na kitabu cha maisha ya Ali Hassan Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu,'' (2021).

Vitabu hivi sikuhusika moja kwa moja ukikitoa kitabu cha Julius Nyerere.
Lakini mengi katika vitabu hivyo nikayajua kiasi cha kuweza kufahamu wapi kalamu haikuandika sawasawa kwa sababu hii au ile.

Vitabu vyote hivi vinahusu historia ya Tanzania na serikali yake. ambayo marais hawa waliongoza.

Kwa bahati mbaya sana waandishi wa vitabu hivi wamejifanyia uhariri mkubwa katika tatizo la Waislam kama kundi la raia ambayo serikali imekuwa kama vile inawatazama kwa jicho lililojaa hofu.

Ukisoma vitabu hivi vyote unatoka na picha ya kuwa Tanzania ni nchi yenye utulivu mkubwa kama wanavyosema watawala walio madarakani na ndiyo walioshika serikali, Tanzania ni kisiwa cha amani.

Hivi ndiyo alivyosema Benjamin William Mkapa na Ali Hassan Mwinyi kadhalika.

Mwalimu Nyerere yeye hakuandika kitabu cha maisha yake.

Matatizo haya ya ubaguzi wa dini kwa hakika yalianza wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza Mwalimu akiwa kwanza Waziri Mkuu wa Tanganyika, kisha Rais wa Tanganyika na mwishowe Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya kuaga aliyotoa Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985 anasema yeye aliondoa upogo baina ya Waislam na Wakristo.

Kwa hiyo marais wote waliofuata baada yake ndiyo kusema wamerithi nchi iliyokuwa haina ubaguzi kwa misingi ya dini.

Kwa ajili hii basi Marais hawa waliokuja baada yake hawakuwa na cha kurekebisha.

Hapa ndipo kinapoingia kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''
Sheikh Ponda anaingia vipi katika orodha hii ya vitabu vinavyowahusu marais watatu waliotawala Tanzania?

Kitabu cha Sheikh Ponda kinapingana na vitabu vyote vitatu vya marais hawa kwa kutoa picha halisi ya ukweli ulivyo toka uhuru upatikane.

Mbali ya maisha yake mwenyewe katika kupigania haki za Waislam, Sheikh Ponda ndani ya kitabu hiki chake anaeleza namna gani taasisi za serikali zinavyofanyakazi pale wanapokabiliana na Waislam na pale wanaposhughulika na raia wengine.

Ukizisoma kurasa hizi Sheikh Ponda anavyoeleza yaliyomfika kwa kupigania haki za Waislam yatakutoka machozi.

Mwanzo wa kitabu Sheikh Ponda anaeleza juhudi za Waislam katika kupata elimu na anahitiilmisha kwa kuweka wazi kwa ushahidi namna Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilivyokuwa linahujumu juhudi hizi.

Sheikh Ponda anaeleza katika kitabu chake juhudi zilizotumika kupata ushahidi wa dhulma hii na kufikisha ushahidi kwa vyombo vinavyohusika ili haki itendeke.

Baada ya kuona juhudi za Waislam zinapuuzwa Sheikh Ponda aliitisha maandamano ambayo serikali iliyapiga marufuku.
Sheikh Ponda hakukubali.

Katika Msikiti wa Kichangani baada ya Sala ya Ijumaa Sheikh Ponda alisimama kuzungumza na Waislam kuhusu umuhimu wa kutoa hofu katika nyoyo zao na kuwataka waanandamane katika maandamano ambayo yeye atakuwa mbele kuyaongoza.

Nilikuwapo hapo msikitini siku ile nimekaa kibla chini ya miguu ya Sheikh Ponda napiga picha na kurekodi yote aliyokuwa anasema yeye akiwa kasimama mbele yangu.

Alipomaliza kuzungumza na Waislam Sheikh Ponda aligeuka akaangalia kibla kisha akanyanyua mikono yake juu kuomba dua.

Kama siku ile mwaka wa 1998 Sheikh Ponda alipotusalisha Msikiti wa Mwembechai Sala ya Maghrib akawaliza Waislam ndani ya sala hali ilirijudia Msikiti wa Kichangani mwaka wa 2012.

Hii ilikuwa miaka 14 baada ya Mwembechai.
Waislam wake kwa waume walitokwa na machozi.

Waislam waliandamana kama vile askari waliokuwa nje ya msikiti na silaha za kutisha na mavazi ya mapambano hawapo.

Askari wale hawakuwashambulia Waislam na maandamano yakafanyika na kama aivyowaahidi Waislam Sheikh Ponda alikuwa mbele akiyaongoza maandamano.

Huyu ndiye Sheikh Ponda aliyenyanyua kalamu kueleza hali ya nchi yetu ilivyo.
Kitabu hiki ni muhimu kwa kila Mtazania anaeitakia nchi yetu amani ya kweli kukisoma.

1731840327639.png
 
Kupenda kwangu kujua au kuuliza swali nikuoenda mabishano?!
Basi kama ni hivyo tuishie hapa, na kama hutaki maswali uwe unaenda kuwamezesha hizi stori hukohuko mtoro, kichangani n.k.
Inside 10,
Unataka ushahidi.
Ushahidi una sheria zake (Law of Evidence).

Mimi siwezi kukidhi masharti yake.
Mimi sizungumzi Msikti wa Mtoro.

Mimi nazungumza Northwestern University, Chicago.
Hawa ndiyo wanaongoza ulimwenguni katika African History.

Mimi nazungumza University of Iowa.

Nazungumza University of Johannesburg, University of Ibadan, Kenyatta University, Dar es Salaam University, nazungumza Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani.

Mimi nazungumza Voice of America (VoA) Washington.
Nimezungumza kwingi duniani kwa mwaliko watu wakitaka kunisikiliza.

Mimi sizungumzi katika misikiti.
Hii jeuri kwangu ya nini?
''... uwe unaenda kuwamezesha hizi stori hukohuko mtoro, kichangani n.k.
Hunijui.
Jitahidi angalau unifahamu kidogo:

1731840846046.jpeg

1731840935700.jpeg

VoA Washington DC
 
Nilikuwapo hapo msikitini siku ile nimekaa kibla chini ya miguu ya Sheikh Ponda napiga picha na kurekodi yote aliyokuwa anasema yeye akiwa kasimama mbele yangu.

Alipomaliza kuzungumza na Waislam Sheikh Ponda aligeuka akaangalia kibla kisha akanyanyua mikono yake juu kuomba dua.
Mzee wetu hapa umeandika kwa hisia kali sana
 
Kina...
Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu zilizosheheni taarifa nyingi za Julius Nyerere.

Maktaba ya kwanza ni ya Dr Salim Ahmed Salim, Mohamed Said na Brig.General Hashim Mbita.

Ndiyo sababu unaona wengi wanakuja kwangu kwa mahojiano.

Lakini mengi niliyonayo nimeyapata kutoka Nyaraka za Sykes.

Haya yapo katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere (Nyerere Biography).
nitafika mzimuni ninunue hivyo vitabu
 
Back
Top Bottom