SoC02 Kitendawili cha utawala bora kwa watawala na viongozi wetu

SoC02 Kitendawili cha utawala bora kwa watawala na viongozi wetu

Stories of Change - 2022 Competition

mosha1997

New Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Neno “Utawala”pekee linaweza kutumika katika fasihi kadhaa, mfano utawala katika ngazi za taasisi (corporate governance), utawala wa kimataifa,(international governance),utawala wa kitaifa, (national governance) lakini pia utawala wa mitaa (local governance).

Utawala bora ni matumizi ya uwezo (mamlaka) wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi; Katika ripoti mbalimbali za utawala bora mfano Kwa mujibu wa ripoti ya Utawala bora na Maendeleo ya Mwaka 1992 iliyofanywa na Benki ya Dunia, “Utawala bora ni matumizi sahihi katika kusimamia uchumi wa nchi na rasilimali za Jamii katika maendeleo”.

Lakini pia utawala bora unaenda sambamba na misingi yake ambayo ni chachu kubwa inayoonesha kuwa kuna utawala bora katika serekali, taasisi za umma au hata taasisi binafsi.

Uwazi: swala la uwazi katika utawala limekua likihimizwa na viongozi wa ngazi zote za serekali lakini japokua hilo halitoshi kusema kwamba serekali imekua na uwazi wa kutosha kwa wananchi wake hasa kwenye mambo ya msingi kama matumizi ya rasilimali za serekali na pesa za umma katika manunuzi na ujenzi wa miondombinu mbalimbali katika ngazi za serekali, lakini moja ya faida kubwa ya uwazi katika utawala bora ni uwajibishwaji pale itakapobainika kuwa kuna tatizo kwenye matumizi ya rasilimali,matumizi ya pesa za serekali, matumizi mabaya ya ofisi za umma au binafsi au hata matumizi mabaya ya madaraka.

Utawala wa sheria;tunakubaliana kabisa kuwa ili kuwe na utawala bora lazima kuwe na utawala ambao unafata sheria na katiba ya nchi , nchi haiwezi kuendeshwa bila ya kufatwa kwa sheria lazima sheria na katiba ambayo ni mama wa sheria zote ifatwe na hapo ndipo tunaweza kusemea swala la utawala bora. lazima yeyote atakaenenda kinyume na sheria awajibishwe iwe ni kiongozi wa serekali kwa ngazi zote kwanzia serekali ya kijiji mpaka serekali kuu taasisi binafsi au za umma na hata mwananchiwa kawaida. Utawala wa sheria unasaidia sana kuondoa rushwa,matumizi ya mabavu na dhana ya haki sawa kwa wote.

Uadilifu; Katika serekali yetu ya Tanzania kwanzia kiongozi mkuu wa serekali yaani raisi na mawaziri wake wamekua wakihimiza sana swala la uadilifu kwa ngazi zote za uongozi waziri mkuu amekua akihimiza hilo katika majukwaa mbalimbali ambayo amepata nafasi ya kuongea na wananchi au hata viongozi wengine wa ngazi za serekali

Uadilifu husaidia nini kwa viongozi? Uadilifu husaidia viongozi kufanya kazi kwa weledi( nadharia na kwa vitendo pia), kufanya kazi kwa kufata misingi yote ya sheria na kutambua kuwa wanayo dhamana ya kuwatumikia wanachi ambao wamewachagua ili kuwa wawakilishi wao katika bunge na ngazi nyingine zote za uongozi katika nchi na taasisi binafsi za za umma.

Usawa; swala la usawa katika utawala bora limekua likihimizwa na viongozi wa ngazi nyingi za serekali waliopita katika misimu kadhaa na hata waliopo madarakani kwa sasa, japokua kwa miaka ya hivi karibuni limeonekana kufanikiwa zaidi kwa mfano serekali yetu ya tanzania tunaongozwa na raisi wa kwanza mwanamke tofauti na kipindi cha nyuma, sasa tunaweza kuona wanawake nao wakipewa nafasi mbalimbali za uongozi na wakafanya vizuri tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilionekana kuwa wanawake hawawezi kuwa viongozi au hawawezi kupewa madaraka katika ngazi za serekali kwanzia kijiji mpaka serekali kuu taasisi binafsi au hata za umma, katika nchi yetu ya Tanzania tunaweza kusema tumefanikiwa kwa asilimia kadhaa japo bado mabadiliko yanahitajika zaidi.

Ushirikishwaji; ndio ni lazima wanachi wote washirikishwe kwenye masuala yote yanayohusu matumizi ya rasilimali za serekali na matumizi ya fedha za umma ni lazima washikishwe kwa kupewa taarifa zote za mapato na matumizi kwa ngazi zote, kwa miaka ya hivi karibuni tunaweza kuona hilo limefanikiwa kidogo tofauti na miaka ya nyuma viongozi wamekua wakiwapa wananchi wake taarifa za mapato na matumizi ya fedha au rasilimali mbalimbali za serekali na imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza swala la rushwa na ubadhilifu wa mali za serekali na wananchi kwa ujumla, Katika hili tunaweza kusema serekali yetu inajitahidi kulifanya hili kwa ngazi zote japokua wapo baadhi ya viongozi wa serekali na taasisi zote binafsi na za umma ambao wamekua wakishindwa kufanya hilo kwa wakati hivyo kuleta sintofahamu kwa wananchi kiujumla.

Uwajibikaji ; viongozi wote wa ngazi za serekali, taasisi za umma au taasisi binafsi wote lazima wawajibike wa uongozi wao na kwa utendaji wao,viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo waziri mkuu amekua akihimiza uwajibikaji wa wabunge mawaziri na viongozi wengine mbalimbali wa serekali katika uongozi wao; tunaweza kuona pia jinsi ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serekali(CAG) inavyowawajibisha wale ambao wameonekana kutowajibika ipasavyo katika uongozi wao japo ni kwa asilimia chache sana sio kwa uongozi wa amamu hii tu bali hata kwa viongozi wa awamu mbali mbali zilizopita.

Misingi hii yote ya utawala bora inaweza kufanikiwa endapo kutakua na mambo mengine muhimu kama katiba ya kidemokrasia, uhuru wa mahakama yaani mahakama iwe huru bila kuingiliwa na serekali au bunge,uhuru wa vyombo vya habari, vyombo vyote vya habari ( vya serekali au binafsi) viwe huru kutoa taarifa zote muhimu kwa wananchi mfano bunge kuwa mubashara kwenye redio na tv ili wananchi wajue ni jinsi gani wawakilishi wao wanavyowawakilisha ,kwa tanzania yetu hili tunaweza kusema limefanikiwa kwa asilimia kadhaa ijapokua bado ni kwa asilimia chache sana kulinganisha na nchi nyingine zilizoendelea;lakini pia lazima kuwe na mgawanyo wa madaraka kwa viongozi wa serekali zote kwanzia kijiji , wilaya ,mkoa na serekali kuu pia hata katika taasisi zote za umma na za binafsi hili lazima lizingatiwe ili dhana ya uwajibiswaji iwepo na iweze kufanya kazi.

Dhana ya utawala bora ni pana sana ambayo inahitaji umakini zaidi ili kuweza kuitekeleza hivyo ni lazima watendaji tuwajibike ipasavyo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyobora na yenye manufaa kwao, na hii si kufanya kazi kwa nadharia bali kufanya kazi kwa vitendo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom