Kitendo cha IGP Sirro kutoa hukumu ya Ugaidi wa Mbowe huku kesi ikiwa Mahakamani ni Uhalifu. Napendekeza kesi hiyo ifutwe haraka

Kitendo cha IGP Sirro kutoa hukumu ya Ugaidi wa Mbowe huku kesi ikiwa Mahakamani ni Uhalifu. Napendekeza kesi hiyo ifutwe haraka

Wote bila shaka mmemsikia Mkuu wa jeshi la Polisi wa Tanzania Mtukufu IGP Simon Sirro , kauli yake hii ni sawa na kulazimisha mahakama kutenda ayanenayo.

Sirro anafahamu kwamba Sheria inakataza yaliyo Mahakamani kujadiliwa vijiweni , na hasa kama anayejadili ana maslahi kwenye kesi iliyo mahakamani , kama yeye Sirro alivyo na maslahi binafsi kwenye kesi hii , lakini ameamua kupuuza ili kumrahisishia maamuzi hakimu wao wanayemtumia kumkomoa Mbowe na Chadema...
Ni kweli IGP huwezi kuongelea mambo kama vile wewe ni mahakama. Kesi ikishaenda mahakamani inatakiwa kufuata utaratibu
 
Me nafikiri Simon Sirro kaeleweka vizuri sema wewe na baadhi ya watu ndio mnakaza fuvu,hivi kwani Mbowe hawezi kufanya uhalifu?

Kwa mujibu wa Sirro Mbowe alijaribu kushawishi baaadhi ya vijana waliofukuzwa jeshini waungane na yeye kwa namna ya kupingana na serikali, na amedai Wana ushahidi kwahiyo kama una bisha ,nenda na ushahidi wako utakaomtetea na sio kupinga kwa thread tu.
 
Kwenye nchi ya watawala walio wastarabu wanaofuata misingi ya haki na sheria tayari kesi hii ni VOID.
Ila ya Sabaya ilipojadiliwa kwenye vijiwe bado haijawa VOID sio? Au kisa anaejadiliwa hapa ni Mbowe?

Tulieni sasa.
 
Taratibu ni kuulize...Hivi mtu anaedai haki yake..Katiba siku hizi ni kuleta fujo?
Hivi kumbe ata Mwl.Nyerere alikua anavuruga amani kwa kuwapinga Makaburu!?
Kuunda njama na vijana wa waliofukuzwa jeshini nayo ni madai ya katiba sio?
 
Wote bila shaka mmemsikia Mkuu wa jeshi la Polisi wa Tanzania Mtukufu IGP Simon Sirro , kauli yake hii ni sawa na kulazimisha mahakama kutenda ayanenayo.

Sirro anafahamu kwamba Sheria inakataza yaliyo Mahakamani kujadiliwa vijiweni , na hasa kama anayejadili ana maslahi kwenye kesi iliyo mahakamani , kama yeye Sirro alivyo na maslahi binafsi kwenye kesi hii , lakini ameamua kupuuza ili kumrahisishia maamuzi hakimu wao wanayemtumia kumkomoa Mbowe na Chadema...
kwa sasa wacha Mbowe apambane na hali yake.
 
siyo rahisi kama unavyofikiria kama mdude ameshatulizwa itakuwa wewe?
Kila mtu anamnyonge wake ,igp hana watoto ,hana mke ,muda ukifika Kila mtu atapata uchungu tusiombee taifa lifike huko tendeni haki ,haki huinua taifa
 
Kama vyama vya siasa na makundi mengine nao wakisema wanao ushahidi wa kutosha kuhusu Mheshimiwa Mbowe kama anavyosema IGP Simon Sirro kuwa anao ushahidi wa kutosha; ni nani atakuwa anaiingilia Mahakama katika kesi hiyo? Hivi anayetakiwa kuyaonya makundi kutokuingilia kesi iliyopo Mahakamani ni Mahakama yenyewe au ni IGP Simon Sirro?

Kama Jeshi la Polisi wanao ushahidi wa kutosha, kwa nini wasikae kimya? Anayemshitaki Freeman Mbowe kwa Ugaidi ni Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro au ni Jamhuri ikiwakilishwa na DPP? Atakayewasilisha ushahidi Mahakamani ni IGP au ni Timu ya DPP? Hivi IGP Simon Sirro, ana maslahi gani na Kesi ya Mbowe zaidi ya kutimiza jukumu la kumkamata?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Kama vyama vya siasa na makundi mengine nao wakisema wanao ushahidi wa kutosha kuhusu Mheshimiwa Mbowe kama anavyosema IGP Simon Sirro kuwa anao ushahidi wa kutosha; ni nani atakuwa anaiingilia Mahakama katika kesi hiyo?...
I hope Samia bado hajaichafua/pollute judiciary and justice will be served...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Aigipii anaogopa mkusanyiko wa watu 05/08/2021.
Tufanye anachoogopa.
Twendeni tukahesabiwe.
 
My hope is too low Mkuu. Let’s wait and see but taking into consideration of what happened the last 5+ years I am worried about this FAKE case against Mbowe.
I hope Samia bado hajaichafua/pollute judiciary and justice will be served...
 
Back
Top Bottom