Kitendawili cha wasiojulikana hatimaye kimeteguliwa na Spika Tulia?

Kitendawili cha wasiojulikana hatimaye kimeteguliwa na Spika Tulia?

Kwa taarifa yako hiyo nyooka naye ni kuwafanyia ukatili wanaowasema. Na hata angesema wawaue wanaowasema vibaya, kwa mahakama hizi asingefanywa lolote. Lakini ingetokea mpinzani kasema hivyo, mahakama ingemtia hatiani mara moja! Usitegemee haki yoyote kwenye mahakama hizi ambazo ni sehemu ya huu utawala wa double standard mbele ya sheria.
Hii kauli naona unaitumia kwasababu ya precedence ya matendo ya CCM kwa upinzani, umetumia matukio yaliyopita kupata hili jibu, sasa ili tupate na jibu la kauli ya Tulia, naona tunatakiwa kusubiri action, kama itakuwa ni kujenga hoja, au vipigo ili tuanze kumhukumu vizuri Tulia kwa hiyo kauli yake.
 
Na hao vijana watakuwa wameelewa hivyo kama ulivyoeleza? "Nyooka naye", vijana wenye vuguvugu la damu watafsiri ni "kujibu hoja", watu wasiojuwa kujenga hoja?
Naona tusubiri matokeo ya hiyo kauli ndio tuanze kuhukumu, tunaweza kuhukumu sasa tukawa tunawanyima haki yao ya kujitetea kwa hoja pale watakapotakiwa kufanya hivyo, japo kwa upande mwingine hiyo subira inaweza kuleta balaa pale itakapothibitika hiyo kauli imetumika vibaya...
 
"Nyooka nae"

Lakini hiyo tungo ni tata, hata akipelekwa mahakamani sidhani kama atafungwa, na inawezekana alijua ndio maana akaitumia.

Inaonekana wengi wanaitafsiri kwa namna wanavyoona/taka wao, hasa kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyopo kati ya CCM na wapinzani.

Lakini hiyo pekee kwangu naona haitoshi kumtia hatiani Tulia pale atakapotakiwa kujitetea.

Anaweza kusema "nyooka nae" alimaanisha kuwaambia vijana wa CCM wajibu hoja kwa hoja, sasa nani ataweza ku prove vinginevyo?
Waswahili wanasemaga Fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung’amua. !!
 
Hii kauli naona unaitumia kwasababu ya precedence ya matendo ya CCM kwa upinzani, umetumia matukio yaliyopita kupata hili jibu, sasa ili tupate na jibu la kauli ya Tulia, naona tunatakiwa kusubiri action, kama itakuwa ni kujenga hoja, au vipigo ili tuanze kumhukumu vizuri Tumia kwa hiyo kauli yake.

Uko sahihi kabisa kuwa nimetumia matukio ya zamani, tena sio zamani bali ni majuzi tu. Je unadhani tabia hizo zimekoma au ni kwakuwa wapinzani wako kwenye silent mode? Juzi juzi hapa kuna kijana wa ccm ametrend akihamasisha uovu, tena akawa anatamba wao watafanya yao, kisha viongozi watabeba jukumu la kuwaombea msamaha. Je kuna hatua yoyote kachukuliwa?
 
Hapa tena naona mambo mawili, kuna kufanya kwa kujiamulia watu binafsi, kama huo mfano wa tukio la juzi juzi ulilotoa, hao wahusika hatujui walitumwa na nani.

Halafu kuna kufanya kwa kutumwa, hii ndio itakuwa applicable pale hao jamaa wa Mbeya na maeneo mengine watakapokwenda kufanya waliyotumwa na boss wao, ngoja tuone..
 
Tulia atakiwa kufahamu kuwa; kila ubaya hulipwa kwa ubaya, ameamua kuwa mlezi na mfadhili wa ubaya ila mkono wa Mungu utalipa ubaya huo!
 
