Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
- Thread starter
- #21
Mkuu Nguruvi3 mimi naogopa. Na mimi nakumbuka kipindi ambacho kiongozi moja wa UVCCM alitamka wazi kabisa kuwa wanaompinga Rais Magufuli wauawe. CCM kama chama kilikaa kimya, hakimuonya wala hakimkemea.
Matokeo yake Spika wa Bunge anawataka vijana hao hao wa CCM wamshughulikie yeyote yule watakayemkuta akiwasema vibaya viongozi wa CCM na serikali. Na mimi nasubiri tamko la CCM, chama tawala, je watakaa kimya?
Wengi walitekwa, wengi waliteswa na wengi walipotezwa, kisa? Kupinga au kukosoa kauli tata zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa CCM na serikali. Yupo na mwingine humu humu Jamii Forum kashauri wanaoikosoa hii serikali wachukuliwe hatua.
Pamoja na hayo leo kama wasemavyo wahenga a light appeared at the end of a long dark channel. Spika tulia kwa kujisahau au kulewa madaraka kawataka vijana hao kuwanyoosha eti wanaowasema vibaya viongozi ikiwa ni pamoja na yeye kama awali.
Kumbe walioitwa wasiojulikana yawezekana walikuwa wakitekeleza miongozo waliyokuwa wakipewa na chama chao...kuwanyoosha wapinzani wao. Wapo walionyoshwa wakapona na wapo walionyoshwa wasiamke tena , Munge walaze pahala pema peponi!