Kitendawili cha mtandao wa internet ambacho mpaka leo kimeshindikana kuteguliwa

Kitendawili cha mtandao wa internet ambacho mpaka leo kimeshindikana kuteguliwa

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Katika mambo ambayo mpaka leo yameshindwa kujulikana, ni nani allitengeza sarafu ya Bitcoin ambaye alijipachika jina la Satoshi Nakamoto.

Watu wengi wamekuwa wakihisiwa lakini mwisho inagundulika siyo wao. Jambo la kustaajabisha, jamaa mara ya mwisho alilog off 2012 na hakuwahi kuonekana tena. Ila dunia inafurahia uvumbuzi wake wake ambao mpaka leo hakuna aliyefanikiwa kuuhack.

Bitcoin network imekuwa undefeated, na imetengeneza teknolojia mipya ya kutengeneza mifumo ya kifedha na mikataba ya kidijitali. Katika watu wengi waliotajwa, kuna mtu mmoja ana kila dalili ya kuwa inawezekana ndiye aliyetengeneza bitcoin, naye ni Paul Le Roux.

Huyu ni mzailwa wa zimbabwe mwaka 1976, ambapo familia yake ilihamia afrika kusini. Baadae alisoma mambo ya computer programming, kisha akahamia Uingereza ambapo aliajiliwa kwenye kampuni ya kutengeneza mifumo ya encryption.

Akiwa hapo aliunda program inayojulikana kama E4M yani Encryption for Masses. Hii ilikuwa ni program ambayo waaharifu na magaidi walipenda kuitumia, ilikuwa inafunga kuigniliwa mawasiliano kwa kila namna iwe email, simu, web access, na kila kitu. CIA walipata tabu sana kupenetrated system iliyolindwa na program hii.

Baadae aliona hawezi kuwa tajiri akahamia Manila, Ufilipino, ambapo alitengeneza call center na kuanzisha mtandao wa kuuza prescribtion drugs kwa Wamarekani. Kwa siku alikuwa anaprocess order zaidi ya 300. Ilikuwa ni biashara haramu ila alikuwa akiingiza pesa ndefu na hakuna aliyeweza kumtrack maana computer yake na mtandao wake wa mauzo alikuwa kautengenezea mfumo wa wa encryption wa hali ya juu.

Akaona pesa haitoshi akaanza uajiri wanajeshi wastaafu wa marekani na Uingereza kuwa genge lake. Jamaa kawa na pesa nyingi akaamua kuwa anawtuma vijana wake wanaenda Hongkng wananunua dhahabu by cash wanaziweka safe house.

Akaona hiyo haitoshi akaenda akatuma mwakilishi Iran akaingia nao mkataba wa kuwaletea silaha, pamoja na kuwauzia formula ya kutengeneza mabomu ya kutungulia misafara ya wamarekani huko Iraq. Hiyo haitoshi akwa na kundi la hit mens, polisi na wanasiasa wa Ufilipino walikuwa kwenye pay roll yake. Watu wengi waalifu walimjua tu kwa jina la Big Boss.

Akaanza uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya Asia. Akatuma vijana wake waka recruit vijana na kujenga military base Pwani ya somalia itakayokuwa kama military barracks, ikiwa na landing strip. Muda wote huo CIA hawakuwahi msikia mpaka ilipotoka report ya UN ndipo CIA wakaanza mfuatilia mpaka kuja kumnasa lIberia mwaka 2012.

Kwanini inasadikika kuwa ndiye mtengenezaji wa btcoin.

1. Ana ufahamu mkubwa wa coding na encryption, hata maka anakamatwa CIA walishindwa kupenetrate mawasilaino yake iwe ya simu au computer, aliyewasaidia ni kijana wake aliyekuwa amemweka SOmalia kama kiongozi baadae akahisi anamwibia akatuma mtu amuue kijana machale yakamcheza akakimbia Na kwenda mafichoni. Huyu ndiye alikuja shirikiana na CIA kwa kuwapa copies za encryption zake na kuwaunga naye maan baadae aliwasiliana na boss wake akimwambia kuwa hakuwa anamwibia halafu akampa deal la kusambaza dawa za wacolumbia kumbe wacolumbia hao walikuwa ndiyo CIA.