Halafu kuna kufanya kwa kutumwa, hii ndio itakuwa applicable pale hao jamaa wa Mbeya na maeneo mengine watakapokwenda kufanya waliyotumwa na boss wao, ngoja tuone..
Ndugu yangu denooJ naona unataka kufunika kombe mwanaharamu apite, hebu jiulize...kauli kama hiyo ingetolewa na upande mwingine, je kungekalika? Wangapi wangekuwa wameshakamatwa na kuwekwa ndani hadi dakika hii?

Je tungoje tuone nini? Huoni hao CCM wamenyamaza kimya utafikiri hawapo? IGP hadi sasa kimya, msajili wa vyama kimya na serikali kwa ujumla wale kimya...je tafsiri gani unaipata hapo? Au tusubiri hadi tuone watu wakipotezwa?

Heri kuzuia kuliko kuponya! Spika Tulia, ili kuonesha unajali utawala unaozingatia na kuheshimu sheria, jiuzulu. Kuendelea kwako kukalia kiti hicho ni kwamba na wewe hujali kama ilivyo kawaida ya wenzako waliolewa madaraka.
 
Ah hapana, nimeona nyuzi nyingi tu kuhusu hili, sikucheki mapema. Watu wa kutishwa wapo na mimi siko katika hiyo list ndugu yangu. Kilichonisukuma ni wale vijana wa UVCCM walivyokuwa wanamshangilia huyo SPIKA TULIA!

Ni kama vile wana kiu ya damu ya mtu! Hapo hapo nikawakumbuka wale WASIOJULIKANA, nikajisemea ebo kumbe ndio maana vyombo vyetu vya usalama vilipatwa na kigugumizi kushughulikia utekaji, utesaji na upotezwaji!

Labda zilikuwa ni maagizo kutoka juu.
Mimi nilijiuliza maswali mengi kuhusu Spika Tulia,msomi wa sheria, wakili na mhadhiri wa zamani wa UDSM kuongea lugha za makamanda wa Interahamwe wa Rwanda!!! Baadaye nilianza kuelewa alivyo toka mbio ktk utumishi wa umma na kwenda gombea Uspika! Kumbe haya ndiyo majembe ya bwana mkubwa wa awamu ya 5!!! Spika wa Bunge la Taifa anawezaje kuhutubia hotuba kama ile kwa vijana semi illiterate???
Mama Samia na mzee Kinana tafadhali tuondolee haya majoka yaliyo jificha CCM!
 
Hili la Tulia ni hatari sana Rais SSH 'wakianza kunyooshana' tatizo litatua mezani mwako! kama Tulia hana baraka za CCM tafadhali fanya la maana kwa masilahi ya Nchi. Tulia must go !

Kama kauli za Tulia zina baraka za CCM basi mwacheni aendelee na uongozi lakini siku kauli yake ikianza kufanya kazi (mungu tujalie yarabi yasitokee) basi sote tutawaambia ! hamkusikia Tulia akichochea kuni?
Huyo binti ni mteule wa Magufuli.

Magufuli alikuwa na kipaji cha kuwapata watu wa aina yake, watu kama Sabaya.

Kuhusu Samia na CCM kukemea haya, sidhani. Inavyoonekana ni kama mkakati wao wa kuwapumbaza waTanzania. Vichaa wanafanya yao kwa njia zao kukifaidisha chama, huku Samia akipulizia kivyake kama panya, bila kuchukua hatua thabiti, ili wananchi waone kama hayo ya vichaa hayampendezi, lakini akifaidika na matokeo ya kazi zao.

Hapana, mkuu 'Nguruvi3', sote tunaitakia nchi yetu Tanzania amani na maelewano kati yetu, lakini nadhani wakati umefika sasa wasilichukulie hili jambo kuwa kama ndiyo kinga yao ya kuendelea kuchafua nchi yetu. Machafuko kama yatakuwepo, ni matokeo ya mambo yanayofanywa na CCM na viongozi wao. Hawa ndio wanaostahili kulaumiwa ikifika watu kushindwa kuvumilia manyanyaso dhidi yao.

Binafsi sipendi vurugu, lakini nimeishiwa na uvumilivu. Nitaunga mkono kundi lolote litakalojitokeza kukataa kwa njia yoyote huu upuuzi unaofanywa na CCM.
 
Naona tusubiri matokeo ya hiyo kauli ndio tuanze kuhukumu, tunaweza kuhukumu sasa tukawa tunawanyima haki yao ya kujitetea kwa hoja pale watakapotakiwa kufanya hivyo, japo kwa upande mwingine hiyo subira inaweza kuleta balaa pale itakapothibitika hiyo kauli imetumika vibaya...
EeeeNheeee, mkuu 'denooJ', ni kama unaamua maksudi mazima kujitoa akili, lakini hiyo ni haki yako.
Tusubiri hadi watakapotoa utetezi wao. Juu ya jambo gani watatakiwa kutoa utetezi wao?
Tundu Lissu hadi leo anasubiri kupata majibu, huo ni mfano mmoja tu; na huwezi kutafuta mfano ulio hai zaidi ya huo unaosubiri majibu, lakini hakuna anayetaka kujibu!
 
Kanuni ya siku zote ni ileile , KILA UBAYA UTALIPWA
Haijalishi iwe kwa Corona, Malaria au mkono wa Mungu moja kwa moja

Kuna wakati janga au balaa linaweza kuwa ni ponyo au uokovu kwa jamii nyingine

Asante Corona ilituponya na balaa tulilokuwanalo watanzania hebu just imagine angukuwepo na vita hii si ingekuwa balaa kilo 100
 
Hapa tena naona mambo mawili, kuna kufanya kwa kujiamulia watu binafsi, kama huo mfano wa tukio la juzi juzi ulilotoa, hao wahusika hatujui walitumwa na nani.

Halafu kuna kufanya kwa kutumwa, hii ndio itakuwa applicable pale hao jamaa wa Mbeya na maeneo mengine watakapokwenda kufanya waliyotumwa na boss wao, ngoja tuone..
CCM kimyaa
IGP Kimyaa
Waziri wa mambo ya ndani kimyaa
Msajili wa vyama vya siasa kimyaa

Unahitaji kujua nini zaidi?

Hili jambo si la Tulia, yeye ni kipaza sauti . Kwa ujumla lina mikono mingi na baadhi ni hiyo hapo juu
 
Ndugu yangu denooJ naona unataka kufunika kombe mwanaharamu apite, hebu jiulize...kauli kama hiyo ingetolewa na upande mwingine, je kungekalika? Wangapi wangekuwa wameshakamatwa na kuwekwa ndani hadi dakika hii?

Je tungoje tuone nini? Huoni hao CCM wamenyamaza kimya utafikiri hawapo? IGP hadi sasa kimya, msajili wa vyama kimya na serikali kwa ujumla wale kimya...je tafsiri gani unaipata hapo? Au tusubiri hadi tuone watu wakipotezwa?

Heri kuzuia kuliko kuponya! Spika Tulia, ili kuonesha unajali utawala unaozingatia na kuheshimu sheria, jiuzulu. Kuendelea kwako kukalia kiti hicho ni kwamba na wewe hujali kama ilivyo kawaida ya wenzako waliolewa madaraka.
Siwezi kuwafunikia kombe hao wanaharamu, nachojaribu kuandika hapa ni kutoa maoni yangu tu, binafsi nimeona hiyo kauli ya Tulia ina utata, hivyo kwangu ningependa badala ya watu kuanza kumshambulia moja kwa moja kama inavyotokea, angalau apewe nafasi ya kuifafanua kwanza.

Lakini kwenda mbali na kumtaka ajiuzulu, kwa sababu ya kutoa kauli yenye utata, kwangu naona atakuwa amehukumiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea, kitu ambacho sio sahihi kulingana na kanuni ya principles natural justice.
 
CCM kimyaa
IGP Kimyaa
Waziri wa mambo ya ndani kimyaa
Msajili wa vyama vya siasa kimyaa

Unahitaji kujua nini zaidi?

Hili jambo si la Tulia, yeye ni kipaza sauti . Kwa ujumla lina mikono mingi na baadhi ni hiyo hapo juu
Kwanini nisiamini ukimya wa hao watu umesababishwa na kutoiona hatari iliyopo kwenye kauli ya Tulia?

Kwasababu kwangu ile tungo ni tata; "Nyooka nae".

Kama nyie mmeona ile kauli ina hatari na kumtaka ajiuzulu, au kufukuzwa, basi wengine kwa kutumia utata wa ile kauli wameona vinginevyo, nao wanastahili kuheshimiwa mawazo yao, wala sio kuwashangaa.

Binafsi, kama Tulia angesema direct "waueni", au "wapigeni", hapo ningeungana nanyi kumlaani kwa kauli yake, lakini sio kwa ile tungo tata, ambayo sasa naona kama inatumika kisiasa kuipatia majibu tuyapendayo.
 
Utata uko wapi ndugu yangu, Spika Tulia kawaagiza hao vijana yeyote yule atakayekutwa anamsema vibaya kiongozi yeyote wa chama na serikali ashughulikiwe.

Akikazia amewataka wamshughulikie yeyote atakayekutwa akihoji utendaji wake yeye binafsi! Kwa kweli naogopa.
Mimi nimemsikia kwa video clip akisema "Nyooka nae" hiyo ya ashughulikiwe sijaiona, kama unayo tuwekee hapa tumalize utata.

Naona mnatumia matukio yaliyopita kuhukumu yaliyopo, ndipo mnapokosea.
 
Kwanini nisiamini ukimya wa hao watu umesababishwa na kutoiona hatari iliyopo kwenye kauli ya Tulia?

Kwasababu kwangu ile tungo ni tata; "Nyooka nae".

Kama nyie mmeona ile kauli ina hatari na kumtaka ajiuzulu, au kufukuzwa, basi wengine kwa kutumia utata wa ile kauli wameona vinginevyo, nao wanastahili kuheshimiwa mawazo yao, wala sio kuwashangaa.

Binafsi, kama Tulia angesema direct "waueni", au "wapigeni", hapo ningeungana nanyi kumlaani kwa kauli yake, lakini sio kwa ile tungo tata, ambayo sasa naona kama inatumika kisiasa kuipatia majibu tuyapendayo.
Utata wa kauli ndilo tatizo kwasababu wapo wanaotafsiri ni kuua, wapo wanaosema ni kupoteza na mleta mada kasema 'wasiojulikana' wengine wana tafsiri hakuna shida

Hawa wanaosema hakuna tatizo si habari kwasababu hakuna tatizo. Tatizo ni hawa wanaotfasiri kwa mtazamo mwingine hasa ukizingatia miaka 6 iliyopita ilivyokuwa. Watu wanakumbu kumbu za akina Kenan Kihongosi na Heri james, wanakumbuka akina Sabaya , wanakumbuka viroba na maiti kutoka south Africa mto Ruvu.
TL alifuatiliwa na gari wakasema hakuna tatizo leo tunajua kilichomkuta

Ikiwa basi kauli hiyo sivyo ilivyo kwanini
CCM hawatoki na kuitetea kwamba haina tatizo wakijua imetolewa na mjumbe wa kamati kuu tena iliyokaa hivi karibuni?
Kwanini Msajili asitoke na kufafanua kama haina utata ? Je angeitoa mwana CDM leo ingaliwakuwaje?
Kwanini IGP asijitokeze na kuwahakilishia watu kuwa kauli hiyo ni safi tu haina shida

Kauli ya Spika inahamasisha vurugu nchini! Alipaswa awe amejiuzulu
 
Thubutu! Kama Madelu, pamoja na kusimamia wizi na kauli chafu, hakujiuzulu wala kuwajibishwa, itakuwa huyu Tulia! Naona huwajui CCM, pamoja na jeuri na dharau yao kwa wananchi, hajiuzulu mtu. Kama nafasi ya juu zaidi ingekuwepo, si ajabu angepandishwa cheo!
Na akitokea amejiuzulu ujue so called system ya ccm haimtaki au haja match character na aliye pale juu.a vivid example ni mtangulizi wake ndugai.
 
Back
Top Bottom