Huu uzi nimeuanzisha baada kusikia tetesi za minong'ono inayoendelezwa na wana CCM wenyewe. Eti wengi wao wamekasirika kweli kweli wakiwashangaa polisi kwa nini hawaingilii hii mikusanyiko na kuwaadhibu hao ndugu zetu, kwa nini wanaachia hali hii ya utulivu iendelee, kweli?. Mwingine kaenda mbali na kuuliza eti na green guard nao wako wapi, anawataka hata hao waingilie kati kupambana na hao wananchi wanaothubutu kujitokeza kwenye mikusanyiko hii, kweli?
Wananchi wengi wamekuwa wakijiuliza, hivi hao polisi wanakuwa wapi wasiojulikana wanapowateka, kuwatesa na kuwamiminia risasi raia wa nchi hii. Watanzania ambao walijulikana duniani kote kama watu wa amani, wasio na makuu na wakarimu, wamepotelea wapi? Na kweli ukiangalia hii mikusanyiko inayompokea Mh. Tundu Lissu ni wale Watanzania original tuliowafahamu, tulioishi nao, tuliokula nao...je hii Tanzania ya akina Bashite, akina Gambo na wengine wametoka wapi?
Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza...Mtanzania gani anayetishia kuwapiga hadi shangazi zetu? Mtanzania gani anawakebehi ndugu zake waliopatwa na maafa? Mtanzania gani ana ukatili hadi kummiminia risasi zaidi ya thelathini mwakilishi wa wananchi? Maswali ni mengi ndugu zangu. Fikiria mlinda usalama, polisi mtanzania mwenye jeuri ya kuwapiga mama zetu wanaodai haki? Kuwapiga watoto wetu wanaodai elimu bora? Kuwaziba mdomo wasitoe dukuduku zao kama raia wa nchi hii?
Machungu, machungu, machungu...