2. Post za Satoshi na maneno na uandishi wake wa kingereza cha ki British ni sawa na wa Paul.

3. Emails alizokuwa aiwatumia developers wengine uandishi wake ni sawa na emails nyingine alizokuwa akizituma kwa vijana wake.

4. Satoshi toka apotee hajwahi kuonekana na inasadikika alimine 1 million bitcoin ambazo mpaka leo hazijatumika, huu a ndiyo muda ambao Paul naye alikamatwa na mpaka leo yuko gerezani Marekani.

satoshi.jpg

satoshi.jpg
 
Duhh ukisikia akili kubwa ndiyo hii Sasa

Sent by IPhone
 
nazani real satoshi huenda alikuwa ni hal finney(R.I.P),,
Huyu jamaa at least anafanania na satoshi na yeye ndio mtu wa kwanza kupokea bitcoin toka kwa satoshi...
 
Lakini pia inasemekena Satishi Nakamoto mwaka 2010 alikabidhi kila kitu kwa GAVIN ANDRESEN mwanzilishi wa 3D graphics na mtaalam wa programu za virtual reality, hii ilikuwa ni baada ya kukamilisha zoezi zima la uundaji wa bitcoin.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japokuwa sekta nyingi za kifedha duniani zimeonyesha kuvutiwa na mapinduzi haya ya kiteknolojia bado zina mashaka kuhusu utekelezaji wa utumiaji wa sarafu za aina hii. Mnamo mwaka 2014 tulishuhudia benki kuu ya Australia ikifunga akanti zote zilizotumika katika ununuaji au uuzaji wa bitcoin.

Kati ya miaka ya 2013 na 2014 mamlaka kuu ya benki za ulaya na mamlaka ya udhibiti wa taasisi za kifedha nchini humo zikitoa tahadhari kuhusu hatari iliyopo katika uwekezaji wa sarafu hii ya bitcoin uliokuwa ukiendelea.

Ndani ya mwaka huo wa 2013 pia Forbes ilitaja uwekezaji katika bitcoin kama uwekezaji bora wa mwaka huo wakati ilipofika 2014 kituo kikubwa cha habari cha Blomberg kiliutaja uwekezaji katika bitcoin kama uwekezaji mbaya kuliko uwekezaji wowote duniani.

Ilipofika 2015 meza ya habari ya kituo cha Blomberg ilishuhudia kufunikwa kwa habari zilizohusu bitcoin tu katika upande wa habari za kifedha na kiuchumi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa bitincharts.com (tovuti inayoonyesha ukuaji wa bitcoin) hadi kufikia mwaka 2017 kulikuwa na bitcoin wallet(mifuko maalumu ya kimtandao inayotumika kuhifadhi bitcoin) ipatayo 9,272 yenye bitcoin zenye thamani zaidi ya dola za kimarekani million 1.

Wapo pia mabepari kama Peter Thiel ambao waliwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 3 ili kusaidia miradi na sekta mbalimbali zilizohusika na maendeleo ya sarafu hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bitcoin network tu ndiyo haijawahi kuwa hacked wengine walishakuwa hacked.

Ila cryptocurrency nayo ina mambo, mpaka leo mwanamama mwanzilishi wa one coin hajulikani yuko wapi na scam yake, aliondoka na mabilion ya ela za watu.

Halafu wakati iko kwenye peak nilipewa kazi na client flani niandike article kuhusu one coin japo sikujua ilienda kuwa posted wapi
 
Hapo kuna watu wanatafutwa, uzuri huu utapeli unawakamata sana wasomi, mzee kastaafu kapata milioni 80 anaambiwa wekeza kwenye bitcoin, mfumo wa kisasa utapata Mara kumi ndani ya miezi mitatu, wamekufa na presha. Hizi bitclub, aws mining na wenzao ni janga sugu la wazawa
 
Hakika leo ndo nimeamini hakuna mwenye wazo jipya la peke yake!!

Yaani from nowhere, huku nikiwa sijawahi kuwaza jambo hilo hata mara moja maishani mwangu, mara wazo likapita tu kichwani mwangu na kuniambia "Hey, listen... we ukiona mambo hayaeleweki eleweki basi, basi jua CIA are behind everything! We unadhani CIA wange-finance vp black ops duniani bila kuwa na confidential means za ku-finance hizo funding"

Nikaona si ajabu wapo waliopata kufikiria kama mimi, na ndipo nikaamua ku-Google "Did CIA Invent Bitcoin?"

Page ya kwanza tu ya search result nikakutana na hii:-
CIA.png

From The Express.

Anyway, mimi sio mfuasi wa Conspiracy Theories but I usually respect and trust my inspirational kwa sababu hizi huwa zinatokea bila kufikiria kitu... they just flash into your mind from nowhere, and that's it!!!
 
Yani wabongo mna speculations sana yani sana hadi muda mwingine uwa najiuliza hivi watu uwa mnajishughulisha kusoma?
Hivi kwa bandiko hili unaweza kuconclude kuwa mtu anashawishi mtu ajiunge bitcoin? Hivi unajua kwanini bitcoin inasifiwa? Bitcoin inasifiwa kwasababu ya mfumo yani technology iliyo nyuma ya pesa hiyo inayojulikana kama blockchain ambayo haiwezi kwua tempered.
Hiyo technology inaweza tumika katika mifumo mingne ya kifedha na mikataba ya kidijitali siyo lazima iwe bitcoin na hiyo ndiyo the greatest invention ya huyu jamaa.
Nashangaa ume conclude kwamba anatafutwa mtu kupigwa ela aisee muwe mnajisomea mambo basi yani na hii internet na habari zote unashindwa soma mambo.
 
Hakika leo ndo nimeamini hakuna mwenye wazo jipya la peke yake!!

Yaani from nowhere, huku nikiwa sijawahi kuwaza jambo hilo hata mara moja maishani mwangu, mara wazo likapita tu kichwani mwangu na kuniambia "Hey, listen... we ukiona mambo hayaeleweki eleweki basi, basi jua CIA are behind everything! We unadhani CIA wange-finance vp black ops duniani bila kuwa na confidential means za ku-finance hizo funding"

Nikaona si ajabu wapo waliopata kufikiria kama mimi, na ndipo nikaamua ku-Google "Did CIA Invent Bitcoin?"

Page ya kwanza tu ya search result nikakutana na hii:-
View attachment 1403119

From The Express.

Anyway, mimi sio mfuasi wa Conspiracy Theories but I usually respect and trust my inspirational kwa sababu hizi huwa zinatokea bila kufikiria kitu... they just flash into your mind from nowhere, and that's it!!!
Still ni speculation bado infact hakuna uhakika ni nani hasa alikuwa Bwana Satoshi Nakamoto
 
Still ni speculation bado infact hakuna uhakika ni nani hasa alikuwa Bwana Satoshi Nakamoto
Na ndo maana nikasema mimi sio mfuasi wa conspiracy theories lakini huwa naziamini inspirational zangu kwa sababu ni mawazo yanayotokea tu kichwani unconsciously!
 
Theoretical blockchain ni ngumu kuhack, lakin in reality watu Wana hack Kama kawaida in bugs/loophole nyingi sana, ndo maana recently imeloose momentum
 
Theoretical blockchain ni ngumu kuhack, lakin in reality watu Wana hack Kama kawaida in bugs/loophole nyingi sana, ndo maana recently imeloose momentum
Ni ngumu sana blockchain ndiyo maana walitoa dau la mamilion mtu aihaihack, nalo likaongezwa kila mwaka mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa. Kuhack blockchain lazima uhack 51% ya the entire network which is technically impossible
 
Smart contract watu Wana hack uko wapi
 
Ni ngumu sana blockchain ndiyo maana walitoa dau la mamilion mtu aihaihack, nalo likaongezwa kila mwaka mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa. Kuhack blockchain lazima uhack 51% ya the entire network which is technically impossible
Blockchain ina bugs nyingi mbona iko kitu watu wamekiongelea sana, ndo maana Kuna makampuni Wana remove bugs kwenye blockchain system kuondoa bugs
 
Back
Top Bottom